Kwanza namshukuru Mungu toka tukiwa wadogo mpaka sasa anaendelea kutulinda. Uongozi mzima wa Venance Blog tunawatakieni maandalizi mema ya Krismas hapo kesho, wale wa kanisani tukafurahi kwani bwana atazaliwa. Msali salama katika misa za mkesha kubwa zaidi kudumisha amani na usalama kuanzia leo mpaka sikuku itakapoisha. MAANDALIZI MEMA YA KRISMAS!!!
Picha kwa hisani ya Freepik Shairi hili linakuja kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka huu nchini Liberia. Katika hali isiyo ya kawaida George Weah aliyekuwa akitetea nafasi yake ali kubali kusindwa na mpinzani wake Joseph Boakai katika Uchaguzi huo pasipo mvutano na migogoro kama ilivyozoeleka katika mataifa mengi ya bara hili . Kama mshairi niliwiwa kuandika ili kupongeza kitendo hiki cha uungwana kukubali kukabidhi madaraka pasipo mvutano ambao mara nyingi hupelekea umwagaji damu. Karibu katika shairi letu kwa lugha adhimu ya Kiswahili. Shairi: Heko Liberia Mtunzi: Venance Gilbert Mpate Mwaka: 19 Novemba 2023 HEKO LIBERIA Heko Liberia naisifu yenu demokrasia, Wenu ukomavu yote Afrika imeshuhudia, Tupeni maarifa darasani tupate kujifunzia, Afrika matokeo mshindani hawezi kuridhia, Uchaguzi mtawala hakubali kupoteza felia, Ninyi metuonesha mtawala aweza kuwa felia, Mpinzani akashika dola imani ikaendelea, Heko Liberia naisifu yenu demokrasia. Mtawala aku...

Comments
Post a Comment