GOODALL MWANASAYANSI WA AUSTRALIA (104) AMEJITOA UHAI WAKE NCHINI USWISI
Mwanasayansi David Goodall, 104, aliyesafiri kutoka Australia hadi Uswisi ili kujitoa uhai amefariki katika kliniki moja nchini Uswisi, shirika linalotetea haki za watu wanaotaka kufa limetangaza. Mwanaikolojia huyo ambaye pia alikuwa mtaalamu wa mimea hakuwa anaugua lakini alisema aliamua kujitoa uhai kutokana na kudhoofika kwa 'ubora wa maisha yake'. Goodall mwaka 1984 enzi za ujana. Bw Goodall alikuwa amezua mjadala kutokana na safari yake ya kutoka Australia kwenda kujitoa uhai. Muda mfupi kabla ya kifo chake, alisema alikuwa na "furaha kuhitimisha" maisha yake. "Maisha yangu yamekuwa dhaifu sana kwa mwaka mmoja hivi uliopita na hivyo basi nina furaha kuyahitimisha," alisema akiwa amezingirwa na jamaa wake kadhaa. "Nafikiria, kuangaziwa kwa kisa changu kutachangia kutetea haki za wazee kuruhusiwa kujitoa uhai, jambo ambalo nimekuwa nikitaka." Mtazame Goodall katika video hii hapa chini: Alifari...