Showing posts with label Michezo. Show all posts
Showing posts with label Michezo. Show all posts

UCL: FAHAMU MACHACHE MECHI YA MAN CITY VS LYON

Mechi itachezwa saa 4:00 usiku saa za Afrika Mashariki katika dimba la Man City Etihad. Mwamuzi wa mechi hii ni Muitalia Daniele Orsato. 

Hii ni mechi ya kwanza baina ya timu hizi. Mpaka sasa hakuna klabu ya Ufaransa iliyowahi kushinda ugenini dhidi ya Man City zaidi ya kuambulia suluhu 1 na kupoteza michezo 2.

Lyon imeshinda mechi 1 tu kati ya 8 ilizocheza na timu za Uingereza. Hii ilikua ni dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield Oktoba 2009.

Hii ni mara ya 8 mfululizo kwa Man City kushiriki katika ligi ya mabingwa Ulaya. Hii ni rekodi ya juu kwa sasa katika timu za Uingereza kushiriki idadi hii ya Man City ambayo mara nyingi imekua ikiondolewa katika mechi ya 5 ya michuano hii hatua ya makundi.

Katika mechi zao zote 42 walizocheza Man City hakuna mechi hata moja ambayo hawakufunga katika ligi hii.

Hii ni mara ya 15 kwa Lyon kushiriki michuano hii. Hii inaifanya kuwa timu pekee kutoka nchini Ufaransa kushiriki mara nyingi zaidi. Wamekuwa wakiondolewa katika hatua ya mtoano kuanzia msimu wa 2003/2004 hadi 2011/2012 na hawajawahi tena kufikia hatua hiyo. 

Lyon wameshinda mechi 3 tu kati ya mechi zao 13 za mwisho katika ligi hii pamoja na kusuluhu mechi 3 na kupoteza mechi 7.

Lyon ilifunga magoli 5 tu katika mechi zao 5 za mwisho katika ligi hii. Magoli 2 yalifungwa nyumbani na magoli 3 ugenini. 

Kocha wa Man City Pep Guardiola amewahi kufikisha timu zake katika hatua ya nusu fainali katika michuano 7 kati ya michuano 9 ya ligi hii aliyoshiriki kama kocha lakini hajatwaa ubingwa tangu alipotwaa mara ya mwisho 2011. Msimu huu atakua anawania kutwaa kombe hilo ili afikie rekodi ya Zinedine Zidane, Carlo Ancelotti na Bob Paisley ya kutwaa kombe hili mara 3.

Raheem Sterling ameifungia klabu yake ya Man City magoli 8 wakiwa nyumbani na kuisaidia kufunga magoli 6 katika mechi 15 alizoichezea klabu hake hiyo. 

Mshambuliaji wa Lyon Moussa Dembélé ameifungia klabu hiyo magoli 3 katika mechi 4 za mwanzo katika klabu hii katika UCL. Awali ya Lyon aliwahi kuichezea Celtic ambapo aliifungia klabu hii goli 1 katika mechi 6 kwenye michuano hii.

Man City itaingia uwanjani bila wachezaji wake Benjamin Mendy, Danillo, Claudio Bravo, Kelvin De Bruyne, Sergio Kun Arguero, Eliaqim Mangala na Philippe Sandler ambao ni majeruhi. Kwa upande wa Lyon watakosekana Amine Gouiri na Fernando Marcal. 

TAZAMA HAPA MAGOLI 10 BORA YA KOMBE LA DUNIA 2018

Michuano ya Kombe la Dunia tayari imemalizika nchini Urusi jana Julai 15, 2018 ambapo Ufaransa ilii chapa 4 - 2 Croatia. Leo nakupa nafasi ya kuangalia magoli 10 bora yaliyofungwa katika michuano hii, magoli haya ni kama ifuatavyo:
10: Cristiano Ronaldo, Portugal vs Spain
09: Toni Kroos, Germany vs Sweden
08: Lionel Messi, Argentina vs Nigeria
07: Ricardo Quaresma, Portugal vs IR Iran
06: Nacho, Spain vs Portugal
05: Aleksandar Kolarov, Serbia vs Costa Rica
04: Angel Di Maria, Argentina vs France
03: Philippe Coutinho, Brazil vs Switzerland
02. Benjamin Pavard, France vs Argentina
01. Denis Cheryshev, Russia vs Croatia.


Unaweza kutazama magoli hayo katika video hii hapa chini:


Magoli haya ni kwa hisani ya Kwesé Sports ambao walikua ni washirika rasmi wa FIFA wa kuonesha michuano hii ya Kombe la Dunia 2018.

