Showing posts with label Fahamu. Show all posts
Showing posts with label Fahamu. Show all posts

WAFAHAMU MATAJIRI 10 WA TANZANIA MWAKA 2018

10. YUSUF MANJI

Manji ni mmiliki wa mali zisizohamishika hasa majengo kwa ajili ya makazi ya watu na biashara. Pia ni muanzilishi wa kampuni ya Quality Group of Companies. Anajihusisha pia na vipuli vya magari. Haya yamemfanya kua miongoni mwa matajiri wa juu zaidi nchini.

9. FIDA RASHID

Fida ni muanzilishi wa kampuni ya Africarrier Group. Hii ni kampuni inayohusika na magari yaliyotumika. Pia kampuni hii inahusika na usambazaji wa magali ya kampuni ya Eicher na Golden Dragon hapa nchini. Hii imefanya kampuni yake kufanya vyema sana katika idara hii. Fida pia ni mmiliki wa mali zisizohamishika pamoja na majengo kama Zahra Tower na Raha Tower. Amekua mjasiriamali anayetengeneza zaidi mazingira mazuri ya biashara zake kama wafanyavyo wengine.

8. GHALIB SAID MOHAMMED

Ghalib Mohammed alikua akifanya biashara ya korosho hapo awali na biashara nyingine akishirikiana na baba yake. Baadaye Ghalib Said aliamua kuanzisha kampuni yake na kuiita GSM Group ambayo inajihusisha na uuzaji wa bidhaa za rejareja, usafirishaji wa vifaa na bidhaa, huduma za kifedha, vyombo vya habari na mengine mengi. Vyanzo vyote hivi vinamfanya kua miongoni mwa matajiri wakubwa nchini. Kama mjasiriamali aliamua kujihusisha zaidi na mazao ya kilimo pamoja na baba yake jambo ambalo limewafanya kufikia walipo kwa sasa.

7. SUBASH PATEL

Patel ni mwanachama wa Taasisi ya Wahandisi wa Umeme na ana ubia na kampuni ya MMI Steels Resource Limited na Nyaza Road Works. Katika kipindi cha miaka 20 amefanikiwa kupanua biashara zake mpaka kufikia kuwa na kampuni inayoitwa Motsun Group. Kampuni hii imegawanyika katika makampuni mengine 11 ambazo zinahusika na bidhaa za chakula, madini, majengo na kusaidia makampuni mengine kitaalamu.

6. SHEKHAR KANABAR

Shekhar ni meneja katika kampuni ya Synarge Group. Hii ni kampuni inayohusika na bidhaa za magari. Kampuni hii pia inahusika na utengenezaji wa madini ya risasi. Licha ya kwamba kampuni hii ni mali ya familia, Shekhar anabainishwa kuwa miongoni mwa matajiri nchini kutokana na uongozi wake mzuri katika kampuni hiyo. Kampuni hii pia inahusika na usambazaji wa spea za magari nchini. Huwezi kuzungumzia Teknolojia hii ya magari bila kumzungumzia Shekhar. Synarge imekua ikifanya vema katika mauzo ya bidhaa za magari nchini.

5. ALLY AWADH

Awadh ni miongoni mwa watu wenye akili ya biashara. Amefanya uwekezaji katika sekta za mafuta na gesi, ni muwekezaji muhimu sana katika sekta hizi. Alifanya kazi kwa juhudi sana ili apewe kibali na serikali na baadaye alifanikiwa katika hilo na sasa ana kampuni yake ya Lake Oil Group inayohusika na kuingiza pamoja na kusambaza mafuta ya petroli na gesi nchini. Biashara ya mafuta inatajirisha kwa haraka sana lakini kwa Awadh haikua hivyo, amepitia changamoto nyingi pamoja na magumu mengi mpaka hapo alipofikia.

4. REGINALD MENGI

Mengi ni mmiliki na mkuu wa kampuni kubwa ya habari nchini IPP Media Group. Kampuni hii ina jumla ya vituo vya redio 11, vituo vya televisheni, magazeti na huduma za mtandao (Internet). Mengi pia ni mmiliki wa kampuni ya Kilimanjaro Spring Water na Bonite Bottlers. Ndoto yake na mapenzi katika tasnia ya habari vimemfanya kutimiza malengo yake ya kutangaza na kufikisha habari kwa Watanzania. Anamiliki utajiri unaokadiriwa kuwa dola milioni 560.

3. SAID SALIM BAKHRESA

Bakhresa aliacha masomo ya shule ya sekondari akiwa na umri wa miaka 14. Kwa kipindi hicho alikua akifanya biashara ya kuuza viazi na akafungua mgahawa wa kuuza chakula na kisha akafungua mashine ya kusaga nafaka. Bakhresa ameijenga biashara yake kwa muda wa miaka 30 iliyopita mpaka kufikia leo, pia ni miongoni mwa matajiri wakubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki. Kampuni yake ya Bakhresa Group of Companies ni maarufu kwa uzalishaji wa bidhaa za chakula, mafuta ya petroli, usafirishaji ndani ya bahari ya Hindi na usagaji wa nafaka. Pia ni mmiliki wa king'amuzi cha Azam TV ambacho kinatoa huduma kwa malipo katika ukanda wa Afrika Mashariki. Akiwa ameajiri zaidi ya watu 3000 katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, akiwa na matawi ya kibiashara nchini Msumbiji, Malawi na Uganda, Bakhresa anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 650 za Marekani. Bakhresa amekuwa akitoa msaada wa kifedha kwa watu wenye uhitaji nchini.

2. ROSTAM AZIZ

Rostam anashikiria rekodi ya kuwa bilionea wa mwanzo nchini Tanzania. Anamiliki kampuni ya madini inayotwa Caspian Mining, kampuni hii inatoa huduma za kitaalamu kwa makampuni makubwa ya madini nchini kama vile Barrick Mining na BHP Billiton. Alinunua 17.2% ya hisa za kampuni ya Vodacom Tanzania mwaka 2014. Anamiliki mali zisizohamishika nchini Tanzania, Lebanon, Dubai na Oman. Pia ni mdau mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam. Utajiri wake unakadiriwa kuwa dola bilioni 1 za Marekani. Alikua ndiye bilionea wa kwanza nchini mpaka pale MO Dewji alipochukua nafasi hii. Ndiye tajiri wa kwanza kuwahi kufikia kada hii ya matajiri bilionea kutoka Tanzania.


