KINGEREZA CHAMCHANGANYA MKALIMANI AFRIKA KUSINI
Serikali ya Afrika Kusini imesema kampuni iliyomtoa mtafsiri wa lugha za ishara wakati wa ibada ya kumbukumbu kifo cha Nelson Mandela imekuwa ikidanganya kwa miaka mingi na imekuwa ikitoa watafsiri wenye kiwango cha chini.
Wataalamu wa lugha za ishara wamesema mtafsiri huyo wa lugha za ishara, Thamsanqa Dyanty, alikuwa "akitapatapa" wakati wa ibada hiyo siku ya jumanne. Naibu Waziri wa Afrika Kusini Hendrietta Bogopane - Zulu amesema hakuna suala lolote la kukiuka taratibu za kiusalama wakati mtafsiri huyo alipokuwa akisimama kwani alikuwa na vibali halali.
Katika maoni yake mtafsiri huyo anayelalamikiwa, Bwana Dyanty , amesema alipatwa ugonjwa wa kuchanganyikiwa. Kwa upande wake mmiliki wa kampuni iliyomtoa mtafsiri huyo imetupilia mbali madai ya Naibu waziri Bogopane Zulu.
Awali Naibu Waziri huyo aliwaomba radhi jamii ya viziwi kwa kiwango cha chini cha kutafsiri kilichofanywa na Bwana Dyanty kutoka kampuni ya SA Interpreters."Mtafsiri huyo anazungumza lugha ya Xhosa hivyo kiingereza kilikuwa kigumu sana kwake," alisema Waziri huyo.
Comments
Post a Comment