WAFUNGAJI BORA NA WALIOCHEZA MECHI NYINGI KATIKA KOMBE LA DUNIA 1930-2014

WAFUNGAJI 5 WA MUDA WOTE

1. Miroslav Klose - Ujerumani

Klose wakati wa droo ya kombe la dunia mwaka jana 2017.
Amezaliwa Juni 9, 1978. Ana jumla ya magoli 16 katika michuano ya kombe la dunia na magoli 23 katika mechi za kufuzu, hii inafanya jumla ya magoli kuwa 29.  Aling'aa katika mechi ya awali kufuzu michuano hii ambapo Ujerumani iliichapa Abania 2-1 mwaka 2002. Amecheza mechi 43; 24 zikiwa za kombe la dunia na 19 zikiwa za kufuzu michuano hiyo. Katika mechi alizocheza na timu yake wameshinda mechi 30 wamesuluhu mechi 8 na kupoteza mechi 5. Ana kadi 1 ya njano katika michuano ya FIFA na kadi 2 za njano katika hatua ya makundi kufuzu kucheza kombe la dunia. Mwaka 2006 alishinda kiatu cha dhahabu cha Adidas na mwaka 2014 alikuwepo katika kikosi cha Ujerumani walipotwaa kombe la dunia katika fainali dhidi ya Ajentina nchina Brazil.
Klose wakati wa mechi ya robo fainali kati ya Ujerumani na Ufaransa katika dimba la Marakana Rio de Jeneiro Julai 4, 2014.


2. Ronaldo de Lima - Brazil

Ronaldo de Lima alipokabidhiwa tuzo ya Hall of Fame nchini Italia mwaka 2016
Amezaliwa Septemba 22, 1976. Amecheza mechi 45; 19 za kombe la dunia, 15 za kufuzu kombe la dunia, 5 za kombe la mabara na 6 za Olimpiki. Katika mechi hizi alifunga jumla ya magoli 34; 15 ya kombe la dunia, 10 ya kufuzu michuano hii, 4 ya kombe la mabara na 5 ya Olimpiki. Akiwa katika timu ya Brazil walishinda mechi 31, suluhu 8 na kufungwa mechi 6. Umaarufu wake ulianza kuonekana katika michuano ya Olympic mwaka 1996 iliyofanyika Atlanta dhidi ya Japan. Brazil iliifunga Japan 1-0. Amewahi kupewa kadi za njano mara 4 tu katika michuano yote. Alipokuwa Brazil walitwaa kombe la dunia mwaka 1994 na 2002. Mwaka 2002 ndiye aliyekua mchezaji bora wa michuano ya kombe la dunia FIFA. Mwaka 1997 akiwa na timu yake walishinda kombe la dunia la mabara. Ronaldo amewahi kushinda tuzo ya mpira wa dhahabu ya Adidas kama mchezaji bora. Mwaka 2002 pia alishinda kiatu cha dhahabu cha Adidas. Amewahi kushinda tuzo ya Balloon d'Or ya Ufransa mwaka 1997 na 2002.
Ronaldo enzi za Brazil.


    3. Gerd Mueller - Ujerumani

    Mueller alipokua kocha wa Bayern Munich  II
    Alizaliwa Novemba 3, 1945. Amecheza mechi 19 na timu yake ya Ujerumani; 13 zikiwa za kombe la dunia na 6 zikiwa za kufuzu michuano hiyo. Katika mechi hizo alizokuwepo walishinda mechi 16, suluhu 1 na kufungwa 2. Ana magoli 23; 14 yakiwa ya kombe la dunia la 9 yakiwa ya kufuzu michuano hiyo. Amewahi kupewa kadi za njano 2 tu katika michuano ya kombe la dunia. Mwaka 1970 alishinda tuzo mbili; kiatu cha dhahabu cha Adidas pamoja tuzo ya Ballon d'Or. Pia ni miongoni mwa waliokuwepo katika kikosi cha Ujerumani kilichotwaa kombe la dunia mwaka 1974.
    Gerd Mueller mwaka 1974 waliposhinda fainali ya kombe la dunia.

