BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA

Ramani ya Afrika.
Karibu tena mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG. Leo katika safu yetu ya Fahamu napenda kukufahamisha mambo kadhaa ambayo huenda hukuyafahamu yote kuhusu bara la Afrika. Na tuanze sasa kuyahesabu mambo hayo:


1. Karibu nchi zote za Afrika zilitaliwa na wakoloni isipokuwa nchi mbili tu: Ethiopia na Liberia.

2. Kabla ya Ukoloni, Afrika ilikuwa na tawala zilizokaribia 10,000 (Kingdoms/Empire/State) na tawala hizi zilijiongoza kila moja kivyake zikiwa na lugha tofauti na mila na desturi tofauti tofauti.

3. Lugha ya kiarabu inazungumzwa na watu takribani milioni 170 ikifuatiwa na lugha ya kiingereza inayozungumzwa na watu zaidi ya milioni 130, Kiswahili kikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 100, Kifaransa takribani wazungumzaji milioni milioni 115. Pia, kuna wazungumzaji wa lugha ya Xhosa wakiwa milioni 50. Kireno kinakadiriwa kuwa na wazungumzaji milioni 20 huku Kispanyola kikiwa na wazungumzaji wanaokadiriwa kuwa milioni 10. Vilevile takribani 25% ya lugha zote duniani zinazungumzwa barani Afrika huku kukiwa na lugha za makabila zaidi ya 2,000.

4. Afrika ni bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani ambao wanakadiriwa kuwa bilioni 1.1 huku zaidi ya 50% ya wakazi wake wakiwa ni vijana wenye umri chini ya miaka 25. Inakadiriwa kwamba mpaka kufikia mwaka 2050 bara la Afrika litakuwa na takribani watu bilioni 2.3. Hii ni kwa mujibu wa taarifa za idadi ya watu iliyotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 2015.

5. Takribani 40% ya wazee wakazi wa bara hili hawajui kusoma na kuandika.

6. Vita ya pili ya Kongo ndiyo vita hatari kutokea duniani baada ya Vita ya Pili ya dunia. Vita hii iligharimu uhai wa watu takribani milioni 5.4

7. Jangwa la Sahara ni kubwa kuliko yote duniani na ukubwa wake ni zaidi ya nchi ya Marekani.

8. Kuna zaidi ya wachina milioni 1 katika baraka la Afrika. Nchi ya Angola ikiwa na zaidi ya wachina 350,000.

9. Kiwango cha ukataji miti barani Afrika ni mara mbili ya kiwango chote cha ukataji miti duniani. Zaidi ya hekta milioni 4 zinakatwa miti barani hapa kila mwaka.

10. Ziwa Victoria ni ziwa kubwa kuliko yote barani Afrika huku likiwa ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani na kuwa na maji laini duniani.

11. Wanyama kama vile twiga, pundamilia, viboko, sokwe na nyumbu ni wanyama pekee wanaopatikana katika bara hili.

12. Ziwa Nyasa ambalo kwa jina jingina linaitwa Ziwa Malawi ndilo ziwa lenye aina nyingi za samaki (fish species) kuliko maziwa mengine duniani.

13. Bara hili lina zaidi ya asilimia 85 ya Tembo wote wanaopatikana duniani kote, pia, 99% ya Simba waliosalia duniani wanapatikana katika bara hili. 

14. Mto Naili ambao una urefu wa kilomita 6,650 ni mto mrefu kuliko yote duniani na unapatikana katika bara hili.

15. Mbuga ya Serengeti ambayo inapatikana nchini Tanzania ni hifadhi pekee ambayo ina kundi kubwa la wanyama duniani ikiwa na pundamilia zaidi ya 750,000. Katika hifadhi hii nyumbu zaidi ya milioni 1.2 huhama kila mwaka kutoka hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania kuelekea katika hifadhi ya Masai Mara iliyoko Kenya. Katika kundi hilo la nyumbu wanaohama kila mwaka kutafuta malisho wanyama kama pundamilia, swala na pofu huwepo katika uhamaji huo ambalo ni tukio la kipekee duniani.

