Posts

Showing posts from August, 2014

VIFAA VYA KUWATAMBUA WENYE UGONJWA WA EBOLA VYAINGIZWA NCHINI

Serikali imeanza kuingiza nchini vifaa vya kuwabaini watu wanaohisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa homa kali ya ebola ambavyo vitawekwa kwenye viwanja vya ndege pamoja na baadhi ya maeneo ya mipakani. Jana Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Steven Kebwe alikabidhi mashine nne za kuwapima abiria wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege bila kuwagusa. Vifaa hivyo vinabaini mtu kuwa na dalili za ebola kutokana na joto lake na abiria wanapimwa kwa kumulikwa machoni na kwenye masikio. Kwa kuanzia mashine hizo ambazo ni mfano wa kamera zitapelekwa kwenye viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar na Dar es Salaam. Maeneo hayo kwa mujibu wa naibu waziri huyo ndiyo yanapokea wagonjwa wengi kutoka nje ya nchi. Dk Kebwe pia aliagiza shehena ya mashine zingine zitakazoingizwa nchini kuanzia leo zipelekwe kwenye viwanja vingine vya Mtwara, Kigoma na maeneo ya mipakani kuhakikisha kuwa kila abiria anayetoka nje ya nchi anapimwa dalili za ugonjwa huo hatari. Pia aliagiza wanadi

EXCLUSIVE: JUX ASEMA VANESSA MDEE ANA SIFA ZA KUWA MKE

Jux amekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake Vanessa Mdee na kudai kuwa Vanessa ni mshikaji wake tu lakini amekiri kuwa muimbaji huyo wa ‘Come Over’ ana kila sifa ya kuwa mke. Jux ambaye hivi karibuni alionekana kuwa karibu na Vanessa amesema Vanessa ni mtu wake wa karibu anayefanya kazi naye. “No ni mshikhaji wangu tu, tunafanya naye kazi, kuna tabia zinaendana, kama ninavyokuwa na rafiki na Stamina, Mo Music ni kawaida, sema unajua ni mwanamke na ni njia toafuti ndio maana imekuwa hivyo,” alisema Jux. Alipoulizwa kama Vanessa anafaa kuwa wife material Jux alijibu Vanessa ana kila sifa ya kuwa mke. “Ni msichana mzuri, mwonekano wake mzuri, she is smart, yeah she is a wife material, yuko vizuri, lakini na mimi tumeendana sana tabia zetu kama washikaji. Sema nipo naye karibu na kwa sababu mimi sionekanagi na wasichana wengi ndio maana imekuwa hivyo. Lakini sijui labda baadaye kwa sasa hivi ni mapema, vyote anapanga Mungu,” alisisitiza Jux. CHANZO: BONGO5

BOB JUNIOR AKANUSHA KUHUSU KURUDIANA NA MKEWE

Rais wa Masharobaro, muimbaji na mtayarishaji wa muziki, Bob Junior amekanusha tetesi zilizokuwepo kuwa amerudiana na mke wake. Akiongea na segment ya Inbox ya kipindi cha New Chapter cha Radio Free Africa, Bob Junior amesema mazoea ya kuwa na mke na kumuona mtoto wake kila siku yanamfanya awe na huzuni kubwa kuwa mbali nao. Junior amesema aliachana na mke wake na hajarudiana naye tena na hana mpango wa kuoa hivi karibuni. Hivi karibuni kwenye Instagram Bob Junior alipost picha ya mwanae na kuandika: Namshukuru Mungu kukupata wewe maisha yangu yote nguvu zangu zote Nitapigana hadi kufa ni kwaajili yako my son Rummy Raheem Rummy maisha yako huta jutia kupata baba kama mimi ila amini kilicho tokea……. ukija kukuua ipo siku utajua yote naishi kwenye maumivu mengi juu yako sana na hapa naandika text hii nalia sana kwa kuwa mbali nawewe sikuoni karibu my son ila jua i love u na kama mapenzi kupenda nasema nitakupenda na hata kuja yoyote kuzidi mapenzi yangu kwako mengine sisemi ila jua mwana