    4. Just Fontaine - Ufaransa

    Fountaine mwaka 2017
    Alizaliwa Agosti 18, 1933. Yeye alicheza 8 tu 6 zikiwa zakombe la dunia na 2 zikiwa za kufuzu michuano hiyo, katika mechi hizi alifunga magoli 16; katika hayo 13 yalikua ya kombe la dunia na 3 yalikuwa ya mechi za kufuzu michuano hiyo. Katika mechi alizocheza 6 walishinda na hawakusuluhu ila walipoteza nchi 2 tu. Alionekana katika kombe la dunia kwenye mechi ya kati ya Ufaransa na Luxembourg ambapo waliifunga nchi hiyo 8-0 na hapo nyota yake iling'aa. Hakuwahi kupewa kadi katika mechi zote alizocheza. Mwaka 1958 alishinda kiatu cha dhahabu cha Adidas. Katika kipindi chote alichocheza hawakuwahi kushinda ubingwa. Ufaransa illitwaa ubingwa baadaye mwaka 1998. Fontaine aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Morocco ambapo aliiongoza timu hiyo katika kufuzu kucheza kombe la dunia. Kama kocha timu yake ya Morocco ilicheza mechi 4. Mwaka 1982 Morocco ilicheza na Zambia na waliifunga 2-0.
    Fontaine mwaka 1958

    5. Pele (Edson Arantes do Nascimento) - Brazil

    Pele mwaka 2017
    Alizaliwa Oktoba 23, 1940. Alicheza mechi 20 ambapo 14 zilikuwa za kombe la dunia na 6 zikiwa za kufuzu kucheza kombe la dunia. Alifunga magoli 18 katika michuano hiyo 12 yakiwa ya kombe la dunia na 6 yakiwa katika hatua za kufuzu. Pele anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji pekee duniani aliyeshuhudia timu yake ya Brazil ikishinda kombe la dunia mara 3 (1958, 1962, 1970) akiwepo katika kikosi cha timu hiyo mara 3 zote. Mwaka 1958 alishinda tuzo ya Hyundai ya mchezaji mdogo wakati ule akiwa na miaka 18 tu. Mwaka 2007 Pele alishinda tuzo ya heshima ya Rais wa FIFA. Katika mechi hizo 20 alizocheza, 18 walishinda, 1 walisuluhu na 1 walifungwa.
    Pele katika enzi zake kwenye soka.


    WACHEZAJI 5 WALIOCHEZA MECHI NYINGI

    1. Luthar Matthaus - Ujerumani

    Matthaus kwa sasa yupo Sky Sport.
    Amezaliwa Machi 21, 1961. Amecheza mechi 36; 25 zikiwa za kombe la dunia, 8 zikiwa za kufuzu michuano hiyo na 3 zikiwa za kombe la mabara. Umaarufu wake ulitokana na mechi ya kombe la dunia 1982 na Chile ambapo waliichapa timu hiyo 4-1. Katika mechi zote 36 alishinda 22, alisuluhu 8 na kufungwa 6. Mwaka 1990 alishinda Ballon d'Or pamoja na kuchukua ubingwa wa dunia na timu yake ya Ujerumani. Mwaka 1991 alikuwa mchezaji bora wa mwaka. Alifunga magoli 10; 6 yakiwa ya kombe la dunia, 3 yakufuzu michuano hiyo na 1 ikiwa kombe la mabara. Amewahi kupewa kadi za njano mara 9. Pia amewahi kua kocha wa timu ya Croatia, kama kocha aliifunga Hungaria magoli 3-0.
    Lothar akibusu kombe la dunia waliposhinda mwaka 1990.

    2. Miroslav Klose - Ujerumani

    Klose akiwa na wanaye baada ya Ujerumani kutwaa kombe la dunia mwaka 2014 dhidi ya Ajentina.
    Amezaliwa Juni 9, 1978. Ana jumla ya magoli 16 katika michuano ya kombe la dunia na magoli 23 katika mechi za kufuzu, hii inafanya jumla ya magoli kuwa 29. Aling'aa katika mechi ya awali kufuzu michuano hii ambapo Ujerumani iliichapa Abania 2-1 mwaka 2002. Amecheza mechi 43; 24 zikiwa za kombe la dunia na 19 zikiwa za kufuzu michuano hiyo. Katika mechi alizocheza na timu yake wameshinda mechi 30 wamesuluhu mechi 8 na kupoteza mechi 5. Ana kadi 1 ya njano katika michuano ya FIFA na kadi 2 za njano katika hatua ya makundi kufuzu kucheza kombe la dunia. Mwaka 2006 alishinda kiatu cha dhahabu cha Adidas na mwaka 2014 alikuwepo katika kikosi cha Ujerumani walipotwaa kombe la dunia katika fainali dhidi ya Ajentina nchina Brazil.
    Klose katika kombe la dunia mwaka 2006.

