ZITTO AKERWA KUITWA MUONGO BUNGENI

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, amesema anatarajia kuwasilisha maelezo binafsi kuhusu, kauli ya Mwanasheria Mkuu aliyoitoa juzi bungeni dhidi yake na kumuita muongo kuhusu suala la kuwa na orodha ya watu wanaodaiwa kuficha fedha nje ya nchi.Zitto, aliyasema hayo bungeni juzi, ikiwa ni siku moja tu baada ya Mwanasheria Mkuu (AG), Jaji Frederick Werema, kudai mbele ya Bunge kuwa Serikali inashughulikia kisheria suala la Zitto kudanganya Bunge na Kamati kuhusu majina ya watu walioficha mabilioni ya fedha Uswisi.Akizungumza na HabariLeo Jumapili, Zitto alisema kwa sasa hataki kuzungumzia suala hilo, ila ukweli wote ataubainisha kwenye maelezo yake binafsi ambayo atayawasilisha wiki ijayo kwenye mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea.“Nimeamua hili suala nilizungumzie ndani ya Bunge, kwa hiyo tayari nimewasilisha maelezo yangu kwenye Ofisi ya Bunge, na wameniambia kuwa nitapangiwa kuwasilisha maelezo hayo wiki ijayo, kila kitu nitakibainisha siku hiyo, sina zaidi,” alisisitiza Zitto.Wakati akitoa majumuisho ya mjadala wa taarifa zilizowasilishwa bungeni juzi, ambazo ni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Werema alisema katika suala hilo, Zitto amezidi kuwa mzito.AG huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kuchunguza madai ya mabilioni hayo amesema ili kumalizia uchunguzi wa fedha hizo ameomba Spika wa Bunge kuongezea kamati hiyo miezi sita.Werema alisema alishangaa kitendo cha Zitto kutaka suala hilo liangalie mfumo na siyo majina ya watu walioficha mabilioni hayo. Alisema awali yeye alishauri kuangalia mfumo wa uwekaji wa fedha hizo, lakini Zitto alikataa na kusema anataka kutoa dukuduku kwa kutaja majina ya watu walioficha fedha hizo.Alisema mwezi Februari Kamati ilikutana na Zitto na kuwaeleza kuwa ana taarifa na nyaraka na kutoa masharti lakini aliondoka kwenda katika kambi ya Jeshi ambako Kamati ilimfuata lakini bado aliwataka kukutana Dar es Salaam.Alisema Mei mwaka huu hadi aliposema hakuwa na jina wala akaunti ya mtu yeyote ambaye ana akaunti nje ya nchi kwa kiapo maalumu.“Jambo la kushangaza ni leo kudai Serikali haina dhamira na suala la walioficha fedha Uswisi? Kwa kweli Zitto Kabwe ni mzigo na sasa tunaingia kufanya kazi hiyo ya uchunguzi kama Serikali kwa kutafuta taarifa bila kumuonea mtu,” alisema Werema.

Comments

Popular Posts

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU

WAFAHAMU MATAJIRI 10 WA TANZANIA MWAKA 2018