Producer Man Water wa combinataion sound, ameelezea sababu ya kupenda kuwarudisha wasanii wa kitambo kwenye game, ambao tayari walishapotea kimuziki. Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Man Water amesema hupenda kufanya hivyo kwani ana imani wasanii hao bado wana uwezo mkubwa, na kwa kuwa alitoka nao mbali kikazi. “Kurudisha wasanii waliopotea mimi na kuwa nao karibu kwa sababu ni watu wangu ambao nimetoka nao mbali, najua hustle zao tulipita wote, na kwa sababu mi mwenzao bado nimebaki kwenye game, sasa nikiwaita wale nawaambia jinsi gani game ya sasa ilivyo na wabadilike vipi ili waweze kurudi”, alisema Man Water. Man Water alishawahi kumrudisha kwenye game msanii 20% , Alikiba, Lady Jaydee na wengine, huku bado akiwa na mpango wa kuendelea kuwarudisha wasanii wengine kama Mr. Nice. Chanzo: EATV