1. MOHAMMED DEWJI

MO Dewji ni miongoni mwa matajari wenye umri wa miaka 40 barani Afrika. Anamiliki 75% ya hisa zote katika kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (METL) ambayo inamiliki viwanda vingi nchini. Baada kupata umiliki wa viwanda vya nguo na mimea ya mafuta kutoka serikali ya Uganda utajiri wake ukaanza kukua kwa kasi. Ana utajiri uanaokadiriwa kufikia dola bilioni 1.3 za Marekani, hii inamfanya kuwa tajiri namba 1 kwa sasa nchini. MO alitajwa na Forbes kuwa tajiri namba 1 nchini mwanzoni mwa mwaka huu na bado ameendelea kushikilia namba hiyo. 


Chanzo: Forbes Raking

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

Ramani ya Afrika.
Karibu tena mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG. Leo katika safu yetu ya Fahamu napenda kukufahamisha mambo kadhaa ambayo huenda hukuyafahamu yote kuhusu bara la Afrika. Na tuanze sasa kuyahesabu mambo hayo:


1. Karibu nchi zote za Afrika zilitaliwa na wakoloni isipokuwa nchi mbili tu: Ethiopia na Liberia.

2. Kabla ya Ukoloni, Afrika ilikuwa na tawala zilizokaribia 10,000 (Kingdoms/Empire/State) na tawala hizi zilijiongoza kila moja kivyake zikiwa na lugha tofauti na mila na desturi tofauti tofauti.

3. Lugha ya kiarabu inazungumzwa na watu takribani milioni 170 ikifuatiwa na lugha ya kiingereza inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 130, Kiswahili kikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 100, Kifaransa takribani wazungumzaji milioni milioni 115. Pia, kuna wazungumzaji wa lugha ya Xhosa wakiwa milioni 50. Kireno kinakadiriwa kuwa na wazungumzaji milioni 20 huku Kispanyola kikiwa na wazungumzaji wanaokadiriwa kuwa milioni 10. Vilevile takribani 25% ya lugha zote duniani zinazungumzwa barani Afrika huku kukiwa na lugha za makabila zaidi ya 2,000.

4. Afrika ni bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani ambao wanakadiriwa kuwa bilioni 1.1 huku zaidi ya 50% ya wakazi wake wakiwa ni vijana wenye umri chini ya miaka 25. Inakadiriwa kwamba mpaka kufikia mwaka 2050 bara la Afrika litakuwa na takribani watu bilioni 2.3. Hii ni kwa mujibu wa taarifa za idadi ya watu iliyotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 2015.

5. Takribani 40% ya wazee wakazi wa bara hili hawajui kusoma na kuandika.

6. Vita ya pili ya Kongo ndiyo vita hatari kutokea duniani baada ya Vita ya Pili ya dunia. Vita hii iligharimu uhai wa watu takribani milioni 5.4

7. Jangwa la Sahara ni kubwa kuliko yote duniani na ukubwa wake ni zaidi ya nchi ya Marekani.

8. Kuna zaidi ya wachina milioni 1 katika baraka la Afrika. Nchi ya Angola ikiwa na zaidi ya wachina 350,000.

9. Kiwango cha ukataji miti barani Afrika ni mara mbili ya kiwango chote cha ukataji miti duniani. Zaidi ya hekta milioni 4 zinakatwa miti barani hapa kila mwaka.

10. Ziwa Victoria ni ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika huku likiwa ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani na kuwa na maji laini duniani.

11. Wanyama kama vile twiga, pundamilia, viboko, sokwe na nyumbu ni wanyama pekee wanaopatikana katika bara hili.

12. Ziwa Nyasa ambalo kwa jina jingina linaitwa Ziwa Malawi ndilo ziwa lenye aina nyingi za samaki (fish species) kuliko maziwa mengine duniani.

13. Bara hili lina zaidi ya asilimia 85 ya Tembo wote wanaopatikana duniani kote, pia, 99% ya Simba waliosalia duniani wanapatikana katika bara hili. 

14. Mto Naili ambao una urefu wa kilomita 6,650 ni mto mrefu kuliko yote duniani na unapatikana katika bara hili.

15. Mbuga ya Serengeti ambayo inapatikana nchini Tanzania ni hifadhi pekee ambayo ina kundi kubwa la wanyama duniani ikiwa na pundamilia zaidi ya 750,000. Katika hifadhi hii nyumbu zaidi ya milioni 1.2 huhama kila mwaka kutoka hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania kuelekea katika hifadhi ya Masai Mara iliyoko Kenya. Katika kundi hilo la nyumbu wanaohama kila mwaka kutafuta malisho wanyama kama pundamilia, swala na pofu huwepo katika uhamaji huo ambalo ni tukio la kipekee duniani.

16. Bara la Afrika lina zaidi ya 25% ya aina ya ndege wote wanaopatikana duniani.

17. Zaidi ya mabwawa 1,270 yamejengwa kandokando ya mito barani hapa. Mabwawa haya yana kazi kubwa ya kuzalisha umeme unaotumia ngumu za maji.

18. Bara la Afrika ni la pili kwa ukubwa na bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya bara la Asia. Afrika ina takribani watu bilioni 1.2 na hii ni kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa mwaka 2015. Hii ni sawa na 16% ya idadi yote ya watu waliopo duniani.

19.  Afrika ni bara la pili kwa kuwa na joto baada ya bara la Australia.

20. Uislamu ni dini yenye wafuasi wengi barani Afrika ikifuatiwa na dini ya Kikristo huku ikikadiriwa kwamba takribani 38% ya Wakristo wote wataishi kusini mwa jangwa la Sahara mpaka kufikia mwaka 2050.

21. Afrika ni bara lililopo katika nyuzi 0 (0°) katika mstari wa grinwichi meridiani na ikweta.

22. Nchi kubwa kuliko zote barani Afrika ni Algeria ikiwa na eneo la kilomita za mraba milioni 2.381 ikifuatiwa na DR Congo yenye eneo la kilomita za mraba 2.844 wakati nchi ndogo kuliko zote ni Shelisheli yenye eneo la kilomita za mraba 459.

23. Nigeria ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika ikiwa na takribani watu wanaokadiriwa kufika milioni 218.5 hadi kufikia mwezi Septemba 2023. Hii ni sawa na 18% ya watu wote wanaoishi barani hapa. Pia, hii ni sawa na 2% ya watu wote wanaoishi duniani.

