Mtu mmoja ameuawa katika mapigano kati ya wanafunzi wanaokiunga mkono Chama cha Muslim Brotherhood na wakazi jijini Cairo nchini Misri, maafisa wameeleza.Maafisa mjini humo wamesema kuwa mwanafunzi mmoja alipoteza maisha baada ya pande hizo mbili kushambuliana kwa risasi katika mji wa Nasr.Tukio hilo limetokea siku moja baada ya Serikali ya Misri kukitaja chama cha Muslim Brotherhood kuwa kundi la kigaidi.Katika tukio jingine, watu watano wamejeruhiwa kwa bomu lililokuwa karibu na basi moja mjini Nasr, bomu hilo lilitegwa na kulipuka wakati basi hilo lilipokuwa likipita karibu na eneo lilipotegwa bomu.Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na tukio hilo.Siku ya alhamisi, takriban wafuasi 16 wa chama cha Muslim Brotherhood walikamatwa wakishutumiwa kujihusisha na kundi hilo linalodaiwa kuwa la kigaidi.Miongoni mwa waliokamatwa ni Mtoto wa Naibu Kiongozi wa Chama hicho.Shirika la Habari la Misri, Mena limesema Watu hao walikamatwa na kushutumiwa kuchochea machafuko na mapigano dhidi ya Jeshi na Polisi.Siku ya jumanne, Watu 16 waliuawa na zaidi ya 100 walijeruhiwa katika shambulio la bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari katika jengo la usalama mjini Mansoura, Maafisa wameeleza.Serikali imesema kuwa Muslim Brotherhood inahusika na shambulio hilo, madai ambayo yamepingwa vikali na Chama hicho.Kundi lenye uhusiano na Al Qaeda, Ansar Beit al-Maqdis (washindi wa Yerusalemu) walikiri kuhusika na shambulio hilo.
KUANZISHWA KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA Mafanikio ya michuano ya mpira wa miguu ya Olimpiki ndiyo yalikua mwanzo wa FIFA kutamani kuwa na michuano yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo wa mpira wa miguu. Ikumbukwe kwamba kipindi hicho mpira wa miguu wa wanaume pekee ndiyo ulikuwepo. Maswali yalitumwa kwa wahisani wa FIFA ili kuona kama wanakubaliana na uanzishwaji wa michuano hiyo na kwa masharti yapi? Kamati maalumu ilichunguza maswali hayo chini ya uongozi wa Rais wa FIFA wa kipindi hicho Jules Rimet akishirikiana na Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa kwa wakati ule Henri Delaunay. Rais wa FIFA Jules Rimet aliyeanzisha na kusimamia Kombe la Dunia la kwanza . Kufuatia uwepo wa muswada wa Kamati Tendaji ya FIFA, lilifanyika kongamano la FIFA Mei 28, 1928 jijini Amsterdam nchini Uholanzi likiazimia kuwepo kwa michuano ya mabingwa wa soka duniani ambayo ilipangwa na shirikisho hilo la mpira duniani na sasa nchi waandaji wa michuano hiyo zilitakiwa ...

Comments
Post a Comment