CELEBRITY WA SIKU: PAUL WALKER
Leo katika kipengele cha Celebrity wa siku tunaye Paul Walker ambaye kwa sasa ni maremu. Kwa nini Paul Walker leo? Kwa sababu leo ni tarehe ambayo alizaliwa mwaka 1973 huko California. Na tuangalie historia yake ili kumfahamu zaidi.
KUZALIWA
Paul Walker alizaliwa Septemba 12, 1973 huko Glendale, Calfornia nchini Marekani.
ELIMU
Alipata Elimu yake katika Village Christian School.
KAZI
Paul Walker alikuwa muigizaji nchini Marekani ambapo alianza kazi hiyo katika televisheni mbalimbali kama vile katika vipindi vya The Young and the Restless na Touched by an Angel. Alipata umaarufu katika movie za vijana kama vile She's All That na Varsity Blues. Walker alipata umaarufu zaidi katika movie za Brian O'Conner ambapo zinahusisha uendeshaji wa magari mitaani 'The Fast and the Furious'. Alishiriki pia katika filamu kama vile Eight Below, Timeline, Into the Blue, Joy Ride na Running Scared.
Mbali na uigizaji, Walker pia alikuwa mtangazaji wa kipindi cha The Coty Prestige fragrance brand, Davidoff Cool Water for Men na alishiriki katika Chanel zinazoonesha Matukio ya kijiografia chini Marekani katika mfululizo wa vipindi vya Expedition Great White.
Pia alianzisha kikundi cha kusaidia jamii haswa wale wanaokumbwa na majanga ya asili kilichoitwa Reach Out WorldWide (ROWW).
Mpaka mauti yanamfika, Walker alikuwa anaigiza movie 3 ambazo ni Hours (2013), Brick Mansions (2014) na Furious 7 (2015). Wiz Khalifa alimuimbia wimbo wa heshima 'See You Again' ambao ulitumika kama soundtrack ya Furious 7. Wimbo huo ulitajwa kushiriki tuzo za Golden Globe Awards katika kipengele cha Wimbo Bora katika Tuzo ya 73 ya Golden Globe Wards.
MIAKA YA UMAARUFU
Paul Walker alikuwa maarufu kati ya mwaka 1984 hadi mwaka 2013 alipofikwa na mauti.
UTAJIRI ALIOKUWA NAO
Mpaka anafariki alikadiriwa kuwa na utajiri uliofikia dola za kimarekani bilioni 25 kwa makadirio ya mwaka 2014.
MAISHA YAKE
Walker alizaliwa Glendale California na alikuwa ni mtoto wa Cherly ambaye alikuwa mwanamitindo na baba yake Paul William Walker III alikuwa ni mkandarasi na mwanamasumbwi aliyeshinda ubingwa wa Golden Gloves mara mbili.
Paul Walker baada ya kumaliza elimu ya pili (kwa Tanzania kidato cha 5 & 6) alijiunga na vyuo mbali mbali Kusini mwa California akisomea baiolojia ya viumbe wa majini.
DINI
Walker alikuwa ni muumini wa Dini ya Kikristu. Kanisa lake linaitwa Nondenominational Christianity ambalo mwanzo lilijulikana kama The Church of Jesus Christ of Latter-day Saints.
FAMILIA
Aliacha mtoto mmoja aitwaye Meadow Walker. Pia alikuwa na Ndugu wawili wa kiume; Cody Walker na Caleb Walker.
KIFO
Paul Walker alifariki Novemba 30, 2013 katika ajali mbaya ya gari ambayo alikuwepo yeye na rafiki yake Roger Rodas miaka 38. Siku hiyo Walker akiwa na Roger walikuwa wakielekea katika taasisi yake ya kusaidia watu ROWW ambapo iliwalenga waanga wa kimbunga Typhoon Haiyan (Yolanda). Siku hiyo Roger ndiye aliyekuwa dereva huku Paul akiwa kama abiria. Inadaiwa kuwa Roger aliendesha gari kwa umbali wa maili 45 kwa saa sawa na kilomita 72 kwa saa na baadae gari yao Porsche Carrera GT ilipiga mzinga maeneo ya Kelly Johnson Parkway huko Valencia Santa Clarita California na badae gari yao iliungua. Ajali ilionekana kwenye camera ya ulinzi iliyokuwa maeneo hayo.
Mwaka 2014 uchunguzi zaidi ulionesha kuwa chanzo cha ajali kilikuwa ni mwendokasi ambapo alidaiwa kuwa gari ilikimbizwa katika mwendokasi wa kilomita 103 kwa saa.
Majivu ya mwili wa Paul Walker yalizikwa huko Forest Lawn Memorial Park, Hollywood Hills nchini Marekani.
Comments
Post a Comment