16. Bara la Afrika lina zaidi ya 25% ya aina ya ndege wote wanaopatikana duniani.

17. Zaidi ya mabwawa 1,270 yamejengwa kandokando ya mito barani hapa. Mabwawa haya yana kazi kubwa ya kuzalisha umeme unaotumia ngumu za maji.

18. Bara la Afrika ni la pili kwa ukubwa na bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya bara la Asia. Afrika ina takribani watu bilioni 1.2 na hii ni kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa mwaka 2015. Hii ni sawa na 16% ya idadi yote ya watu waliopo duniani.

19.  Afrika ni bara la pili kwa kuwa na joto baada ya bara la Australia.

20. Uislamu ni dini yenye wafuasi wengi barani Afrika ikifuatiwa na dini ya Kikristo huku ikikadiriwa kwamba takribani 38% ya Wakristo wote wataishi kusini mwa jangwa la Sahara mpaka kufikia mwaka 2050.

21. Afrika ni bara lililopo katika nyuzi 0 (0°) katika mstari wa grinwichi meridiani na ikweta.

22. Nchi kubwa kuliko zote barani Afrika ni Algeria ikiwa na eneo la kilomita za mraba milioni 2.381 ikifuatiwa na DR Congo yenye eneo la kilomita za mraba 2.844 wakati nchi ndogo kuliko zote ni Shelisheli yenye eneo la kilomita za mraba 459.

23. Nigeria ndiyo nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika ikiwa na takribani watu wanaokadiriwa kufika milioni 218.5 hadi kufikia mwezi Septemba 2023. Hii ni sawa na 18% ya watu wote wanaoishi barani hapa. Pia, hii ni sawa na 2% ya watu wote wanaoishi duniani.

24. Umbali mfupi kati ya Ulaya na Afrika ni kilomita 14 sawa na maili 8.7 ukipitia mlango bahari wa Gibraltar.

24. Maporomoko ya Victoria yaliyopo kati ya mpaka wa Zambia na Zimbabwe ni maporoko ya makubwa zaidi ya maji kuliko yote duniani. Pia, ni moja kati ya maajabu saba ya dunia.

25. Kiboko ni mnyama hatari sana barani Afrika kuliko hata Simba na Chui. Anaua watu wengi kuliko Simba na Mamba wakijumlishwa kwa pamoja.

26. Takribani 90% ya wagonjwa wa Malaria duniani kote wanapatikana barani hapa. Ugonjwa huu unaua takribani watoto 30,000 kila mwaka.


27. Nchini Eswatini (Swaziland) katika kila watu 4 kati yao 1 ni muathirika wa UKIMWI.


28. Tanzania ni nchi inayoongoza kuwa na walemavu wengi wa ngozi (albino) kuliko nchi nyingine duniani. Wakati katika mataifa mengine ya kusini mwa jangwa la Sahara ikikadiriwa kuwa mtu 1 katika watu 5,000 hadi 15,000 ana ualbino, kwa Tanzania mtu 1 katika watu 1,500 ana ualbino. Hii inaifanya Tanzania kuwa na watu wengi wenye ulemavu huu wa ngozi kuliko nchi nyingine duniani kote. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. 


29. Misri ni nchi inayoongoza kwa kutembelewa na idadi kubwa ya watalii kuliko nchi nyingine barani hapa. Inapokea watalii zaidi ya milioni 10 kila mwaka 


30. Bendera ya nchi ya Msumbiji ni bendera pekee barani Afrika kuwa bendera ya taifa yenye silaha aina ya AK-47. Silaha hiyo inaashiria ulinzi wa nchi hiyo. Msumbiji ni nchi pekee yenye bendera yenye silaha ya aina hiyo duniani. Nchi nyingine zenye bendera zenye silaha duniani ni Guatemala na Haiti.


31. Bara la Afrika lilikuwa limeungana na mabara mengine miaka mingi iliyopita, lilitengana na mabara hayo katika kipindi cha kijiolojia (taaluma ya miamba na muundo wa ndani wa dunia) katika kipindi cha kijiolojia kiitwacho Mesozoic.