    3. Paulo Maldini - Italia

    Maldin mwaka 2013.
    Alizaliwa Juni 26, 1968. Amecheza mechi 48; 23 zikiwa za kombe la dunia, 23 za kufuzu na 2 zikiwa za kombe la mabara. Alifunga magoli 3 tu katika mechi za kufuzu. Amewahi kupewa kadi za njano mara 3 tu. Katika mechi zote alizocheza 31 walishinda, 13 wakisuluhu na kupoteza 4. Mechi ya kombe la dunia mwaka 1990 wakati Italia ilipoifunga Austria 1-0 ilipelekea nyota yake kung'aa.
    Maldin mwaka 1998 katika robo fainalai ya kombe la dunia.

    4. Uwe Seeler - Ujerumani

    Seeler mwaka 2016
    Alizaliwa Novemba 5, 1936. Amecheza mechi 28; 21 zikiwa za kombe la dunia wakati 7 zikiwa za kufuzu. Amefunga magoli 23; 9 yakiwa ya kombe la dunia na 3 yakiwa ya kufuzu michuano hiyo. Katika mechi alizocheza 19 walishinda, 5 walisuluhu na 4 walifungwa. Nyota ilianza kung'aa katika kombe la dunia 1958 wakati Ujerumani ilipoifunga 3- 1 Ajentina. Hakuwahi kupewa kadi.

    5. Diego Maradona - Ajentina

    Maradona.
    Alizaliwa Oktoba 30, 1960. Alicheza mechi 35; 21 zikiwa za kombe la dunia, 8 zikiwa za kufuzu kombe la dunia na 6 zikiwa za kombe la dunia chini ya miaka 20 (U-20). Maradona alifunga magoli 17; 8 yakiwa ya kombe la dunia, 3 ya kufuzu na 6 kombe la dunia U-20. Katika mechi alizocheza 23 walishinda, 6 walisuluhu na 6 walifungwa. Nyota ya Maradona iling'aa wakati wa michuano ya vijana nchini Japan mwaka 1979 wakati Ajentina ilipoifunga 5-0 Indonesia. Mwaka 1979 alishinda mpira wa dhahabu wa Adidas, FIFA U-20 pamoja na kombe hilo mwaka huo huo. Mwaka 1986 alishinda kiatu cha dhahabu pamoja na kushinda kombe la dunia. Maradona amewahi kuwa kocha wa timu ya taifa lake ambapo mechi 13 zilichelezwa akiwa kocha. Alishinda mechi 8 na kufungwa 5. Umaarufu wake kama kocha ulitokana katika mechi ya kirafiki dhidi ya Venezuela mwaka 2010 ambapo waliichapa timu hiyo 4-0.
    Maradona akinyanyua kombe la dunia mwaka 1986 dhidi ya Ujerumani.


    MAKALA HII IMEANDALIWA KWA HISANI YA MTANDAO WA FIFA.

    TAKWIMU ZA MUDA WOTE ZA KOMBE LA DUNIA LA FIFA: TIMU, MECHI, KADI NA MAGOLI 1930-2022

    TIMU, MECHI & IDADI YA MAGOLI

    1. Mwaka 1930 jumla ya timu 13 zilicheza jumla ya mechi 18 na yalipatikana jumla ya magoli 70 hii ikiwa ni wastani wa magoli 3.9 katika kila mechi.

    2. Mwaka 1934 jumla ya timu 16 zilicheza jumla ya mechi 17 na yalipatikana jumla ya magoli 70 hii ikiwa ni wastani wa magoli 4.9 katika kila mechi.

    3. Mwaka 1938 jumla ya timu 15 zilicheza jumla ya mechi 18 na yalipatikana jumla ya magoli 84 hii ikiwa ni wastani wa magoli 4.7 katika kila mechi.

    4. Mwaka 1950 jumla ya timu 13 zilicheza jumla ya mechi 22 na yalipatikana jumla ya magoli 88 hii ikiwa ni wastani wa magoli 4.0 katika kila mechi.


    5. Mwaka 1954 jumla ya timu 16 zilicheza jumla ya mechi 26 na yalipatikana jumla ya magoli 140 hii ikiwa ni wastani wa magoli 5.4 katika kila mechi.

    6. Mwaka 1958 jumla ya timu 16 zilicheza jumla ya mechi 35 na yalipatikana jumla ya magoli 126 hii ikiwa ni wastani wa magoli 3.6 katika kila mechi.


    7. Mwaka 1962 jumla ya timu 16 zilicheza jumla ya mechi 32 na yalipatikana jumla ya magoli 89 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.8 katika kila mechi.

    8. Mwaka 1966 jumla ya timu 16 zilicheza jumla ya mechi 32 na yalipatikana jumla ya magoli 89 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.8 katika kila mechi.

    9. Mwaka 1970 jumla ya timu 16 zilicheza jumla ya mechi 32 na yalipatikana jumla ya magoli 95 hii ikiwa ni wastani wa magoli 3.0 katika kila mechi.

