WANAJESHI WAUAWA KWA BOMU SOMALIA

Milipuko imekuwa ikijitokeza mara kwa mara nchini Somalia. Takriban wanajeshi watano na afisa wa jeshi wameuawa katika mlipuko wa bomu mjini Mogadishu nchini Somalia mashuhuda wameeleza.

Mlipuko huo unaelezwa kutokea wakati wanajeshi hao wakipata malipo yao nje kidogo ya mji huo. Sababu ya mlipuko huo haijafahamika majeruhi kadhaa wamepelekwa hospitalini kwa matibabu.

Wanamgambo wa kiislamu, Al Shabab walitimuliwa kwa nguvu mjini Mogadishu mwaka 2011 lakini wameendelea kufanya mashambulizi nchini humo. Kundi hilo lenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda linadhibiti maeneo kadhaa katikati ya Somalia.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

CELEBRITY: SHANIA TWAIN ANATIMIZA MIAKA 53 LEO AGOSTI 28, 2018

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

WAFAHAMU MATAJIRI 10 WA TANZANIA MWAKA 2018

FAHAMU MAMBO HAYA 20 KUHUSU TANZANIA

KANSELA ANGELA MERKEL ASEMA UJERUMANI YA SASA NI BORA ZAIDI