32. Ustaarabu (Civilization) ulianzia barani Afrika. Misri inapata sifa hii kwa kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa ustaarabu wa kifarao ambao ulianza mwaka 3300 kabla ya Kristo.


33. Shelisheli ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na pato kubwa la taifa (GNP). Pato lake linakadiriwa kuwa takribani dola za marekani milioni  15,400 huku Sudan Kusini ikiwa ndiyo yenye pato dogo zaidi ambalo linakadiriwa kuwa dola milioni 245.9.


34. Jangwa la Sahara ndilo jangwa lenye joto zaidi kuliko yote duniani. Linachukua eneo la mraba takribani milioni 9.1 ya majangwa yote duniani.

35. Kama jinsi ilivyo katika bara la Asia, barani hapa pia watu hutembea takribani maili 3.7 kila siku kutafuta maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali.


36. Madagascar ni kisiwa kikubwa kuliko vyote barani Afrika na kisiwa cha 4 kwa ukubwa duniani. Kinapatikana mashariki mwa bahari ya Hindi.


37. Tembo ni mnyama mkubwa kuliko wote duniani na anakadiriwa kuwa na uzito wa tani 6 hadi 7 anapatikana barani Afrika pekee huku Twiga akiwa ni mnyama mrefu kuliko wote dunani naye anapatikana Afrika tu. Pia, mnyama anayekimbia sana kuliko wote ambaye ni Duma anapatikana Afrika pekee huku Mamba akiwa ni mnyama mkubwa kuliko wote katika jamii ya reptilia naye anapatiakana Afrika pekee.


38. Mabaki ya mtu wa kale zaidi yalipatikana barani hapa nchini Ethiopia. Mabaki hayo yanaaminika kuwepo toka miaka laki 2 iliyopita. Charles Darwin alikua akishikilia dai hili lakini lilipingwa na waz
ungu mpaka ilipogundulika katika karne ya 20.

39. Inakadiriwa kwamba takribani watu milioni 12.5 walitekwa barani hapa na kuuzwa katika bara la Amerika kama watumwa kati ya mwaka 1525 hadi 1866.


40. Wakati nchi ya Misri inasifika kwa umaarufu wa kuwa na mapiramidi mengi duniani, Sudan ni nchi pekee yenye idadi kubwa ya mapiramidi hayo ambayo yanakadiriwa kufikia 223 hii ikiwa ni mara mbili ya mapiramidi yote yanayopatikana nchini Misri.


41. Nchini Kenya kuna kabila linalojulikana kama Kalenjin ambalo ni kabila maarufu kwa kutoa wakimbiaji wanaoongoza kwa mbio za riadha duniani.


42. Taasisi ya Elimu kongwe kuliko zote duniani ambayo bado inatumika mpaka leo ipo barani hapa. Taasisi hiyo ni Chuo Kikuu cha Al-Karaouine ambayo iko Morocco. Taasisi hii ilianza kama madrasa na ilianzishwa mwaka 859 baada ya Kristo na ilianzishwa na Fatima Al-Fihri.


43. Takribani 60% ya bara la Afrika ni kame. Sehemu hii inasababishwa na uwepo wa majangwa ya Kalahari, Sahara na Namib.


45. Bara la Afrika lina 30% ya madini yote yanayopatikana duniani.


46. Nigeria ni nchi ya 4 kwa kuzalisha mafuta duniani. Nchi 10 zinazoongoza kwa kuzalisha mafuta barani hapa ni Nigeria, Algeria, Angola, Libya, Misri, Sudan, Guinea ya Ikweta, Congo Brazzaville, Gabon na Afrika ya Kusini.


47. Bara hili lina 40% ya akiba madini ya dhahabu, 60% ya ziada ya madini ya shaba na 90% ya madini ya platini.


48. Zaidi ya 55% ya nguvu kazi ya Afrika wanajihusisha na kilimo cha mazao ya chakula ambayo pia ni sekta inayokuza uchumi barani hapa.


49. Zaidi ya 90% ya udongo wa bara hili sio rafiki kwa kilimo, ni 0.25% ya udongo ambayo ni rafiki kwa kilimo barani hapa.


