Venance Blog inawatakieni HERI YA KRISMAS. Mpendwa msomaji wa blog hii, leo Wakristu duniani kote wanaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwokozi wao, Yesu Kristu aliyezaliwa takribani miaka 2000 iliyopita. Venance Blog inakukumbusha katika sikukuu hii kama ni mnywaji usilewe sana na pia ukumbuke ugonjwa hatari wa UKIMWI hasa siku kama hii ya leo kuwa makini sana, pia tuwasaidie watoto wetu au wadogo zetu kuvuka mabarabara salama huko mitaani kwetu. Krismasi ni siku ya furaha na kuoneshana upendo, hivyo tupendane wote kwa pamoja.
HERI YA KRISMAS NA KRISMAS YENYE FURAHA SHEREHEKEA KWA AMANI NA UPENDO!!!
Picha kwa hisani ya Freepik Shairi hili linakuja kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka huu nchini Liberia. Katika hali isiyo ya kawaida George Weah aliyekuwa akitetea nafasi yake ali kubali kusindwa na mpinzani wake Joseph Boakai katika Uchaguzi huo pasipo mvutano na migogoro kama ilivyozoeleka katika mataifa mengi ya bara hili . Kama mshairi niliwiwa kuandika ili kupongeza kitendo hiki cha uungwana kukubali kukabidhi madaraka pasipo mvutano ambao mara nyingi hupelekea umwagaji damu. Karibu katika shairi letu kwa lugha adhimu ya Kiswahili. Shairi: Heko Liberia Mtunzi: Venance Gilbert Mpate Mwaka: 19 Novemba 2023 HEKO LIBERIA Heko Liberia naisifu yenu demokrasia, Wenu ukomavu yote Afrika imeshuhudia, Tupeni maarifa darasani tupate kujifunzia, Afrika matokeo mshindani hawezi kuridhia, Uchaguzi mtawala hakubali kupoteza felia, Ninyi metuonesha mtawala aweza kuwa felia, Mpinzani akashika dola imani ikaendelea, Heko Liberia naisifu yenu demokrasia. Mtawala aku...

Comments
Post a Comment