Posts

Showing posts from March, 2016

MALAWI IMETEKETEZA TANI 2 ZA PEMBE ZA NDOVU KUTOKA TANZANIA

Image
Malawi imeteketeza tani 2.6 ya pembe za ndovu ambazo zilinaswa na maafisa wa usalama zikitokea nchi jirani ya Tanzania. Meno hiyo 781 ya tembo ambayo inakisiwa kugharimu takriban dola milioni tatu ilipatikana baada ya operesheni dhidi ya ulanguzi na uwidaji haramu. Mkurugenzi wa idara inayosimamia mbuga za wanyama pori Bright Kumchedwa, amesema kuwa hiyo ni ishara ya kwanza na dhabiti kutoka kwa Malawi kuwa haitaruhusu tena ardhi yake kutumika kulangua bidhaa za uwindaji haramu. Hafla ya hiyo ya kihistoria ilifanyika katika eneo la Mzuzu kaskazini mwa nchi hiyo. Kenya inatarajiwa kutekeleza hatua kama hiyo mwishoni mwa mwezi huu. Kenya imekamata takriban tani 120 ya meno ya ndovu. Chanzo: BBC

ZITTO KABWE: RAIS AMELIINGIZIA TAIFA HASARA YA TSH. BILIONI 36

Image
Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa Rais John Pombe Magufuli ameliingizia taifa hasara ya bilioni 36 mpaka sasa toka alipoingia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.   Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika kuwa kitendo cha Rais Magufuli kushindwa kuchukua hatua juu ya malipo ya IPTL ambayo yanalipwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kila mwezi yamepelekea sasa hivi kufikia jumla ya bilioni 36.   "Tshs bilioni 8 kila mwezi TANESCO bado wanalipa IPTL. Rais haijampendeza kumaliza ufisadi huu. IPTL nadhani ni Jipu la Mgongoni (kwa kutumia maneno ya Hidaya wa Richard Mabala ). Rais, kwa kutochukua kwake hatua, ameshaliingizia taifa hasara ya tshs 36 bilioni toka aingie madarakani" aliandika Zitto Kabwe.  Wakati Rais John Magufuli anatimiza siku 100 toka kutangazwa kama Rais Zitto Kabwe alitoa tathimini yake na kugusia sakata la Escrow pamoja na kampuni ya IPTL na kusema kuwa pesa ambazo wamelipwa I

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU MAREKANI: TRUMP NA RUBIO WATOFAUTIANA KUHUSU UISLAM

Image
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio amemshtumu Donald Trump kwa kusema kuwa Uislamu unachukia Marekani katika mjadala uliokuwa moja kwa moja runingani. Bwana Rubio ambaye anakabiliwa na ushindani wa maisha yake katika jimbo la Florida siku ya Jumanne amesema kuwa Uislamu una tatizo la itikadi kali lakini akaongezea kuwa Waislamu wengi wanapenda Wamerekani. ''Marais hawawezi kusema kile wanachotaka ,kuna madhara'',alisema huku raia wakimpigia makofi. Wagombea hao wanne wa chama cha Republican walisikia maombi kutoka kwa viongozi wa chama hicho kuwa na mjadala wa amani. Ikilinganishwa na mjadala uliopita ambao ulikabiliwa na na matusi ya kibinafsi mjadala huu ulikuwa na muongozo mzuri huku wagombea wote wakitoa malengo ya sera zao. ''Kufikia sasa siamini vile tumekuwa watulivu hapa'',bwana Trump alinukuliwa akisema. Lakini katika swala la Uislamu,kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Trump na wagombea wengine huku wen

