TEKNOLOJIA ZA KALE ZINAZOTUMIKA HADI SASA
U hali gani? Nakukaribisha tena kwa mara nyingine katika blog hii. Leo nakukaribisha hapa tuangalie kuhusu mfululizo wa teknolojia tukijikita zaidi katika teknolojia za kale. Kwa kusema hivi nataka nikukutanishe na vumbuzi 10 za kale ambazo zilibadilisha maisha ya binadamu kwa kiasi kikubwa na bado vumbuzi hizo ni za manufaa hata kwa maisha ya leo. Nakukumbusha tena kwamba huu ni mfululizo wa teknolojia na vumbuzi mbalimbali. Tuanze sasa kuhesabu vumbuzi hizo: 1. Gurudumu Mabadiliko katika maendeleo ya magurudumu katika vyombo mbalimbali. Ugunduzi wa gurudumu ni moja ya maendeleo muhimu zaidi ya kiteknolojia katika historia ya mwanadamu. Magurudumu ya awali zaidi hayakutumika kwa usafiri badala yake kama magurudumu ya mfinyanzi yanayoaminika kutumika mara ya kwanza huko Mesopotamia (kwa sasa Iraq) karibu mwaka 3500 KK (Kabla ya Kristo). Kufikia mwaka 3200 KK, watu wa Mesopotamia walianza kutumia magurudumu kwa magari ya vita na mikokoteni. Magurudumu haya ya kwanza yalikuwa...