Posts

Showing posts from July, 2017

RAIS PUTIN AMEAGIZA WANADIPLOMASIA 755 WA MAREKANI KUONDOKA URUSI

Image
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza wafanyakazi 755 wa ubalozi wa Marekani nchini Urusi kusitisha shughuli zao kufikia Septemba mosi mwaka huu. Urusi imeidhinisha hatua hiyo kwa ghadhabu kufuatia vikwazo vipya vilivyopitishwa na bunge la Marekani dhidi yake, kwa tuhuma za kuingilia uchaguzi wa taifa hilo mwaka jana. Marekani kwa upande wake, inasema imesikitishwa na uamuzi huo, na inapima athari na kutafakari namna ya kujibu hatua hiyo. Hatua hii ya Urusi imekuja baada ya vikwazo vipya dhidi ya Urusi kuidhinishwa kwa wingi wa kura na mabunge yote ya congress nchini Marekani Jumanne, licha ya kwamba Ikulu ya White house ilipinga kura hiyo. Rais huyo wa Urusi ameapa kuwa upo uwezekano wa kuongeza vikwazo zaidi dhidi ya serikali ya Marekani. Akizungumza kwenye televisheni ya taifa ya Urusi, rais Putin alisema kuwa alitarajia uhusiano baina ya Moscow na Washington ungebadilika na kuwa mzuri, lakini hilo haliwezekani kwa sasa. Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Estonia,

MMILIKI WA NGURDOTO HOTEL AFARIKI DUNIA

Image
Mfanyabiashara maarufu nchini, Maleu Mrema amefariki dunia jana akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini. Akizungumza na Mwananchi ndugu wa marehemu,Vincent Laswai alithibitisha msiba huo akiwa nyumbani kwa marehemu eneo la Uzunguni jijini Arusha. Akihojiwa na gazeti la Mwananchi Laswai amesema kwamba alipokea taarifa za kifo cha marehemu jana saa 12 jioni na uongozi wa familia utatoa taarifa za kifo cha mfanyabiashara huyo leo. Laswai, amesema kwamba ni mapema kuzungumzia chanzo cha kifo kwa sababu bado hawajapata taarifa kutoka katika hospitali aliyokuwa akitibiwa nchini humo. Hivi karibuni marehemu Mrema alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya ambapo Juni mwaka huu alipelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu. Chanzo: Mwananchi

PICHA 20 KUTOKA KWA DIAMOND NA ZARI WAKIWA KENYA WALIZOPOST INSTAGRAM

Image
Diamond na Zari wameendelea na starehe zao huko Mombasa Kenya huku team ya WCB ikitia mguu pia mahali hapo; Harmonize na Sallam walihusika pia. Hizi ni baadhi ya picha kutoka katika mapumziko hayo. Hapa Zari aliamua kumtania shemeji yake Harmonize. mkubwa Simba na Zari katika starehe zao Harmonize alipata nafasi ya kusema chochote BClub Katika picha hii Diamond kaandika caption ya kiingereza ambayo Kiwashili chake ni "namwambia Harmonize kwamba wenye chuki wote hawana maana. Tuna uwezo na ni matarijiri" Unamuona Zari anavyozidi kupendeza kama ndo kwanza ana miaka 12 Kila mtu apambane na mahusiano yake tu. Huu mkao sasa Zari alivyomtegea Mond afu anajifanya kama hana habari yuko busy na simu Sallam alihusika pia B Club Wanapendeza hawa wapendanao unamuona Zari? KWA PICHA, MATUKIO, HABARI NA MAELEZO KAMA HAYA NA MENGINE MENGI USISITE KUTEMBELEA VENANCE BLOG: Facebook: VENANCE BLOG Twitter: @Venan

DIAMOND AWAJIA JUU WANAOMSEMA ZARI KUHUSU MSIBA WA MAMA YAKE

Image
Mwanamuziki wa Tanzania aliyeikamata Afrika na Dunia kwa uimbaji wake wa lugha ya Kiswahili, Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote, Baba Tee, Simba na majina mengineyo usiku wa leo amewajia juu hasa wadada wanaomsema mpenzi wake Zarina Hassan kufuatia kifo cha mama yake kilichotokea majuzi tu. Zari ameonekana na Diamond wakiwa katika starehe za mahusiano yao kitu kilichopelekea wadau na mashabiki wao kuliongelea suala hilo. Kwa tamaduni za kiafrika na jinsi tulivyozoea, mtu anapofiwa hasa na Mama yake mzazi humchukua muda sana kabla ya kurudi katika utaratibu wa kawaida, hii imekuwa tofauti kwa Zari ambaye siku chache tu baada ya msiba ameonekana na Diamond wakiponda raha huku wakijirekodi video na kuzituma katika mtandao wa Instagram hali iliyopelekea mashabiki kuliongelea sana suala hilo. Diamond Platnumz amefunguka baada ya kuonekana kukerwa na maneno ya watu katika mtandao wa Instgram na kuyaandika haya: " Kuna vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa misiba ya

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU KABLA YA KUCHAGUA KOZI CHUO KIKUU

Image
Kumekuepo na manung'uniko miongoni mwa wanafunzi wengi wa vyuo vikuu, manung'uniko haya hutokana na zile kozi wanazosoma chuoni. Kuna sababu kadha wa kadha zinazopelekea manung'uniko hayo miongoni mwa wasomi hawa tukiachilia mbali suala la ucheleweshwaji wa mikopo miongoni mwa wasomi hawa  (kwa sasa changamoto hii inapungua kadiri siku zinavyosonga) tatizo lingine ambalo linawasumbua wasomi hawa ni suala la uchaguzi wa kozi gani akaisome Chuo Kikuu. Kuna mambo kadhaa ambayo huwakuta wanafunzi hawa wawapo vyuo vikuu, mambo haya yaweza kuwa; kutoendelea na masomo ya Chuo Kikuu kutokana na kufeli masomo (Discontinuation from studies), kufeli majaribio mara kwa mara kutokana na kutoridhika na kile wanachosomea ama ugumu wa masomo. Sababu kubwa hapa zaweza kuwa tatu; kwanza, uchaguzi wa kozi kwa kufuata mkumbo wa marafiki, pili, kushawishiwa ama kuchaguliwa kozi na mzazi ama mtu yeyote aliyesoma kozi husika na kupata mafanikio kwa hivyo na mchaguaji anaona naye asome kozi