JANET JACKSON AAHIRISHA KUFANYA ZIARA YA MUZIKI ULAYA KUFUATIA MAUZO MABAYA YA TIKETI

Image
Janet Jackson amefuta ziara yake kimuziki 'Unbreakable' barani Ulaya kufuatia mauzo mabaya ya tiketi barani humo. 'Alikuwa anaelekea kushindwa vibaya' kilisema chanzo cha habari. Muuza tiket mkuu alimuandikia barua pepe Janet mapema wiki hii kuhusu kurudishwa kwa hela za watu waliokuwa wamenunua tiketi. Hii ni wiki tatu kabla Janet alikuwa aende kufanya onesho jijini London, 'haitawezekana kwa sasa kusema ni lini tutapanga tena tarehe mpya ya onesho kwa hiyo tunarudisha hela kwa wale waliokuwa wamenunua tiketi' iliandikwa hivyo barua pepe hiyo. Upande wa Janet haukuzungumzia kuhusu kufutwa kwa onesho hilo lakini chanzo cha habari kilisema kuwa ni kufuatia mauzo mabay ya tiketi. 'Alikuwa anaelekea kushindwa vibaya, msanii anapofuta au kuahirisha ziara ya muziki sababu huwa ni mauzo mabaya ya tiketi' kilisema chanzo hicho na kuongeza 'ni bora kuahirisha kuliko kufanya onesho ukumbi ukiwa haujajaa watu haswa kwa msanii Janet Jackson'. Cha

MECHI KATI YA LEICESTER NA WEST BROM FAHAMU HAYA

Image
Mchezo wa leo kati ya Leicester city na West Bromwich Albion utapigwa katika dimba la King Power Stadium, ambapo Leicester watakuwa ni wenyeji wa dimba hilo. Mtanange utaanza saa 4 na dakika 45 usiku saa za Afrika Mashariki. Novemba 1, 2013, West Brom alimfunga Leicester goli moja bila katika dimba la King Power Stadium. Mwaka 2015, April 11 West Brom wakiwa wenyeji katika dimba la nyumbani, The Hawthorns walipigwa bao tatu dhidi ya mbili na Leicister city. Lakini pia October 31, mwaka jana 2015, West Brom akiwa mwenyeji kwenye dimba la The Hawthorns alifungwa na Leicester city magoli 3 kwa mawili kama mechi iliyopita. Leicester City inaongoza ligi ikiwa na pointi 56 ambapo imecheza mechi 27 imeshinda mechi 16, imetoka sare mechi 8, na kupoteza mechi 3 ikiwa na magoli ya kifunga 20. Kwa upande wa West Brom wao wapo katika nafasi ya 13 wakiwa wamecheza mechi 27, wameshinda mechi 9, sare mechi 8 na kupoteza mechi 10 wakiwa wmemfungwa magoli10. West Brom wana pointi

MAMBO YA KUFAHAMU KATI YA CHELSEA NA NORWICH CITY

Image
Chelsea imeshinda mechi saba na haijapoteza katika mechi tisa ilizokutana na Norwich City kwenye EPL. Norwich City imefenikiwa kuifunga Chelsea magoli manne tu na kushindwa katika mechi nne ambazo walikutana mara ya mwisho na The Blues. Steven Naismith wa Norwich City amefanikiwa kuifunga Chelsea magoli sita katima mechi saba walizokutana na The Blues EPL. Norwich City imeshinda mechi nne tu, sare nne na kupotezaechi nane katika mechi 16 ilizocheza katika dimba lao la nyumbani, Carrow Road. (W4 D4 L8). Norwich City imepata magoli 10 tu katika dimba lao la nyumbani, hii ni baada ya kushinda mechi mbili kati ya tano za EPL katika dimba hilo. Katika mechi 7 za EPL na kufunga magoli 7 pamoja na kuwa na jumla ya magoli 19 kwenye ligi. Chelsea imeshuhudia wachezaji wake 15 wakiifungia magoli timu hiyo msimu huu. Rekodi ambayo ni ya juu zaidi katika mashindani msimu huu. Guus Hiddink amepoteza mechi moja tu kati ya mechi 23 kama kocha na meneja wa klabu katika