WANASAYANSI WAGUNDUA UHAI KATIKA SAYARI YA SATURN
Sayari ya Sarateni "Saturn" Mwezi wa Enceladus ambao uko kwenye sayari ya Saturn huenda ukawa mahali bora zaidi pa kwenda kutafuta maisha nje ya dunia. Tathmini hii inatokea kufuatia uchunguzi katika sayari hiyo yenye kilomita 500 uliofanywa na Cassini. Uchambuzi wa kemia wa Cassini unaonyesha matundu ya maji moto kwenye sakafu ya bahari ya Enceladus, maeneo ambayo yanahusishwa na kuwepo kwa maisha, hapa duniani. Kuwepo kwa maji haya sio thibitisho kamili kwamba vitu vilivyo na uhai vinaishi katika mwezi huo mdogo lakini teknolojia zinaweza kutumika kupima maji hayo na kutoa ushahidi zaidi. "Tuna uhakika kuwa kitu chenye uhai kinaweza kuishi kwenye bahari ya Enceladus lakini lazima tufanye utafiti zaidi," alisema mwanasayansi wa Cassini kutoka Taasisi ya Utafiti ya Southwest, San Antonio, Dkt. Hunter Waite. "Iwapo hakuna maisha huko, ni sawa, lakini ikiwa maisha yapo itakuwa bora zaidi," alieleza BBC. Bahari iliyopo kwenye En...