Alive -“Hii ni hadithi ya kweli ya Vast Bracket, safari yake hadi alivyopona kansa mwaka 2013. Huu ni wimbo wa shukrani kwa kumfanya mshindi aliyeishinda kansa.” Hayo ni maneno yanayoonekana mwanzoni mwa video ya wimbo mpya ya kundi la Bracket kutoka Nigeria iliyotoka wiki hii, ambao wamemshirikisha Diamond Platnumz na Tiwa Savage. Kipindi Vast anaumwa kansa Memba wa kundi hilo aitwaye Vast, mwaka 2013 alikuwa akipigania uhai wake baada ya kuugua kansa ya damu ambayo baadae alifanikiwa kupona, ndio sababu ya kundi hilo kuamua kurekodi wimbo huu ‘Alive’ kwaajili ya kumshukuru Mungu kutokana na kumuwezesha msanii huyo kupona. Vast ni yule ambaye anaimba vesre ya kwanza na kwenye video anaonekana yupo hospitali. Video hii hapa Vast aliwahi kuelezea jinsi alivyougua hadi kupona katika mahojiano mbalimbali aliyofanyiwa 2013: “It all started when we went on an American tour and I started feeling feverish. I found myself taking my bath with hot...