Posts

Showing posts from November, 2016

TATHIMINI KWA UFUPI CHELSEA vs EVERTON KABLA YA MECHI SAA 2:30 EAT

Image
Timu hizi mbili zimekutana katika michezo 49 ambapo Chelsea imeshinda mechi 22 na Everton imeshinda mechi 10 na kudroo mechi 17. Chelsea imeshinda nyumbani mechi 13 wakati Everton imeshinda mechi 9. Nje, Chelsea imeshinda mechi 9 wakati Everton imeshinda 2. Katika mechi 3 zilizopita Chelsea ilifungwa na Everton magoli 2 kwa nunge, hii ilikuwa mechi ya Machi 12, 2016. Lakini pia mechi ya Januari 16, 2016 timu hizi zilitoka sare ya magoli 3. Na ile ya Septemba 12, 2015 Chelsea alipigwa magoli 3 kwa 1. Katika msomu huu Chelsea ipo katika nafasi ya 4 wakati Everton ipo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa Ligi. Chelsea imeshinda 70% ya mechi ilizocheza huku Everton ikishinda 50%. Mechi za nyumbani Chelsea ina asilimia 80% dhidi ya mpinzani wake Everton 50% huku mechi zilizopigwa nje Chelsea ana 60% na Everton 40%. Chelsea ina wastani wa 2.1 katika magoli iloshinda wakati Everton ana wastani wa 1.5 Lakini pia Chelsea imefungwa wastani wa 0.9 wakati Everton ina 0.8.

TAHLISO YATOA WIKI MOJA KWA SERIKALI KUTOA MIKOPO

Image
Shirikisho la serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) limetoa muda wa wiki moja kwa wanafunzi waliokosa mikopo licha ya kuwa na vigezo vyote ikiwemo uhitaji kusikilizwa na serikali kabla hatua nyingine hazijachukuliwa. Tamko hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa shirikisho hilo Bwana Stanslaus Peter, katika kikao cha pamoja kilichohusisha marais wa vyuo vyote nchini, waliokutana Jijini Dar es Salaam leo, kujadili sintofahamu inayowakumba wanafunzi wanaojiunga mwaka wa kwanza katika vyuo mbalimbali nchini. Stanslaus amesema kuwa kuna kundi kubwa la wanafunzi ambao wameondolewa kwenye orodha ya wanufaika, na wengine kunyimwa kabisa ama kwa visingizio au bila sababu, jambo linalowafanya waishi katika mazingira magumu na kuhatarisha hatma yao kimasomo. Amesema wamekubalina kuwa, endapo serikali haitafanyia kazi ombi hilo ndani ya wiki moja, basi shirikisho hilo litachukua hatua ikiwa ni pamojana kuhamasisha wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

Image
Google Inc. kupitia teknolojia yao ya Android wanakuja na Version nyingine 7.0 na 7.1 Android Nougat. Katika historia ya version za Android zilizowahi kuwagunduliwa version ya Kwanza ilikuwa Android Alpha 1.0 ya mwaka 2007. Hapo katikati zikaletwa Zombie Arts, Jeally Bean, KitKat, Lollipop na Mashallow. Sasa ni zamu ya Android Nougat. TUANGALIE SIFA ZA ANDROID NOUGAT 7 Android Nougat ipo kwa ajili hako. Ina njia nyingi za kufanya uhisi teknolojia hii ni ya kwako. Kwa mujiu wa Android, Nougat ni toleo zuri kuwahi kutolewa katika teknolojia hii. 1. Ni Mfumo wa Uendeshaji (Operating System, OS) unaotumia lugha yako. Inayasogeza karibu maneno ya lugha yako ikiwa na emoj mpya na uwezo wa kutumia lugha 2 kwa wakati mmoja. Ina zaidi ya emoj 1500 ikijumuisha emoj mpya 72. 2. Inakuruhusu kufanya mambo 2 kwa wakati mmoja. Sasa unaweza kutumia vitumizi viwili (applications) kwa kugusa mara mbili (double trap) na kutumia vitumizi viwili pande mbili. Kwa mfano, unaweza

BATCH 4 WALIOCHAGULIWA MZUMBE (DEGREE, DIPLOMA, CERTIFICATE & TRANSFER)

Image
Yafuatayo ni majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu Mzumbe kwa awamu ya 4 kwa mwaka 2016/2017. Pia yapo na majina ya waliohamishwa kutoka kwingineko kwenda Mzumbe. 👉BOFYA HAPA KUONA NA KUPAKUA MAJINA HAYO👈