24. Umbali mfupi kati ya Ulaya na Afrika ni kilomita 14 sawa na maili 8.7 ukipitia mlango bahari wa Gibraltar.

24. Maporomoko ya Victoria yaliyopo kati ya mpaka wa Zambia na Zimbabwe ni maporoko ya makubwa zaidi ya maji kuliko yote duniani. Pia, ni moja kati ya maajabu saba ya dunia.

25. Kiboko ni mnyama hatari sana barani Afrika kuliko hata Simba na Chui. Anaua watu wengi kuliko Simba na Mamba wakijumlishwa kwa pamoja.

26. Takribani 90% ya wagonjwa wa Malaria duniani kote wanapatikana barani hapa. Ugonjwa huu unaua takribani watoto 30,000 kila mwaka.


27. Nchini Eswatini (Swaziland) katika kila watu 4 kati yao 1 ni muathirika wa UKIMWI.


28. Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na walemavu wengi wa ngozi (albino) kuliko nchi nyingine duniani. Wakati katika mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara ikikadiriwa kuwa mtu 1 katika watu 5,000 hadi 15,000 ana ualbino, kwa Tanzania mtu 1 katika watu 1,500 ana ualbino. Hii inaifanya Tanzania kuwa na watu wengi wenye ulemavu huu wa ngozi kuliko nchi nyingine duniani kote. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. 


29. Misri ni nchi inayoongoza kwa kutembelewa na idadi kubwa ya watalii kuliko nchi nyingine barani hapa. Inapokea watalii zaidi ya milioni 10 kila mwaka 


30. Bendera ya nchi ya Msumbiji ni bendera pekee barani Afrika kuwa bendera ya taifa yenye silaha aina ya AK-47. Silaha hiyo inaashiria ulinzi wa nchi hiyo. Msumbiji ni nchi pekee yenye bendera yenye silaha ya aina hiyo duniani. Nchi nyingine zenye bendera zenye silaha duniani ni Guatemala na Haiti.


31. Bara la Afrika lilikuwa limeungana na mabara mengine miaka mingi iliyopita, lilitengana na mabara hayo katika kipindi cha kijiolojia (taaluma ya miamba na muundo wa ndani wa dunia) katika kipindi cha kijiolojia kiitwacho Mesozoic.


32. Ustaarabu (Civilization) ulianzia barani Afrika. Misri inapata sifa hii kwa kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa ustaarabu wa kifarao ambao ulianza mwaka 3300 kabla ya Kristo.


33. Shelisheli ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na pato kubwa la taifa (GNP). Pato lake linakadiriwa kuwa takribani dola za marekani milioni  15,400 huku Sudan Kusini ikiwa ndiyo yenye pato dogo zaidi ambalo linakadiriwa kuwa dola milioni 245.9.


34. Jangwa la Sahara ndilo jangwa lenye joto zaidi kuliko yote duniani. Linachukua eneo la mraba takribani milioni 9.1 ya majangwa yote duniani.

35. Kama jinsi ilivyo katika bara la Asia, barani hapa pia watu hutembea takribani maili 3.7 kila siku kutafuta maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali.


36. Madagascar ni kisiwa kikubwa kuliko vyote barani Afrika na kisiwa cha 4 kwa ukubwa duniani. Kinapatikana mashariki mwa bahari ya Hindi.


37. Tembo ni mnyama mkubwa kuliko wote duniani na anakadiriwa kuwa na uzito wa tani 6 hadi 7 anapatikana barani Afrika pekee huku Twiga akiwa ni mnyama mrefu kuliko wote dunani naye anapatikana Afrika tu. Pia, mnyama anayekimbia sana kuliko wote ambaye ni Duma anapatikana Afrika pekee huku Mamba akiwa ni mnyama mkubwa kuliko wote katika jamii ya reptilia naye anapatiakana Afrika pekee.


38. Mabaki ya mtu wa kale zaidi yalipatikana barani hapa nchini Ethiopia. Mabaki hayo yanaaminika kuwepo toka miaka laki 2 iliyopita. Charles Darwin alikua akishikilia dai hili lakini lilipingwa na waz
ungu mpaka ilipogundulika katika karne ya 20.

39. Inakadiriwa kwamba takribani watu milioni 12.5 walitekwa barani hapa na kuuzwa katika bara la Amerika kama watumwa kati ya mwaka 1525 hadi 1866.


40. Wakati nchi ya Misri inasifika kwa umaarufu wa kuwa na mapiramidi mengi duniani, Sudan ni nchi pekee yenye idadi kubwa ya mapiramidi hayo ambayo yanakadiriwa kufikia 223 hii ikiwa ni mara mbili ya mapiramidi yote yanayopatikana nchini Misri.


41. Nchini Kenya kuna kabila linalojulikana kama Kalenjin ambalo ni kabila maarufu kwa kutoa wakimbiaji wanaoongoza kwa mbio za riadha duniani.


42. Taasisi ya Elimu kongwe kuliko zote duniani ambayo bado inatumika mpaka leo ipo barani hapa. Taasisi hiyo ni Chuo Kikuu cha Al-Karaouine ambayo iko Morocco. Taasisi hii ilianza kama madrasa na ilianzishwa mwaka 859 baada ya Kristo na ilianzishwa na Fatima Al-Fihri.


43. Takribani 60% ya bara la Afrika ni kame. Sehemu hii inasababishwa na uwepo wa majangwa ya Kalahari, Sahara na Namib.


45. Bara la Afrika lina 30% ya madini yote yanayopatikana duniani.


46. Nigeria ni nchi ya 4 kwa kuzalisha mafuta duniani. Nchi 10 zinazoongoza kwa kuzalisha mafuta barani hapa ni Nigeria, Algeria, Angola, Libya, Misri, Sudan, Guinea ya Ikweta, Congo Brazzaville, Gabon na Afrika ya Kusini.


47. Bara hili lina 40% ya akiba madini ya dhahabu, 60% ya ziada ya madini ya shaba na 90% ya madini ya platini.


48. Zaidi ya 55% ya nguvu kazi ya Afrika wanajihusisha na kilimo cha mazao ya chakula ambayo pia ni sekta inayokuza uchumi barani hapa.


49. Zaidi ya 90% ya udongo wa bara hili sio rafiki kwa kilimo, ni 0.25% ya udongo ambayo ni rafiki kwa kilimo barani hapa.


50. Zaidi ya watu milioni 300 barani hapa wanategemea maji yanayotoka chini kwa matumizi ya kunywa. Maji ni tatizo katika bara hili.


