ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA
Lugha ya Kiswahili inazungumzwa
katika nchi za Afrika Mashariki. Kiswahili hutumika nchini Tanzania,
Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji na Rwanda.
Zaidi
ya watu milioni 15 katika bara hili huitumia lugha hii kama lugha ya kwanza na wazungumzaji wengine wakiitumia kama lugha ya pili au ya tatu. Ni lugha
rasmi ya Muungano wa Afrika. Hii inafanya bara hili kuwa na idadi inayozidi milioni 100 ya wazungumzaji wa lugha hii. Kiswahili ni miongoni mwa lugha kumi zinazoongoza kwa kua na idadi kubwa ya wazungumzaji barani Afrika.
TANZANIA
Kiswahili nchini
Tanzania ni lugha rasmi na lugha ya Taifa. Ni lugha ya utambulisho kwa
Mtanzanianainatumika kama lugha ya kuimarisha uelewano, ushirikiano na
umoja wa kitaifa.
Katika
kuiendeleza, juhudi za usanifishaji zimefanyika kwa kuwatumia wataalamu
wa fasihi na isimu, wadau wengine na wachapishaji vitabu. Taasisi
mbalimbali zimebuniwa kuhusu lugha hii kama vile BAKITA, BAKIZA, Taasisi ya Elimu,
UWAVITA, TATAKI (zamani TUKI pia TAKILUKI) na UKUTA. Pia vyuo vikuu mbalimbali vya Bara na Visiwani
vilianza kufundisha Kiswahili kuanzia Shahada za Awali, Uzamili na Uzamivu kama vile Chuo Kikuu Mzumbe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Huria cha TanzaniA, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino n.k.
KENYA
Kiswahili nchini Kenya ni
lugha rasmi na pia ni lugha ya Taifa. Rais wa kwanza wa taifa la Kenya
hayati Mzee Jomo Kenyatta alitoa kauli kwamba Kiswahili kinafaa kutumika
kama lugha rasmi ya Kenya mwaka 1969. Mwaka 1975 kiswahili kilianza
kutumika bungeni.Serikali ya Kenya ilianzisha somo la Kiswahili katika Idara ya Lugha za Kiafrika na Isimu ya Chuo Kikuu cha Nairobi. Kuanzia miaka ya themanini mwishoni, takribani vyuo vikuu vyote
vilivyoanzishwa na Serikali vilifundisha masomo ya Kiswahili kwa lugha
ya hii.
UGANDA
Mwaka 1960, Serikali ya
Uganda iliruhusu na kulazimisha Kiswahili kitumike nchini humo.
Kiingereza na lugha za kikabila zilikuwa tayari zinatawala mawasiliano
Uganda nzima. Lugha ya maandishi ya Kiswahili yalianza kutumika
katika Baraza la Kifalme la Buganda na Bunyoro hata kabla ya ukoloni mwaka 1862. Kiswahili hutumika katika shughuli za biashara, dini na mila.
Nchini Uganda Kiswahili kilifikiriwa kwamba ni lugha ya watumwa. Lakini Kiswahili kilitumiwa zaidi na Polisi na Wanajeshi.
Wikendi
hii Katibu mtendaji wa Kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki,
Keneth Cimara imeipongeza serikali ya Uganda kwa juhudi ya kuendeleza
Kiswahili tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Katika warsha ya siku mbili iliyokamilika mwishoni mwa juma katika
hoteli ya Imperial Royal mjini Kamapla iliyowajumuisha walimu wa vyuo
vikuu, shule za upili na taasisi mbalimbali nchini Uganda.
Keneth
Cimara amesema miaka ya themani raia wengi wa Uganda walikiona
Kiswahili kama lugha ya wahalifu ikitumiwa na askari kuwanyanganya mali
zao, aidha kuwatendea uhalifu.
Cimara ameongeza kwamba sasa
Serikali ya Uganda ni miongoni mwa mataifa ya Jumuia ya Afrika Mashariki
ambayo yameweka mikakati ya kuendeleza matumizi ya lugha ya Kiswahi
kama anavyosema tena Katibu mtendaji.
RWANDA
Kiswahili ni lugha
rasmi nchini Rwanda. Kabla ya mwaka 1994, wakati wa mauaji ya kimbali
lugha ya kiswahili ilizungumzwa kwenye miji tofauti nchini Rwanda.
Lugha ya Kiswahili ilisambaa baada ya Wanyarwanda kuwaruhusu Wajerumani nchini mwao kama watawala karne ya 19.
Mwaka wa 1976-1977 lugha ya Kiswahili ilianza kufundishwa katika shule za upili na chuo Kikuu Cha Rwanda
JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO
Kiswahili
kiliingia nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kuanzia karne ya
19. Kiswahili kilianza kuenea kutoka Mashariki mwa nchi hiyo, kuelekea
kandokando ya mto Kongo.
Pia kuna wazungumzaji wachache katika nchi za Burundi, Msumbiji, Comoros, Malawi , Madagascar na Zambia.
Chanzo: BBC
Comments
Post a Comment