WAFAHAMU MATAJIRI 10 WA TANZANIA MWAKA 2018

10. YUSUF MANJI

Manji ni mmiliki wa mali zisizohamishika hasa majengo kwa ajili ya makazi ya watu na biashara. Pia ni muanzilishi wa kampuni ya Quality Group of Companies. Anajihusisha pia na vipuli vya magari. Haya yamemfanya kua miongoni mwa matajiri wa juu zaidi nchini.

9. FIDA RASHID

Fida ni muanzilishi wa kampuni ya Africarrier Group. Hii ni kampuni inayohusika na magari yaliyotumika. Pia kampuni hii inahusika na usambazaji wa magali ya kampuni ya Eicher na Golden Dragon hapa nchini. Hii imefanya kampuni yake kufanya vyema sana katika idara hii. Fida pia ni mmiliki wa mali zisizohamishika pamoja na majengo kama Zahra Tower na Raha Tower. Amekua mjasiriamali anayetengeneza zaidi mazingira mazuri ya biashara zake kama wafanyavyo wengine.

8. GHALIB SAID MOHAMMED

Ghalib Mohammed alikua akifanya biashara ya korosho hapo awali na biashara nyingine akishirikiana na baba yake. Baadaye Ghalib Said aliamua kuanzisha kampuni yake na kuiita GSM Group ambayo inajihusisha na uuzaji wa bidhaa za rejareja, usafirishaji wa vifaa na bidhaa, huduma za kifedha, vyombo vya habari na mengine mengi. Vyanzo vyote hivi vinamfanya kua miongoni mwa matajiri wakubwa nchini. Kama mjasiriamali aliamua kujihusisha zaidi na mazao ya kilimo pamoja na baba yake jambo ambalo limewafanya kufikia walipo kwa sasa.

7. SUBASH PATEL

Patel ni mwanachama wa Taasisi ya Wahandisi wa Umeme na ana ubia na kampuni ya MMI Steels Resource Limited na Nyaza Road Works. Katika kipindi cha miaka 20 amefanikiwa kupanua biashara zake mpaka kufikia kuwa na kampuni inayoitwa Motsun Group. Kampuni hii imegawanyika katika makampuni mengine 11 ambazo zinahusika na bidhaa za chakula, madini, majengo na kusaidia makampuni mengine kitaalamu.

6. SHEKHAR KANABAR

Shekhar ni meneja katika kampuni ya Synarge Group. Hii ni kampuni inayohusika na bidhaa za magari. Kampuni hii pia inahusika na utengenezaji wa madini ya risasi. Licha ya kwamba kampuni hii ni mali ya familia, Shekhar anabainishwa kuwa miongoni mwa matajiri nchini kutokana na uongozi wake mzuri katika kampuni hiyo. Kampuni hii pia inahusika na usambazaji wa spea za magari nchini. Huwezi kuzungumzia Teknolojia hii ya magari bila kumzungumzia Shekhar. Synarge imekua ikifanya vema katika mauzo ya bidhaa za magari nchini.

5. ALLY AWADH

Awadh ni miongoni mwa watu wenye akili ya biashara. Amefanya uwekezaji katika sekta za mafuta na gesi, ni muwekezaji muhimu sana katika sekta hizi. Alifanya kazi kwa juhudi sana ili apewe kibali na serikali na baadaye alifanikiwa katika hilo na sasa ana kampuni yake ya Lake Oil Group inayohusika na kuingiza pamoja na kusambaza mafuta ya petroli na gesi nchini. Biashara ya mafuta inatajirisha kwa haraka sana lakini kwa Awadh haikua hivyo, amepitia changamoto nyingi pamoja na magumu mengi mpaka hapo alipofikia.

4. REGINALD MENGI

Mengi ni mmiliki na mkuu wa kampuni kubwa ya habari nchini IPP Media Group. Kampuni hii ina jumla ya vituo vya redio 11, vituo vya televisheni, magazeti na huduma za mtandao (Internet). Mengi pia ni mmiliki wa kampuni ya Kilimanjaro Spring Water na Bonite Bottlers. Ndoto yake na mapenzi katika tasnia ya habari vimemfanya kutimiza malengo yake ya kutangaza na kufikisha habari kwa Watanzania. Anamiliki utajiri unaokadiriwa kuwa dola milioni 560.

3. SAID SALIM BAKHRESA

Bakhresa aliacha masomo ya shule ya sekondari akiwa na umri wa miaka 14. Kwa kipindi hicho alikua akifanya biashara ya kuuza viazi na akafungua mgahawa wa kuuza chakula na kisha akafungua mashine ya kusaga nafaka. Bakhresa ameijenga biashara yake kwa muda wa miaka 30 iliyopita mpaka kufikia leo, pia ni miongoni mwa matajiri wakubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kampuni yake ya Bakhresa Group of Companies ni maarufu kwa uzalishaji wa bidhaa za chakula, mafuta ya petroli, usafirishaji ndani ya bahari ya Hindi na usagaji wa nafaka. Pia ni mmiliki wa king'amuzi cha Azam TV ambacho kinatoa huduma kwa malipo katika ukanda wa Afrika Mashariki. Akiwa ameajiri zaidi ya watu 3000 katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, akiwa na matawi ya kibiashara nchini Msumbiji, Malawi na Uganda, Bakhresa anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 650 za Marekani. Bakhresa amekuwa akitoa msaada wa kifedha kwa watu wenye uhitaji nchini.

2. ROSTAM AZIZ

Rostam anashikiria rekodi ya kuwa bilionea wa mwanzo nchini Tanzania. Anamiliki kampuni ya madini inayotwa Caspian Mining, kampuni hii inatoa huduma za kitaalamu kwa makampuni makubwa ya madini nchini kama vile Barrick Mining na BHP Billiton. Alinunua 17.2% ya hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania mwaka 2014. Anamiliki mali zisizohamishika nchini Tanzania, Lebanon, Dubai na Oman. Pia ni mdau mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam. Utajiri wake unakadiriwa kuwa dola bilioni 1 za Marekani. Alikua ndiye bilionea wa kwanza nchini mpaka pale MO Dewji alipochukua nafasi hii. Ndiye tajiri wa kwanza kuwahi kufikia kada hii ya matajiri bilionea kutoka Tanzania.


1. MOHAMMED DEWJI

MO Dewji ni miongoni mwa matajari wenye umri wa miaka 40 barani Afrika. Anamiliki 75% ya hisa zote katika kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (METL) ambayo inamiliki viwanda vingi nchini. Baada kupata umiliki wa viwanda vya nguo na mimea ya mafuta kutoka serikali ya Uganda utajiri wake ukaanza kukua kwa kasi. Ana utajiri uanaokadiriwa kufikia dola bilioni 1.3 za Marekani, hii inamfanya kuwa tajiri namba 1 kwa sasa nchini. MO alitajwa na Forbes kuwa tajiri namba 1 nchini mwanzoni mwa mwaka huu na bado ameendelea kushikilia namba hiyo. 


Chanzo: Forbes Raking

Comments

Popular Posts

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

ZIFAHAMU GAUNI BORA 20 ZA MWAKA 2017