51. Bara la Afrika lina naeneo zaidi ya 3,000 yanayolindwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya utalii duniani. Takribani maeneo 198 ya bahari, maeneo 129 yanayohifadhiwa na UNESCO kama maeneo ya urithi wa kujivunia na maeneo 80 chepechepe (wetland) ambayo ni ni muhimu kimataifa.


52. Afrika ni bara maskini kuliko yote duniani. Pato lake ni 3.1% ya pato lote la dunia kwa mwaka kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia.


53. Wayunani wa kale na Warumi walitumia neno Afrika wakimaanisha ukanda wa kaskazini mwa Afrika peke yake. Katika lugha ya kilatini Afrika ina maana ya ~enye hali ya jua. Wayunani wanatambua kama Aphrike wakiwa na maana kwamba ~isiyo na baridi.


54. Afrika ni bara pekee lenye kingo fupi za kanda za pwani licha ya kua bara la pili kwa ukubwa.


55. Katika bara hili wanawake wanakadiriwa kufanya kazi masaa mengi kuliko wanaume. Wanawake hufanya kazi masaa 12 hadi 14 kwa siku barani hapa.


56. Chura mkubwa zaidi kuliko wote duniani maarufu kwa jina la Goliath anapatikana nchini Guinea ya Ikweta.


57. Benin ni nchi pekee duniani ambayo inashikiria rekodi ya kuwa nchi yenye vizazi mapacha kuliko nyingine zaidi duniani. Katika kila vizazi 1,000 nchini Benin 27.9 ni vizazi vya watoto mapacha. Takwimu ya dunia ni utokeaji wa vizazi mapacha 13.6 katika vizazi 1,000.


58. Niger ni nchi inayoongoza kwa kuwa wanawake wenye uwezo mkubwa wa kuwa na vizazi. Inakadiriwa kua kila mwanamke nchini humo ana watoto 6.62. Burundi ni nchi inayofuatia baada ya Niger ikiwa na 6.04 na hii ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016 kutoka mtandao wa Statista "The Statistical Portal"


59. Kahun ni jiji la kwanza chini ya mipango miji duniani. Jiji hili lipo nchini Misri. 


60. Afrika ni bara linaloongoza kwa vifo vya Mama na mtoto wakati wa kujifungua.


61. Takribani watu milioni 589 kusini mwa jangwa la Sahara wanaishi bila umeme. Hii ni sawa na 20% tu wakati 80% wakiishi kwa kutegemea vyanzo vingine vya nishati kama vile kuni na mkaa kwa ajaili ya kupikia.


62. Inakadiriwa kwamba mtoto 1 katika 3 kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika wana utapiamlo.


63. Bara la Afrika linakadiriwa kua na watumiaji wa mtandao (Internet) milioni 453.3 ambao ni sawa na 35.2% ya wakazi wote wa bara hili. mpaka kufikia Desemba 31, 2017 huku kukiwa na watumiaji milioni 177 wa Facebook. Mwaka 2000 bara la Afrika lilikua na watumiaji wa mtandao milioni 4.5. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa mtandao wa Internet World Stats.


64. Nchi zote 54 za bara hili ni nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Morocco iliwahi kujitoa katika umoja huu na baadaye iliamua kurejea tena. Umoja huu ulianzishwa mwaka 1963 kama OAU na baadaye ulibadilishwa kua AU mwaka 2002. Makao yake makuu yapo Addis Ababa, Ethiopia.

65. Bara la Afrika ndilo lenye nchi nyingi kuliko bara lilingine duniani.



Orodha hii imeandaliwa kwa msaada wa mtandao. Haya ni baadhi ya machache kati ya mengi unayopaswa kuyafahamu na ni jukumu lako kutafuta mengine mengi ya kufahamu. Kwa maoni na ushauri niandikie kupitia:
📧 venancegilbert@gmail.com
📞 0753400208.

ZIJUE FAIDA NA HASARA ZA KUWA NA AKAUNTI BINAFSI "PRIVATE" KATIKA MTANDAO WA INSTAGRAM


Uhali gani mpenzi msomaji wa segment yetu ya Fahamu? Nakukaribisha katika segment yetu ya kila siku ya Fahamu, kama ilivyo kawaida, hapa nakufahamisha mambo kadhaaa ambayo labda hukuyafahamu ama uliyafahamu ila si kwa kina basi huwa nakufahamisha hapa. Kumekuwepo na akaunti nyingi binafsi hasa hasa zile za watoto wa kike kwenye mtandao wa Instagram. Kuna faida na hasara za kuweka akaunti yako kuwa binafsi na hasara zake pia. Leo nakuletea mada kuhusu faida na hasara za kuwa na akaunti binafsi ambazo hizi ndizo zinazotofautisha kua na akaunti huru na binafsi:
Related image
Huu ni mfano wa akaunti binafsi ya Instagram ukiitembelea
FAIDA ZAKE
1. KUA NA MAMLAKA YA KURUHUSU AMA KUTORUHUSU NANI AKUFUATE
Unapaokuwa na akaunti private ya instagram basi unakua na uwezo wa kuamua mwenyewe kwamba nani akufuate (following) na nani asikufuate kwa mfano unaweza kuzuia watu ambao ni wanafamilia ikiwa akaunti yako ina mambo yako ya siri lakini hii haizuii wao kuangalia kwa maana bado wanaweza kutumia majina usiyoyafahamu. Kila anayetaka kua mfuasi wako anapata ruhusa kutoka kwako kabla ya kua mfuasi. Huu ni usalama binafsi kwa namna moja ama nyingine.

2. INAZUIA MUINGILIANO NA MITANDAO NA TOVUTI NYINGINE
Unapokuwa na akaunti binafsi unazuia muingiliano wa mitandao mingine na tovuti nyingine kwa mfano muingiliano wa tovuti nyingine hii inakupunguzia uwezo wa kupata wafuasi wapya kwa maana.

3. INAZUIA WATU KUDOWNLOAD PICHA NA VIDEO UNAZOWEKA
Hii kwa namna moja ama nyingine inaweza kua ni faid na pia hasara kwa namna nyingine. Instagrama inazuuia uwezo wa watu kudownload picha na video zako kama akaunti yako ni private hii inatokana na kufunga link ya kudownload. Hii ni kwa wafuasi wako kwa maana ndiyo wenye uwezo wa kuiona akaunti yako.