    10. Mwaka 1974 jumla ya timu 16 zilicheza jumla ya mechi 38 na yalipatikana jumla ya magoli 97 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.6 katika kila mechi.

    11. Mwaka 1978 jumla ya timu 16 zilicheza jumla ya mechi 38 na yalipatikana jumla ya magoli 102 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.7 katika kila mechi.

    12. Mwaka 1982 jumla ya timu 24 zilicheza jumla ya mechi 52 na yalipatikana jumla ya magoli 146 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.8 katika kila mechi.

    13. Mwaka 1986 jumla ya timu 24 zilicheza jumla ya mechi 52 na yalipatikana jumla ya magoli 132 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.5 katika kila mechi.

    14. Mwaka 1990 jumla ya timu 24 zilicheza jumla ya mechi 52 na yalipatikana jumla ya magoli 115 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.2 katika kila mechi.

    15. Mwaka 1994 jumla ya timu 24 zilicheza jumla ya mechi 52 na yalipatikana jumla ya magoli 141 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.7 katika kila mechi.


    16. Mwaka 1998 jumla ya timu 32 zilicheza jumla ya mechi 64 na yalipatikana jumla ya magoli 171 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.7 katika kila mechi.

    17. Mwaka 2002 jumla ya timu 32 zilicheza jumla ya mechi 64 na yalipatikana jumla ya magoli 161 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.5 katika kila mechi.

    18. Mwaka 2006 jumla ya timu 32 zilicheza jumla ya mechi 64 na yalipatikana jumla ya magoli 147 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.3 katika kila mechi.

    19. Mwaka 2010 jumla ya timu 32 zilicheza jumla ya mechi 64 na yalipatikana jumla ya magoli 145 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.3 katika kila mechi.

    20. Mwaka 2014 jumla ya timu 32 zilicheza jumla ya mechi 64 na yalipatikana jumla ya magoli 171 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.7 katika kila mechi.

    21. Mwaka 2018 jumla ya timu 32 zilicheza jumla ya mechi 64 na yalipatikana jumla ya magoli 169 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.6 katika kila mechi.

    22. Mwaka 2022 jumla ya timu 32 zilicheza jumla ya mechi 64 na yalipatikana jumla ya magoli 172 hii ikiwa ni wastani wa magoli 2.7 katika kila mechi.

    23. Mwaka 2026 jumla ya timu 48 zitashiriki michuano hii na kuweka rekodi ya kuwa michuano ya kwanza ya kuwa na timu 48.


    TIMU ZILIZOSHIRIKI MARA NYINGI (HADI MARA 10)

    1. Brazil inashikilia rekodi ya kucheza michuano yote 22 tangu kuanzishwa kwake (1930, 1934, 1938, 1950, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022)

    2. Ujerumani imeshiriki mara 20 kati ya michuano yote 20 tangu kuanzishwa kwake (1934, 1938, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022)

    3. Ajentina imeshiriki mara 18 (1930, 1934, 1958, 1962, 1966, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022)

    4. Italia pia inafuatia kwa kucheza michuano 18 kati ya yote 22 (1934, 1938, 1950, 1954, 1962, 1966, 1970, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014)

    5. Mexico imeshiriki mara 17 (1930, 1950, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1978, 1986, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022)

    6. Uingereza imeshiriki mara 16 (1950, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1982, 1986, 1990, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022)

    7. Ufaransa imeshiriki mara 16 (1930, 1934, 1938, 1954, 1958, 1966, 1978, 1982, 1986, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022)

    8. Hispania imeshiriki mara 16 (1934, 1950, 1962, 1966, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022)

    9. Ubeligiji imeshiriki mara 14 (1930, 1934, 1938, 1954, 1970, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2014, 2018, 2022)

    10. Urugwai imeshiriki mara 14 (1930, 1950, 1954, 1962, 1966, 1970, 1974, 1986, 1990, 2002, 2010, 2014, 2018, 2022)

    11. Swideni imeshiriki mara 11 (1934, 1938, 1950, 1958, 1970, 1974, 1978, 1990, 1994, 2002, 2006, 2018)

    12. Serbia imeshiriki mara 13 (1930, 1950, 1954, 1958, 1962, 1974, 1982, 1990, 1998, 2006, 2010, 2018, 2022)

    13. Uholanzi imeshiriki mara 11 (1934, 1938, 1974, 1978, 1990, 1994, 1998, 2006, 2010, 2014, 2022)

    14. Urusi imeshiriki mara 10 (1958, 1962, 1966, 1970, 1982, 1986, 1990, 1994, 2002, 2014)

    15. Uswisi imeshiriki mara 12 (1934, 1938, 1950, 1954, 1962, 1966, 1994, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022)

     16. Marekani imeshiriki mara 12 (1930, 1934, 1950, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022)

    17. Jamhuri ya Korea ya Kusini imeshiriki mara 11 (1954, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014, 2018, 2022)

    TIMU 10 ZILIZOCHEZA MECHI NYINGI ZAIDI

    Kikosi cha Ujerumani dhidi ya Hungaria mwaka 1954
    1. Brazil inashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi katika michuano hii. Imecheza mechi 114 ikishinda mechi 79 imesuluhu mechi 19 na kufungwa mechi 19.