50. Zaidi ya watu milioni 300 barani hapa wanategemea maji yanayotoka chini kwa matumizi ya kunywa. Maji ni tatizo katika bara hili.


51. Bara la Afrika lina naeneo zaidi ya 3,000 yanayolindwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya utalii duniani. Takribani maeneo 198 ya bahari, maeneo 129 yanayohifadhiwa na UNESCO kama maeneo ya urithi wa kujivunia na maeneo 80 chepechepe (wetland) ambayo ni ni muhimu kimataifa.


52. Afrika ni bara maskini kuliko yote duniani. Pato lake ni 3.1% ya pato lote la dunia kwa mwaka kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia.


53. Wayunani wa kale na Warumi walitumia neno Afrika wakimaanisha ukanda wa kaskazini mwa Afrika peke yake. Katika lugha ya kilatini Afrika ina maana ya ~enye hali ya jua. Wayunani wanatambua kama Aphrike wakiwa na maana kwamba ~isiyo na baridi.


54. Afrika ni bara pekee lenye kingo fupi za kanda za pwani licha ya kua bara la pili kwa ukubwa.


55. Katika bara hili wanawake wanakadiriwa kufanya kazi masaa mengi kuliko wanaume. Wanawake hufanya kazi masaa 12 hadi 14 kwa siku barani hapa.


56. Chura mkubwa zaidi kuliko wote duniani maarufu kwa jina la Goliath anapatikana nchini Guinea ya Ikweta.


57. Benin ni nchi pekee duniani ambayo inashikiria rekodi ya kuwa nchi yenye vizazi mapacha kuliko nyingine zaidi duniani. Katika kila vizazi 1,000 nchini Benin 27.9 ni vizazi vya watoto mapacha. Takwimu ya dunia ni utokeaji wa vizazi mapacha 13.6 katika vizazi 1,000.


58. Niger ni nchi inayoongoza kwa kuwa wanawake wenye uwezo mkubwa wa kuwa na vizazi. Inakadiriwa kua kila mwanamke nchini humo ana watoto 6.62. Burundi ni nchi inayofuatia baada ya Niger ikiwa na 6.04 na hii ni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016 kutoka mtandao wa Statista "The Statistical Portal"


59. Kahun ni jiji la kwanza chini ya mipango miji duniani. Jiji hili lipo nchini Misri. 


60. Afrika ni bara linaloongoza kwa vifo vya Mama na mtoto wakati wa kujifungua.


61. Takribani watu milioni 589 kusini mwa jangwa la Sahara wanaishi bila umeme. Hii ni sawa na 20% tu wakati 80% wakiishi kwa kutegemea vyanzo vingine vya nishati kama vile kuni na mkaa kwa ajaili ya kupikia.


62. Inakadiriwa kwamba mtoto 1 katika 3 kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika wana utapiamlo.


63. Bara la Afrika linakadiriwa kua na watumiaji wa mtandao (Internet) milioni 453.3 ambao ni sawa na 35.2% ya wakazi wote wa bara hili. mpaka kufikia Desemba 31, 2017 huku kukiwa na watumiaji milioni 177 wa Facebook. Mwaka 2000 bara la Afrika lilikua na watumiaji wa mtandao milioni 4.5. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa mtandao wa Internet World Stats.


64. Nchi zote 54 za bara hili ni nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Morocco iliwahi kujitoa katika umoja huu na baadaye iliamua kurejea tena. Umoja huu ulianzishwa mwaka 1963 kama OAU na baadaye ulibadilishwa kua AU mwaka 2002. Makao yake makuu yapo Addis Ababa, Ethiopia.

65. Bara la Afrika ndilo lenye nchi nyingi kuliko bara lilingine duniani.



Orodha hii imeandaliwa kwa msaada wa mtandao. Haya ni baadhi ya machache kati ya mengi unayopaswa kuyafahamu na ni jukumu lako kutafuta mengine mengi ya kufahamu. Kwa maoni na ushauri niandikie kupitia:
📧 venancegilbert@gmail.com
📞 0753400208.

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU MARAIS 10 WA AFRIKA WALIOFARIKI WAKIWA MADARAKANI

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS