Posts

Showing posts from September, 2013

UNGEKUWA WEWE UNGEFANYA NINI?

Image
House girl alitandika kitanda cha bosi wake Kama Sehemu ya jukumu lake la kila siku. Alipomaliza akakitazama sana kile kitanda cha bosi wake akasema naweza kufa bure bila ya kulalia kitanda kama hiki. Akasema ngoja nijaribu kulala angalau kidogo.  Akavua nguo zote akaziweka chini, akabaki na gagulo tu akawasha AC akajifunika brangeti gubigubi akalala. Kwa bahati mbaya usingizi ukampitia kweli akalala fofofo. Ghafla Mume wa bosi akarudi na haikuwa kawaida yake kurudi Muda huo. Alipoingia chumbani, akajua hakika huyu ni mke wangu na kwa kuwa jana tulikwaruzana atakuwa amekasirika tu. Akaogopa kumwamsha. Mwanamme akasaula, akabaki na msuli naye akajifunika hilo hilo blanketi kwa taratibu sana kwa hofu ya kumwamsha mke wake. Kwa bahati mbaya naye usingizi ukampitia, akalala fofofo . Bosi aliporudi, akaingia chumbani, akakuta watu wawili wamelala fofofo. Akafunua blanketi kwa nguvu, akawakuta wote wawili; yaani yule mfanyakazi na mume wake wamelala pamoja. Walipoulizwa kila mtu akaele