POLISI WAKAMATA BASTOLA NYUMBA YA KULALA WAGENI
JESHI la Polisi wilayani Igunga mkoani Tabora limefanikiwa kukamata bastola katika nyumba ya kulala wageni ambayo inadhaniwa imesahaulika na majambazi.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi mkoani Tabora, Peter Ouma alisema silaha hiyo imekamatwa juzi katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Sophia Lodge iliyopo mtaa wa Bank, Igunga mjini.Alisema kuwa bastola hiyo yenye namba za usajili 224335 aina ya Browing Court ilidakwa na risasi 38 pamoja na magazini 4.
Comments
Post a Comment