4. INAZUIA WATU KUWAONA WAFUASI WAKO NA WALE ULIOWAFUATA
Kama bado hujakubaliana na ombi la mtu kukufuata inakua ni vigumu kwa yeye kuwaona wafusai wako hii ni kwa sababu sera ya faragha inazuia isntagram kutoa taarifa zako kama hizi; wafuasi na uliowafuata, picha na video zako lakini hii haizuii wasifu wako (bio) kutoonekana.


HASARA ZAKE
1. INAKUPUNGUZIA IDADI YA WAFUASI
Wapo watu ambao kwa namna moja huja kwenye akaunti yako kuangalia picha na video unazoweka ili wakufuate mtandaoni hapo hivyo wanapokuta akaunti yako ni binafsi na kutoona taarifa zako kama vile picha na ama makala zako basi wanaamua hata kutokukufuata kabisa. Kuna wakayti unashea na watu picha yako katika mitandao ya Facebook na Twitter na hivyo watu wakavutiwa na kukufuata lakini wanapokuta aaunti yako ni binafsi wanaamua kuachana na akaunti yako.

2. INAPUNGUZA MUINGILIANO
Unapokua na akaunti binafsi unapunguza uwezo wa watu kuingiliana na akaunti yako kwa mfano kupata watembeleaji wapya, kufanya biashara na watu kupitiaa Instagram na hata kufanya matangazo na mtaandao wa Instagram (Sponsored links) Ni lazima iwe akaunti huru kwa umma ili uweze kupata miingiliano kama hii na mingineyo.

3. INAKUPUNGUZIA WATEJA KAMA NI AKAUNTI YA BIASHARA
Kama wewe ni mfanya biashara na akaunti yako unaiendeza kwa msingi wa kuwa akaunti binafsi fahamu kwamba unapunguza idadi kubwa sana ya wateja yako. Hii inafanya watembeleaji wapya wasiwe na uwezo wa kuziona picha zako za matangazo ya biashara. Instagram ni mahala pazuri sana kutangaza biashara yako kwa vile inaruhusu picha na maelezo yake.

4. INACHOSHA KUPITIA MAOMBI YA WATU WANAOTAKA KUKUFUATA
Inaweza kua suala la kawaida kupitia maombi ya watu wanaotaka kukufuata lakini ni usumbufu pia na inachosha kupitia maombi yote has pale idadi ya watu wanaotaka kukufuata inapokuwa kubwa. Unapokua na akaunti huru unapata tu taarifa kwamba mtu fulani kakufuata basi.


Kwa Maoni na Ushauri wasiliana nami kwa moja kati ya njia hizi:
Barua pepe: venancegilbert@gmail.com
Simu: 0712586027 (na WhatsApp pia) na 0753400208.

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

Lugha ya Kiswahili inazungumzwa katika nchi za Afrika Mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda.

Zaidi ya watu milioni 15 katika bara hili huitumia lugha hii kama lugha ya kwanza na wazungumzaji wengine wakiitumia kama lugha ya pili au ya tatu. Ni lugha rasmi ya Muungano wa Afrika. Hii inafanya bara hili kuwa na idadi inayozidi milioni 100 ya wazungumzaji wa lugha hii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi zinazoongoza kwa kua na idadi kubwa ya wazungumzaji barani Afrika.

TANZANIA

Kiswahili nchini Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa Mtanzanianainatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na umoja wa kitaifa.
Katika kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu. Taasisi mbalimbali zimebuniwa kuhusu lugha hii kama vile BAKITA, BAKIZA, Taasisi ya Elimu, UWAVITA, TATAKI (zamani TUKI pia TAKILUKI) na UKUTA. Pia vyuo vikuu mbalimbali vya Bara na Visiwani vilianza kufundisha Kiswahili kuanzia Shahada za Awali, Uzamili na Uzamivu kama vile Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Huria cha TanzaniA, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino n.k.

KENYA

Kiswahili nchini Kenya ni lugha rasmi na pia ni lugha ya Taifa. Rais wa kwanza wa taifa la Kenya hayati Mzee Jomo Kenyatta alitoa kauli kwamba Kiswahili kinafaa kutumika kama lugha rasmi ya Kenya mwaka 1969. Mwaka 1975 kiswahili kilianza kutumika bungeni.Serikali ya Kenya ilianzisha somo la Kiswahili katika Idara ya Lugha za Kiafrika na Isimu ya Chuo Kikuu cha Nairobi. Kuanzia miaka ya themanini mwishoni, takribani vyuo vikuu vyote vilivyoanzishwa na Serikali vilifundisha masomo ya Kiswahili kwa lugha ya hii.

UGANDA

Mwaka 1960, Serikali ya Uganda iliruhusu na kulazimisha Kiswahili kitumike nchini humo. Kiingereza na lugha za kikabila zilikuwa tayari zinatawala mawasiliano Uganda nzima. Lugha ya maandishi ya Kiswahili yalianza kutumika katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro hata kabla ya ukoloni mwaka 1862. Kiswahili hutumika katika shughuli za biashara, dini na mila.
Nchini Uganda Kiswahili kilifikiriwa kwamba ni lugha ya watumwa. Lakini Kiswahili kilitumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi.
Wikendi hii Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, Keneth Cimara imeipongeza serikali ya Uganda kwa juhudi ya kuendeleza Kiswahili tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Katika warsha ya siku mbili iliyokamilika mwishoni mwa juma katika hoteli ya Imperial Royal mjini Kamapla iliyowajumuisha walimu wa vyuo vikuu, shule za upili na taasisi mbalimbali nchini Uganda.
Keneth Cimara amesema miaka ya themani raia wengi wa Uganda walikiona Kiswahili kama lugha ya wahalifu ikitumiwa na askari kuwanyanganya mali zao, aidha kuwatendea uhalifu.
Cimara ameongeza kwamba sasa Serikali ya Uganda ni miongoni mwa mataifa ya Jumuia ya Afrika Mashariki ambayo yameweka mikakati ya kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahi kama anavyosema tena Katibu mtendaji.


RWANDA

Kiswahili ni lugha rasmi nchini Rwanda. Kabla ya mwaka 1994, wakati wa mauaji ya kimbali lugha ya kiswahili ilizungumzwa kwenye miji tofauti nchini Rwanda.
Lugha ya Kiswahili ilisambaa baada ya Wanyarwanda kuwaruhusu Wajerumani nchini mwao kama watawala karne ya 19.
Mwaka wa 1976-1977 lugha ya Kiswahili ilianza kufundishwa katika shule za upili na chuo Kikuu Cha Rwanda

JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Kiswahili kiliingia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kuanzia karne ya 19. Kiswahili kilianza kuenea kutoka Mashariki mwa nchi hiyo, kuelekea kandokando ya mto Kongo.

