Home »
» NELSON MANDELA AFARIKI NYUMBANI KWAKE JOHANESBURG
NELSON MANDELA AFARIKI NYUMBANI KWAKE JOHANESBURG
Jana usiku shujaa wa Afrika Mzee Nelson Mandela alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Amefariki kwa ugonjwa wa maambukizi ya pafu, ugonjwa uliomsumbua kwa muda mrefu. Pia katikati ya mwaka huu alikaa hospitali kwa muda wa miezi 3 na baadaye mwezi wa tisa alitolewa hospitali na kwenda kutibiwa nyumbani kwake Johanesburg mpaka mauti yalipomfika. Rais wa nchi hiyo, Jackob Zuma amesema taifa limempoteza shujaa wao na kwamba mwili wake utasifirishwa kwenda kuhifadhiwa katika mochwari ya mji mkuu Pretoria na kwa taratibu za mazishi zitafanywa Jumamosi ijayo pia atazikwa kwa heshima kubwa ya kitaifa na pia bendera zote zitapepea nusu mlingoti nchini humo kama maombolezo ya shujaa huyo...
MUNGU AMPUMZISHE KWA AMANI..
0 comments:
Post a Comment