Mahakama ya rufaa nchini Misri imeamuru kuachiliwa huru kwa wanawake, 21 wakiwemo wasichana saba waliofungwa jela mwezi jana kwa kuandaa maandamano ya kumuunga mkono aliyekuwa Rais Mohammed Morsi.Watoto hao wamepewa kifungo cha nje cha miezi mitatu. Mahakama hiyo pia ilipunguza kifungo cha miaka 11 walichokuwa wamepewa wanawake hao 14.Mahakama iliwapata na hatia mwezi jana ya kuwa sehemu ya kundi la kigaidi lililokuwa linatatiza usafiri wa magari, kufanya hujuma na kutumia nguvu kufanya vitendo vyao.Hata hivyo makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa hukumu hiyo.Mmoja wa wanaharakati hao walitaja hukumu hiyo kama ya wazimu.Wanawake hao walifikishwa mahakamani wakiwa wamevalia nguo nyeupe huku wakiwa wamebeba maua ya waridi.Aidha wanawake hao na watoto walishiriki maandamano ya kumuunga mkono aliyekuwa rais Morsi na jamaa zao wanasema ni maandamano ya kwanza waliyowahi kushiriki na kuyaendesha bila vurugu.Mamia ya watu wameuawa nchini Misri tangu hatua ya kumwondoa Morsi madarakani mwezi Julai kusababisha maandamano na vurugu nyingi.
SOURCE: BBC Swahili
KUANZISHWA KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA Mafanikio ya michuano ya mpira wa miguu ya Olimpiki ndiyo yalikua mwanzo wa FIFA kutamani kuwa na michuano yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo wa mpira wa miguu. Ikumbukwe kwamba kipindi hicho mpira wa miguu wa wanaume pekee ndiyo ulikuwepo. Maswali yalitumwa kwa wahisani wa FIFA ili kuona kama wanakubaliana na uanzishwaji wa michuano hiyo na kwa masharti yapi? Kamati maalumu ilichunguza maswali hayo chini ya uongozi wa Rais wa FIFA wa kipindi hicho Jules Rimet akishirikiana na Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa kwa wakati ule Henri Delaunay. Rais wa FIFA Jules Rimet aliyeanzisha na kusimamia Kombe la Dunia la kwanza . Kufuatia uwepo wa muswada wa Kamati Tendaji ya FIFA, lilifanyika kongamano la FIFA Mei 28, 1928 jijini Amsterdam nchini Uholanzi likiazimia kuwepo kwa michuano ya mabingwa wa soka duniani ambayo ilipangwa na shirikisho hilo la mpira duniani na sasa nchi waandaji wa michuano hiyo zilitakiwa ...
Comments
Post a Comment