Pia kuna wazungumzaji wachache katika nchi za Burundi, Msumbiji, Comoros, Malawi , Madagascar na Zambia.


Chanzo: BBC

FAHAMU MAMBO HAYA 20 KUHUSU TANZANIA

tanzania flagLeo nakufahamisha baadhi ya mambo ambayo huenda hukuyafahamu ama ulichukulia kawaida tu. Mambo hayo ni hapahapa Tanzania.  Tanzania ina eneo la kilomita za mraba 945,087. Ina jumla mikoa 31 kote bara na visiwani. Mpaka kufikia mwaka 2017 idadi ya watu nchini ilikadiriwa kuwa milioni 52.554 kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya takwimu. Twende sasa tuanze kuhesabu moja baada ya jingine


#1. Wimbo wa taifa "Mungu Ibariki Tanzania" ni wimbo unaofanana na nyimbo za mataifa ya Afrika Kusini na Zambia. Wimbo huu ulitungwa na Enock Sontonga kwa lugha ya Xhosa "Nkosi Sikelel iAfrika". Wimbo huu pia uliwahi kutumiwa na nchi za Zimbabwe na Namibia.
Image result for enoch sontonga
Enock Sontonga mtunzi wa wimbo Mungu Ibariki Afrika


#2. Ni Tanzania pakee ambako kunapatikana Simba wenye uwezo wa kupanda juu ya miti. Simba hawa wanapatikana katika hifadhi ya taifa ya Ziwa Manyara.
bwindi-and-serengeti-safari_18889423181_o
Simba wenye uwezo wa kupanda miti hifadhi ya Ziwa Manyara.


#3. Tanzania ni nchi ambako fuvu la mtu wa kale zaidi liligunguliwa. Fuvu hili liligunguliwa katika bonde la Olduvai mwaka 1959 na Dr. Louis Leakey.
Olduvai Gorge


#4. Tanzania in Mlima Kilimanjaro ambao ni Mlima mrefu kuliko yote barani Afrika. Mlima huu una urefu wa mita 5895.
Related image



#5. Pamoja na kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa, Tanzania inayo makabila 120 ambayo yana mila, desturi na tamaduni tofauti tofauti. Makabila haya yanaishi vyema na kuelewana chini ya mwamvuli wa Utanzania na lugha ya taifa ya Kiswahili.
Related image
Ramani ya Tanzania ikionesha Makabila

#6. Uwepo wa Ziwa Tanganyika ambalo ni ziwa lenye kina kirefu kuliko yote barani Afrika. Ziwa hili lina kina cha futi 4823 ambazo ni sawa na mita 1470. Ziwa hili pia lipo katika nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi na Zambia. Ziwa hili pia ni la pili duniani kwa kuwa na kina kirefu zaidi baada ya ziwa Baikal likifuatiwa na Caspian.
Related image
Ziwa Tanganyika

#7. Tanzania ina zaidi ya wanyama pori milioni 4 ambao wamegawanyia katika makundi 430 tofauti ya wanyama.



#8. Hifadhi ya taifa ya Serengeti ni hifadhi maarufu kwa kuwa na mimea na wanyama wa aina tofauti tofauti. Pia ni mbuga inayoongoza kwa kuwa na makundi makubwa ya wanyama wanaohama kila mwaka kundi kubwa likiwa ni kundi la nyumbu. Mwaka 1981 hifadhi hii ilitajwa na UNESCO kama sehemu ya urithi wa kujivunia duniani.
Image result for ngorongoro
Hifadhi ya Serengeti.


#9. Tanznaia ina hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ambayo ni maarufu kwa kuwa na ziwa ambalo limetokana na mlipuko wa Volkano; Ziwa Magadi ziwa hili lina kilomita za mraba 264 na maarufu kwa kuwa na ndege wengi aina ya flamingo. Eneo hili la Ngorongoro lina aina mbalimbali za wanyama kama vile tembo, faru, kiboko, pundamilia, nyati n.k. Katika eneo hili jamii ya Wamasai hufanya shughuli zao za ufugaji. Hifadhi hii ilitajwa kama eneo la urithi wa kujivunia wa dunia mwaka 1979.
ngorongoro conservation area
Hifadhi ya Ngorongoro

Ngorongoro-Crater
Ziwa Magadi linalopatikana hifadhi ya Ngorongoro


#10. Tanzania ina mji eneo maarufu kwa kivutio cha utalii ambacho huitwa mji mongwe. Eneo hili lipo Unguja-Zanzibar. Kitovu cha historia yake ni Mji Mkongwe (Stone Town) ulioandikishwa katika orodha ya UNESCO ya “Urithi wa Dunia” (World Heritage). Nyumba za Mji Mkongwe zilijengwa tangu mwaka 1830 wakati Sultani Sayyid Said alipohamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja Unguja.
Image result for mji mkongwe wa zanzibar
Mji Mkongwe uliojengwa tokea enzi za utawala wa Waarabu wa Omani

#11. Uwepo wa daraja la Nyerere linalounganisha wilaya ya Kigamboni kupitia Kurasini. Ujenzi wa daraja hili ulianza Februari 2012 na kukamilika April 2016. Daraja hili lina urefu wa mita 680.
Image result for kigamboni bridge
Daraja la Nyerere linalounganisha wilaya ya Kigamboni na kata ya Kurasini kupitia mkondo bahari wa Kurasini


#12. Ziwa kubwa kulio yote Afrika na Ziwa la tatu kwa ukubwa duniani; Ziwa Victoria lipo Tanzania kwa kiasi kikubwa likipakana na nchi za Uganda na Kenya. Ziwa hili lina ukubwa wa eneo la mraba 68,870 likiwa na urefu wa kilomita 332 na kina cha mita 84 sawa na futi 276.
Related image
Ziwa Victoria

#13. Pengine kuna hili hukulifahamu. Tanzania ina majiji 6 kwa sasa Dar es Salaam likiwa ni jiji kubwa kuliko yote, likifuatia jiji la Mwanza, Arusha na majiji ya Mbeya, Tanga na jiji pipya la Dodoma ambalo limepata hadhi ya jiji April 26, 2018 siku ya kumbukumbu ya maandhimisho Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 19964.
Ramani ya Tanzania ikionesha mikoa yake (mikoa michache haijaoneshwa katika ramani hii)