SIMBA YAZIONYA AFRICAN LYON NA PRISONS

Image
Nahodha wa Simba, Jonas Mkude amesema ari waliyokuwa nayo hivi sasa ana uhakika wa kupata pointi sita nyingine kwenye mechi mbili zilizobaki kabla ya kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara. Akizungumza na gazeti hili jana, Mkude alisema pointi sita walizozipata Shinyanga dhidi ya Mwadui na Stand United, zimedhihirisha ubora waliokuwa nao msimu huu na atahakikisha wanaendelea na kasi hiyo ili kutimiza kile ambacho wamekikusudia. “Lengo ni ubingwa na kwakuwa tunautaka ubingwa kwanza lazima tumalize kinara kwenye mzunguko wa kwanza kwa kuchukua pointi zote sita kwenye michezo yetu miwili iliyobaki na baadaye tujipange kwa ajili ya mzunguko wa pili,” alisema Mkude. Simba imebakiwa na mechi dhidi ya Africany Lyon na Prisons. Mkude alisema anafurahi kuona kila mchezaji ndani ya kikosi chao akicheza kwa kujituma na kufuata kikamilifu maelekezo kutoka kwa wakuu wa benchi lao la ufundi na anaamini ari hiyo itaendelea hadi mwishoni mwa msimu huu na hatimaye kuwa mabingwa. “Hatuja

SERIKALI IMEPELEKA TSH. BILIONI 177 KWENYE HALMASHAURI ZA WILAYA

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali imepeleka katika halmashauri nchini Sh bilioni 177 Oktoba mwaka huu kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Aidha, amempongeza Rais John Magufuli, kwa kufikisha siku 365 za kuwapo madarakani na mafanikio makubwa ya utawala wake tangu alipopewa na Watanzania ridhaa ya kuwa Rais wa Tano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana. Licha ya pongezi zake, amewaomba Watanzania waendelee kumuunga mkono Rais Magufuli ili afanikishe zaidi dhamira yake njema ya kuwatumikia wananchi. Majaliwa aliyasema hayo bungeni mjini Dodoma ambapo alizungumzia mambo mbalimbali katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu. Akizungumzia suala la fedha kupelekwa katika halmashauri, alisema serikali imechukua muda kupeleka fedha mara baada ya bajeti kupitishwa na Bunge kwa kuwa ilitaka kufanya mambo muhimu ya kujiridhisha. Aliyaja maeneo muhimu ambayo serikali ilitaka kuyafanyia kazi kabla ya kupeleka fedha kuwa ni kujiridh

WAHAMIAJI 239 WAHOFIWA KUZAMA KATIKA AJALI YA MELI WAKITOKEA LIBYA

Image
Wahamiaji 239 wamehofiwa kuzama katika ajali ya meli wakitokea nchini Libya. Hii ni kwa mujibu wa habari kutoka shirika la Wakimbizi UNHCR. Msemaji wa UNHCR mjini Roma Italia amesema kuwa taarifa hizo zimethibitishwa na manusura wa ajali walipofikishwa katika ukingo wa bahari katika kisiwa cha Lampedusa. Mpaka sasa hakuna ambaye amekwishapatikana katika hao 239. Sami alisema kuwa watu 31 wamenusurika katika ajali za meli mbili zilizopata ajali baharini kufuatia dhoruba kali. Walisema kuwa watu 29 walinusurika katika meli ya kwanza huku wengine 120 hawajulikani walipo. Katika jitihada za kuokoa watu, wanawake 2 waliokuwa wakiogelea kujinusuru waliwambia waokoaji kuwa watu hao 120 walikufa katika meli hiyo. Katika matukio yote mawili, wengi wa wahamiaji hao wanaonekana kuwa ni raia kutoka eneo la Jangwa la Sahara. Leonard Doyle, msemaji mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) amesema kuwa watu 4,220 wamepoteza maisha katika mwaka huu 2016 kwenye ajali za meli katik

OBAMA AWATAHADHARISHA WAPIGA KURA KUHUSU TRUMP

Image
Rais Barrack Obama amewahimiza wafuasi wa chama cha Democratic kumpigia kura Hillary Clinton na kuonya kwamba Donald Trump ni tishio kwa haki za kijamii, taifa la Marekani na dunia nzima kwa ujumla. Rais wa Marekani Barrack Obama amewahimiza wafuasi wote wa chama cha Democratic kumpigia kura kwa wingi Hillary Clinton siku ya uchaguzi wiki ijayo na kuonya kwamba Donald Trump mgombea urais wa chama cha Republican ni tishio kwa haki za kijamii ambazo ziliafikiwa kupitia hali ngumu , taifa la Marekani na dunia nzima kwa ujumla. Akigusia chaguo la rais siku ya Jumanne wiki ijayo, rais Barrack Obama alimpuuzilia mbali Trump kuwa mtu asiyestahili kabisa kuwa rais. Kufikia sasa Clinton bado anaonyesha uwezekano wa kuwa rais wa 45 wa Marekani lakini huku zikiwa zimesalia siku sita kabla ya uchaguzi huo mkuu, wafuasi wa chama cha Demokratic bado wako chonjo hasa kutokana na mienendo ya Trump isiyotabirika. Obama aliwaambia wapiga kura katika mji wa Chapel Hill kuwa hatima ya taifa h