DIRISHA LA UFADHILI WA MASOMO "SAMIA SCHOLARSHIP" 2023/2014 LIMEFUNGULIWA
TANGAZO LA SAMIA SCHOLARSHIP MWAKA 2023/2024 UFADHILI KUPITIA SAMIA SCHOLARSHIP KWA WAHITIMU WENYE UFAULU WA JUU KATIKA MITIHANI YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2023 KATIKA TAHASUSI ZA SAYANSI 1.0 UTANGULIZI Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatangaza programu ya Ufadhili iitwayo SAMIA SCHOLARSHIP kwa masomo ya shahada ya kwanza kwa wanafunzi waliopata ufaulu wa juu katika mitihani ya Kidato cha Sita mwaka 2023 iliyoendeshwa na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) katika Tahasusi za Sayansi (PCB, PCM, PGM, CBG, CBA, PMC na CBN). SAMIA SCHOLARSHIP itagharamia kwa asilimia mia moja (100%) masomo ya Elimu ya Juu kwa wanafunzi hao ambao wamepata udahili katika fani za Teknolojia, Uhandisi, Hisabati na Tiba. 2.0 SIFA ZA KUPATA UFADHILI Ufadhili huu utatolewa kwa wahitimu wa kidato cha sita wenye sifa zifuatazo: 1. Awe Mtanzania; 2. Awe na ufaulu wa juu kwenye mitihani ya taifa ya kidato cha sita mwaka 2023 iliyoendeshwa na NECTA katika tahasusi za sayansi; 3. Awe amepata ...