#14. Kuna fukwe (beach) nzuri na za kuvutia pindi unapohitaji sehemu ya kupunga upepo baharini. Coco beach, Landmark, Ocean view, Lamada, Nungwi, Sea cliff, Zanzi Resort, Tanga beach, Mbezi beach, Malaika Beach Resort n.k. ni baadhi ya fukwe maarufu nchini
tanzania beach



#15. Tanzania inapakana na nchi 8 ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Zambia na Msumbiji.
Image result for tanzania map with lakes



#16. Tanzania ilisaidia nchi nyingi za Kusini mwa Afrika kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni; nchi hizo ni Jamhuri za Afrika ya Kusini, Angola, Namibia, Msumbiji na Zimbabwe. Mwalimu Nyerere aliwasaidia wapigani uhuru wa vyama vya ANC, MPLA, SWAPO, FRELIMO na ZANU. 
Related image


#17. Tanzania ina kisiwa kikubwa katika visiwa vyote vilivyo ndani ya maziwa ya bara la Afrika; Kisiwa cha Ukerewe ambacho kina eneo la kilomita za mraba 530. Kisiwa hiki kinapatikana ndani ya Ziwa Victoria. Huenda hukuifahamu hii, basi nimekufahamisha.
Image result for ukerewe map
Kisiwa cha Ukerewe kama jinsi ramani inavyoonekana kwa juu.
Image result for ukerewe map
Kisiwa cha Ukerewe (rangi nyekundu)
#18. Tanzania kuna mawe ambayo ni kuvutio kikubwa cha utalii nchini. Mawe haya yamebebana bila kudondoka kwa miaka mingi sasa. Ni maarufu kama Bismarck rock. Yapo jijini Mwanza na yamewekwa katika noti ya Tsh. 1,000/=
Image result for bismarck rock
Mawe ya Bismarck ambayo ni maarufu sana nchini

#19. Uwepo wa banadari ya Dar es Salaam ambayo inakuza uchumi na pato la taifa kwa kuingiza na kusafirisha bidhaa ndani na nje ya nchi. Bandari hii inasaidia pia nchi za Congo DR, Rwanda, Zambia, Burundi na Malawi.
An aerial view of a section of the port. Credit: Tanzania Ports Authority
Picha ya Bandari ya Dar es Salaam kama ilivyopigwa kutoka juu.

#20. Tanzania ina maeneno 7 ambayo yalitangazwa kuwa ni maeneo ya urithi wa kujivunia duniani. Maamuzi hayo yalitajwa kwa nyakati miaka tofauti na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO). Maeneo hayo ni haya yafuatavyo:
  • Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
  • Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro
  • Mlima Kilimanjaro
  • Magofu ya kale ya Kilwa na Songa Mnara
  • Michoro ya Mapangoni ya Kondoa
  • Hifadhi ya Wanyama ya Selous
  • Mji Mkongwe Unguja.


Picha zote kwa msaada wa mtandao. Picha hizi si miliki ya blogu hii, kila picha ina mmliki wake.
Unaweza kuacha maoni yako chini ya chapisho hili ama kutuma barua pepe kupitia venancegilbert@gmail.com kama una lolote la kusema ama kuwasiliana nami kwa WhatsApp namba +255712586027 ama kunipigia kwa namba +255753400208.

FAHAMU MAKALA BORA ZA KISAYANSI ZILIZOSAIDIA JAMII 2017


Karibu ndugu msomaji wa VENANCE BLOG. Leo nimekuletea makala fupi zakisayansi ambazo zilipata umaarufu kwa mwaka huu kwa ufupi sana, na tuanze sasa

Biashara ya siri kuuzwa sokwe Afrika Magharibi









Nemley junior, the infant rescued from traffickers after our investigation

David Shukman na Sam Piranty walifanya utafiti mrefu Afrika Magharibi na BBC kugundua mipango ya siri inayohusiana na uuzwaji wa wanyamapori hasa sokwe. Hii ilisaidia kunusurika kwa sokwe aitwaye Nemley Jr ambaye alikuwa na umri wa mwaka mmoja.


Mtambo wa Kupunguza Kabonidayoksaidi angani

fans
Katika mwaka 2017, riport zilionesha kwamba kuna mrundikano mwingi wa gesi ya kabonidayoksaidi angani mpaka kufikia wingi huo kuvunja rekodi huku juhudi za kimataifa zikishindwa kutatua changamoto hiyo ili kuepuka hatari ya kuongezeka kwa joto duniani. Je teknolojia hiyo inaweza kuondoa gesi hiyo ya kabonidayoksaidi ili kujibu maswali mengi ambayo juhudi za kimataifa zimekua zikishinwa kujibu? Hii iliandikwa na Matt McGrath.

Misheni ya Anga ya Cassini kuitafiti sayari ya Sarateni ilivyokamilika

Artist impression of Saturn and its rings 
Misheni ya anga ijulikanayo kwa jina la Cassini space missionilifikia tamati  mwezi Septemba 2017, baada ya kutumia miaka13 kuchunguza sayari ya Sarateni (Saturn) pamoja na mwezi wa sayari hiyo. BBC iliweza kuonesha makala ya utafiti huo wa anga na jinsi utafiti huu wa anag unaharibu tabaka la hewa la sayari hiyo, lakini pia walihakikisha misheni hiyo walipata nafasi ya kuelezea uzoefu wao kuhusu utafiti huo wa aga. Makala hii iliandikwa na Paul Rincon.

Jinsi dunia yetu inavyofanya kazi zake kijiolojia

Dan McKenzie
Je, ni mambo gani ungeyaweka katika orodha ya mambo makubwa ya kisayansi yaliyowahi kutokea katika karne ya 20? Ugunduzi mkubwa zaidi ni ule unaofahamika kisayansi kama plate tectonic. Nadharia hii ina miaka 50 sasa, ni nadharia iliyotoa majibu ambayo kwa kiasi kikubwa yanaelezea sababu za kutokea kwa volkano na matetemeko ya ardhi. Makala hii iliandikwa na Jonathan Amos.

Ugunduzi ma utengenezaji wa Mtandao (Internet) wa kizazi kijacho

The global internet
Kompyuta zenye kasi zaidi zinagunduliwa na kutengenezwa mahali kote duniani. Lakini je, ni kwa nanmna gani kizazikijacho kitatumia komputa hiyo? Wanasayansi tayari wameanza kufikiria namna ya spidi ya mtandao (internet) abayo itaendana na kompyuta hizo. Makala hii iliandikwa na Mary-Ann Runson.