    2.Ujerumani inafuatia katika orodha.  Imecheza mechi 112 ambapo imeshinda mechi 60 imesare mechi 21 na kufungwa mechi 23.
    3. Ajentina imecheza mechi 88 ikishinda mechi 47 imesuluhu mechi 17 na kufungwa mechi 24.

    4. Italia imecheza mechi 83 ikishinda mechi 45 imesuluhu mechi 21 na kufungwa mechi 17.

    5. Uingereza imecheza mechi 74 imeshinda mechi 32 imesuluhu mechi 22 na kupoteza mechi 20.
    6. Ufaransa imecheza mechi 73 ikishinda mechi 39 imesuluhu mechi 14 na kufungwa mechi 20.

    7. Hispania imecheza mechi 67 imecheza mechi 31 imesuluhu mechi 17 na kufungwa mechi 19.
    8. Mexico imecheza mechi 60 imecheza mechi 17vimesuluhu mechi 15 na kufungwa mechi 28.

    9. Urugwai imecheza mechi 59 imecheza mechi 25 imesuluhu mechi 13 na kufungwa mechi 21.
    10. Uholanzi imecheza mechi 55 imecheza mechi 30 imesuluhu mechi 14 na kufungwa mechi 11.

    TIMU 5 ZINAZOONGOZA KWA KADI ZA NJANO NA NYEKUNDU

    Nahodha wa Ajentina, Daniel Passarella akionesha kombe la dunia la Jules Rimet baadaya kuichapa Uholanzi 3-1 katika fainali ya mwaka 1978.
    1. Ajentina inashikiria rekodi ya kua timu iliyopewa kadi nyingi zaidi katika michuano hii. Ina jumla ya kadi 120; njano 111 ambazo ni nyingi sana katika michuano yote, njao ya pili 1 na nyekundu 8 katika mechi 77 (1930, 1934, 1958, 1962, 1966, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014)

    2. Ujerumani inafuatia kwa kadi 117; njano 110, njano ya pili 2 na nyekundu 5 katika mechi 106 (1934, 1938, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014)

    3. Brazili ina kadi 108; njano 97, njano ya pili 1 na nyekundu 10 ambazo zinaifanya timu hii kuwa idadi nyingi ya kadi nyekundu katika michuano hii kuliko timu nyingine. Kadi hizi zote za aina tatu zimepatikana katika mechi 104 (1930, 1934, 1938, 1950, 1954, 1958, 1962, 1966, 1970, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014)

    4. Italia ina kadi 98; njano 97, njano ya pili 1 ns nyekundu 7 katika mechi 83 (1934, 1938, 1950, 1954, 1962, 1966, 1970, 1974, 1978, 1982, 1986, 1990, 1994, 1998, 2002, 2006, 2010, 2014)

    5. Uholanzi ina kadi 97; njano 90, njano ya pili 4 na nyekundu 3 katika mechi 50 (1934, 1938, 1974, 1978, 1990, 1994, 1998, 2006, 2010, 2014)



    Makala hii imeandaliwa kwa hisani ya mtandao wa FIFA pamoja na takwimu zote.
    Kama una maoni yoyote usisite kuandika chini ya andiko hili ama niandikie kupitia barua pepe yangu; venancegilbert@gmail.com. Simu ni 0753400208.

    KARIBU TENA VENANCE BLOG KWA MENGI ZAIDI.

    HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI


    KUANZISHWA KWA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA

    Mafanikio ya michuano ya mpira wa miguu ya Olimpiki ndiyo yalikua mwanzo wa  FIFA kutamani kuwa na michuano yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo wa mpira wa miguu. Ikumbukwe kwamba kipindi hicho mpira wa miguu wa wanaume pekee ndiyo ulikuwepo. Maswali yalitumwa kwa wahisani wa FIFA ili kuona kama wanakubaliana na uanzishwaji wa michuano hiyo na kwa masharti yapi? Kamati maalumu ilichunguza maswali hayo chini ya uongozi wa  Rais wa FIFA wa kipindi hicho Jules Rimet akishirikiana na Katibu wa Shirikisho la Soka nchini Ufaransa kwa wakati ule Henri Delaunay.
    Rais wa FIFA Jules Rimet aliyeanzisha na kusimamia Kombe la Dunia la kwanza.
    Kufuatia uwepo wa muswada wa Kamati Tendaji ya FIFA, lilifanyika kongamano la FIFA Mei 28, 1928 jijini Amsterdam nchini Uholanzi likiazimia kuwepo kwa michuano ya mabingwa wa soka duniani ambayo ilipangwa na shirikisho hilo la mpira duniani na sasa nchi waandaji wa michuano hiyo zilitakiwa kuchaguliwa. Hungaria, Italia, Uholanzi, Hispania na Uswidi (Sweden) ziliwasilisha maombi  ya kuandaa michuano hiyo kwa mara ya kwanza. Kwa kipindi hicho Urugwai ilikua ni nchi iliyokua ikipigiwa upatu kuandaa michuano hiyo si tu kwa sababu nchi hiyo ilishinda medali ya dhahabu ya Olimpiki mwaka 1924 na 1928 bali pia nchi hiyo ilikuwa ikijiandaa kusherehekea maazimisho ya miaka 100 ya uhuru wa nchi hiyo mwaka 1930. Hili pia lilikua ni kivutio kikubwa sana kwa nchi ya Urugwai pamoja na kule kushinda medali ya dhahabu katika michuano ya soka ya Olimpiki.

    Mbali na hapo Urugwai ilikua tayari kugharamia gharama zote za usafiri pamoja na makazi na malazi kwa timu zote ambazo zingeshiriki michuano hiyo kwa makubaliano kwamba faida yoyote ambayo ingepatikana basi nchi hiyo ingegawana  na FIFA hata kwa kuchukua kiasi kidogo tu. Makubaliano haya yaliazimiwa na hivyo kongamano hilo la FIFA lililofanyika jijini Barcelona, Uhispania mwaka 1929 kuipa kibali Urugwai kuwa nchi ya kwanza kuandaa michuano hiyo ya kombe la dunia. Hii ilifanya nchi nyingine zilizowasilisha maombi hayo kujitoa katika kinyang'anyiro hicho cha kuwania uandaaji wa michuano hiyo.

    Kwa kipindi hiki bara la Ulaya lilikuwa katika mdororo mkubwa wa uchumi ambao ni mkubwa zaidi kuwahi kutokea duniani na hivyo hii ilipekea idadi ndogo ya ushiriki wa nchi za Ulaya. Pia, katika kipindi hiki usafiri wa ndege ulikuwa bado haujapanuka sana kwa hivyo ilizigharimu nchi za Ulaya kusafiri umbali mrefu kwa meli mpaka kufika huko Urugwai ambayo ni nchi katika bara la Amerika ya Kusini. Nchi washiriki wa michuano hii walitakiwa kutangaza wachezaji wao miezi miwili kabla ya michuano hii ili kurahisisha safari kuelekea Urugwai.

    Mashirikisho mengi ya soka barani Ulaya yalivunja ahadi hii ya ushiriki katika michuano hii na ilitumia muda sana kwa Rais wa FIFA wa kipindi kile Rimet kuzishawishi nchi za Ufaransa, Ubelgiji, Romania na Yugoslavia kukubaliana naye katika safari ya kuelekea Buenos Aires, Ajentina kwa safari ya kuelekea Urugwai. Mara ya kwanza hakukuwepo na vigezo vya ushiriki kwa hatua ya makundi. FIFA ilizialika nchi zote ambazo zilikua wanachama wake kwa kipindi kile lakini ni nchi 13 tu zilizoshiriki michuano hiyo. Nchi hizo ni Urugwai, Ajentina, Brazil, Bolivia, Chile, Mexico, Paragwai, Peru, Marekani, Ubeligiji, Ufaransa, Romania na Yugoslavia. Timu zilikua katika makundi 4; kundi A likiwa na timu 4 na makundi B-D yakiwa na timu 3 kila moja. Timu hizi zilicheza mechi 18 na jumla ya magoli 70 yalifungwa, hii ni sawa na wastani wa magoli 3.89 kwa kila mechi. Mechi zote zilichezwa katika viwanja vitatu vyote vikiwa jijini Montevideo mji mkuu wa Uruguay. Guillermo Stábile (Ajentina) ndiye alikua mfungaji bora wa michuano hii. Alifunga jumla ya magoli 8.
    Guillermo Stabile (Argentina) mfungaji bora wa Kombe la Dunia la kwanza 1930.
    Michuano hii ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza ilifunguliwa katika dimba jipya la Estadio Centenario katika jiji la Montevideo, hii ilikuwa Julai 13, 1930. Tukio hili likafungua mwanzo mpya wa soka duniani na kupelekea mafanikio makubwa katika soka  na kifedha pia. Kiukweli, wandaaji wa michuano hii hawakuridhishwa na ushiriki wa nchi 4 tu za Ulaya nilizozitaja hapo juu. Yaliyotokea huko katika michuano hiyo nchini Urugwai yalikuwa ya mafanikio makubwa sana na hii ikapelekea bingwa wa michuano hiyo ya dunia kutotwaaa taji hilo tena kwa miaka minne iliyofuata baadaye. Kwa hivyo Urugwai ndiye mshindi wa kwanza wa michuano hii ya kombe la dunia mwaka 1930 wakiwa nyumbani kwao.
    Dimba la Estadio Centenario mwaka 1930 ambako mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia ilichezwa
    Baraza la Kongresi la FIFA lilipokutana tena baadaye mwaka huo 1930 jijini Budapest, Hungaria waliishukuru sana Uruguay kwa kukubali kuandaa michuano hiyo ya kwanza ya kombe la dunia katika mazingira magumu. Sambamba na shukrani hizo, baraza hilo la FIFA lilielezea masikitiko yake kwa ushiriki ambao haukuridhisha hasa hasa kwa nchi za Ulaya.

