JESHI LA DRC LAFANIKIWA KUZIMA SHAMBULIO LA KIGAIDI

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limesema kuwa limefanikiwa kuzima shambulio lililolenga uwanja wa ndege na kituo cha taifa cha Radio na Televisheni linalodaiwa kutekelezwa kundi lisilofahamika la kigaidi.Waziri wa habari nchini humo Lambeart Mende amesema kwa sasa hali imedhibitiwa ambapo wamefanikiwa kuwaua watu 40 miongoni mwa waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo.Watu hao waliokuwa na silaha 16 kati yao wameuawa katika mapambano na polisi uwanja wa ndege,16 wengine katika eneo la jeshi na nane wao waliuawa katika ofisi za Radio ya Taifa.Amesema kuwa kulikuwa na matukio mengine mawili ya mashambulizi katika maeneo ya uwanja wa ndege na kambi ya jeshi.Kwa mjibu wa waziri Mende watu hao waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo katika televisheni ya taifa na makao makuu ya radio ya taifa walikuwa na silaha zikiwemo bunduki,visu lakini walidhibitiwa kabla ya kusababisha madhara .Mashambulizi haya yametokea wakati Rais Joseph Kabila akiwa ziarani katika jimbo la Katanga nchini humo.Ubalozi wa Marekani umetoa tahadhari kwa raia wake kutofanya safari za ndani ya mji wa Kinshaasa hadi hali itakapodhibitiwa Zaidi.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017