Trump kujenga ukuta mpakani na Mexico kunaharibu uoto wa jangwani mahala hapo pakijengwa

Skull
Rais wa Marekani Donald Trump aliahidi kujenga ukuta  ambao ungetumika kama mpaka kutenganisha nchi hiyo na Mexico, lakini ahadi hii bado inakua ngumu kutekelezeka katika utawala wake huu. Wanasayansi tayari wameanza kuzungumzia madhara ya kiikolojia yatakoyotokana na ujenzi wa ukuta huo. Ujenzi huo utaathiri uoto wa jangwa. Wasayansi hao wanafanya utafiti katika jangwa la Sonoran ambalo tayari lina mpaka unaolitenganisha Marekani na Mexico.Makala hii iliandikwa na Victoria Gill.

Mapinduzi katika ugunduzi wa kupata taarifa za kigenetiki (urithi) kuwafikia watu bilioni1 nchini India

Delhi Metro
Je, jitihada inaweza kutumika nchini India kukusanya taarifa hizi za kijenetiki kutoka katika idadi yake ya watu bilioni 1 ili kuboresha huduma za afya nchini humo? Hii iliandikwa na Kat Arney.

Ndege wanaoukamwatwa na kuuzwa kwa kuwa na sauti zinavutia

SongbirdNdege waliokuwa wanaimba vizuri zaidi yani sauti zao zinavutia wamekuwa wakikamatwa kwenye misitu huko Indonesia na kuuzwa. Hali hii inahatarisha uwepo wa viumbe hawa. Makala hii iliandikwa na Victoria Gill.


Mapinduzi katika utabiri wa hali ya hewa baada ya mwaka 1987

SupercomputerOktoba 15, 1987 kituo cha hali ya hewa cha nchini Uingereza kupitia BBC kilikanusha taarifa za kuwepo kwa kimbunga hatari cha Hurricane ambacho kingeikumba Uingereza. Usiku ule, nchi ilikumbwa na upepo mkali uliosababisha watu 18 kufariki. Katika kumbukumbu ya miaka 30 ya tukio hilo David Shukman aliangalia ni kwa namna gani teknolojia ingeweza kubadilisha utabiri wa hali ya hewa.


Binadamu anayeishi na viumbe wa ajabu na hatari zaidi

Ronald JennerHuwezi kuamini katika fikra zako kwamba kuna viumbe hatari sana ambao bado wanaishi mpaka sasa. Dr. Ronald anasoma kwa karibu tabia za viumbe anaoishi nao hasa wale wenye sumu za hatari kwa maisha ya binadamu. Hii ni makala iliyoandikwa na Jonathan Amos.


Jinsi mtafiti wa mimea wa Uingereza alivyoisadia Sayansi

Plant specimens are pressed under large rocks

Katika miaka ya mwanzoni mwa karne ya 20, muwindaji maarufu nchini Uingereza aliyekuwa akiwinda kwa kupanda juu ya miti alihatarisha maisha yake kwa kuingia nchini China kuchunguza mimea iliyokuwa nchini China kwa mgongo wa Sayansi. Kumbukumbu aliyoicha baada ya utafiti huo inapatikana katika bustani zilizopo nchini Uingereza. Makala hii iliandikwa na Helen Briggs.

Utafiti mpya kuhusu ugunduzi wa kufahamu uwezekano kuweko na maisha kwingineko

View of Europa taken in the 1990s by the Galileo spacecraft 
Baada ya miongo miwili (miaka 20) na kushindwa kukamilisha tafiti, wanasayansi hatimaye walifanikiwa kuitafiti bahari ya Europa. Je, huu utakuwa ni utafiti ambao unaweza kujibu maswali kwamba kuna uwezekano wa kuwepo na maisha katika sehemu nyingine tofauti na duniani? Makala hii iliandikwa na Paul Rincon.

Je, nguo zetu zinachafua mazingira?

Washing on the line 
Utafiti wa kisayansi ulionesha kuwa nguo za material ya polyster na acrylic zinatoa material ya plastiki ambayo wakati wa kufua husababisha uchafuzi wa mazingira hasa bahari. Je, tunawezaje kuzuia tatizo hili la uchafuzi wa mazingira. Makala hii iliandikwa na Victoria Gill.

Utafiti mpya kuhusu ndege jamii ya Dodo kuandikwa tena

Rodrigues Solitaire
Wanasayansi wapo katika hatua za mwisho kutengeneza makala ya kibailojia ambao ilipelekea ndege hawa aina ya Dodo kutoweka duniani. Uandishi huo utakuwa ni muendelezo wa utafiti wa mtafiti wa kifaransa aliyewatafiti ndege hao alipokuwa katika safari zake bahari ya Hindi. Makala hii iliandikwa na Rolly Galloway.

Kuna ugumu gani kumkata nzi?

Housefly 
 Jaribu kukamata nzi yeyeote na utagundua kwamba wao huwa na haraka kuliko wewe. Haraka zaidi. Lakini je ni kwa namna gani viumbe hawa wadogo ubongo wao huweza kuhisi hatari mapema sana na kukimbia? Huu ni utafiti wa kisayansi uliofanywa na Rolly Gallway.

Wadudu hatari ambao pia ni muhimu katika mazingira

Wasp
Mapema mwezi wa nane mwaka huu viumbe hawa walivamia hafla iliyokua imeandaliwa na August Bank nchini Uingerza kuliko hata ambavyo mawaingu yangetanda kuashiria mvua. Profesa Adam Hart mwanasayansi wa Uingerza anasema kwamba licha ya kuwa hatari sana, wadudu hawa ni muhimu sana katika ikolojia.

 
Nitumie maoni yako kupitia Whatsapp 0712586027 ama barua pepe venancegilbert@gmail.com. Facebook VENANCE BLOG na Twitter @Venancetz.


MAKALA HII IMEANDALIWA KWA HISANI YA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA NCHINI UINGEREZA; BBC. PICHA KWA HISANI YA GETTY IMAGES, NASA, CLIMEWORKS, THE GEOLOGICAL SOCIETY; MCKENZIE ARCHIEVE, JULIAN HUME, ROYAL BOTANIC GARDEN; EDINBURGH AND RHS, MET OFFICE, NHM, JPL CATECH, SETI INSTITUTE NASCIENCE PHOTO LIBRARY