RAIS KIKWETE AKABIDHIWA RASIMU YA KATIBA MPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amekabidhiwa rasimu ya pili ya katiba mpya na tume ya katiba inayoongozwa na mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.Rais Kikwete amesema kuwa kazi iliyofanyika katika mchakato huo imewezesha makundi mbalimbali katika jamii kuchangia mawazo yao kupitia tume aliyoiunda ili kupata mawazo ya watanzania kuhusiana na katiba wanayoitaka.Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amekabidhiwa pia rasmu hiyo na kueleza kuwa kuwa wajumbe watakaoteuliwa katika bunge la katiba wanapswa kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa kamati hii iliyomaliza kazi yake.Jaji mstaafu Warioba amesema rasimu hii wanayoiwasilisha ni ndefu kuliko ile ya awali iliyokuwa na ibara 240 wakati hii ina ibara 271 ikiwa ni matokeo ya tume kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba yaliyotoa maoni mengine mapyaAmeyataja baadhi ya mambo ambayo tume imebaini kuwa yalijadiliwa kwa hisia kali katika rasmu hiyo na ile ya awali kuwa ni suala la muungano hasa kuhusu muundo wake. Amesema wakati tume inazindua rasmi ya awali hawakupendekeza kuendelea kuwa na muundo wa serikali mbili ulihitaji ukarabati mkubwa ambao tume ilifikiri hautawezekana, hivyo mabaraza ya katiba yalitoa mapendekezo mengi yaliyoilazimu tume kufanya uchambuzi wa kina na kwamba iliwachukua muda mrefu wa tume.Jaji Warioba amesema wananchi Zaidi ya 39,000 wa Tanzania bara waliotoa maoni yao kuhusu muungano na kati yao karibu 27,000 walizungumzia muundo na Zanzibar wananchi karibia wote waliotoa maoni walijikita katika muungano ambapo kati ya wananchi 38,000 wa Zanzibar waliotoa maoni 19,000 walizungumzia muundo wa muungano.Tanzania bara asilimia 13 walitaka serikali moja, asilimia 24 walipendekeza serikali mbili na 61 walipendekeza serikali tatu, wakati Zanzibar asilimia 34 walipendekeza serikali mbili na asilimia 60 muungano wa mkataba ambapo asilimia 0.1 walihitaji serikali moja.Hata hivyo Rasimu hiyo ya katiba iliyokabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeorodhesha malalamiko 10 kwa upande wa Zanzibar na manane ya Tanzania BaraMalalamiko matatu makubwa kwa Zanzibar ni Serikali ya Tanganyika kuvaa koti la serikali ya muungano hivyo kupunguza nguvu kwa Zanzibar,Ongezeko la mambo ya Muungano,kumuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.Tanzania bara tume hiyo imeyataja malalamiko kuwa ni kuwa Zanzibar imekuwa nchi huru , ina bendera yake ya Taifa, ina serikali yake ina wimbo wake wa taifa na imebadili katika yake ili itambulike kama nchi wakati Tanzania bara imepoteza utambulisho wake, wananchi wa Tanzania Bara kutokuwa na haki ya kumiliki ardhi Zanzibar wakati wenzao wanamiliki Tanzania bara.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017