    Umuhimu wa tukio jipya la michuano hiyo uliongezeka zaidi kufuatia kushindwa kwa kufanyika michuano ya Olimpiki mwaka 1932 ambayo ilipangwa kufanyika Los Angels, California nchini Marekani. Hii ikachochea zaidi ushiriki katika michuano ya FIFA ya kombe la dunia lililofuata.

    FIFA iliichagua Italia ambayo ilikuwa ikiwania uandaaji na Sweden kuwa waandaaji wa pili wa michuano hiyo. Safari hii kulikuwa na mechi za kufuzu tofauti na ilivyokua katika michuano ya awali kufuzu katika hatua ya makundi tofauti na michuano ya awali ambayo kulikua timu ikifungwa basi inaondolewa katika michuano hiyo. Brazil na Argentina ziliondolewa katika mechi moja tu za awali katika michuano ya mara ya kwanza. Kwa mara nyingine tena kama ilivyokua kwa timu waandaaji Uruguay kutwaa ubingwa 1930, timu waandaaji Italia walishinda wakiifunga Czechoslovakia katika muda wa nyongeza. Safari hii michuano hii ya kombe la dunia ilitangazwa redioni kwa mara ya kwanza.

    Miaka 4 iliyofuata, Rais wa FIFA, Rimet alishuhudia matarajio yake yakitimia pindi michuano hiyo ilipoandaliwa kwa mara ya tatu nchini Ufaransa ambapo ni nyumbani kwake. Kwa mara nyingine tena mambo hayakwenda sawa na matarajio baadaya kuona Austria ikijiondoa kwenye michuano hiyo na kufanya Sweden kukosa timu ya kucheza nayo raundi ya kwanza. Uruguay haikutaka tena kushiriki na pia Argentina ilijitoa katika michuano hiyo ya tatu na hii ndiyo ilikuwa sababu nchi za Cuba na Indonesia (wakati ule ikiitwa jimbo la Udachi ya Mashariki ya Hindi) zikielekea Ufaransa kushiriki michuano hiyo ya tatu. Italia ilichukua tena ubingwa kwa mara ya pili ikitetea ubingwa wake wa mwaka 1934 waliochukua wakiwa nyumbani.

    Michuano mingine ya kombe la dunia ilitakiwa kufanyika mwaka 1942 lakini kutokana na mapigano ya Vita ya Pili ya Dunia ambayo ilidumu kuanzia 1939 hadi 1945, michuano hiyo haikuweza kufanyika hivyo Italia iliendelea kuwa kuwa bingwa mtetezi kwa kipindi chote hicho hadi mwaka 1950 ilipochezwa tena michuano hiyo.

    Licha ya Vita hiyo ya Dunia, makao makuu ya FIFA yaliendelea kuwa jijini Zurich nchini Uswisi. Julai 1, 1946 baraza la Kongresi la FIFA lilikutana tena nchini Luxembourg ambapo jumla ya mashirikisho 34 ya soka yalikutana katika jubilei ya miaka 25 ya Urais wa Rimlet FIFA. Kuanzia hapo kombe la dunia liliitwa jina la Kombe la Jules Rimet (Jules Rimet Cup) kwa heshima ya Rais huyu katika michuano hii hadi mwaka 1970. Baadaye mwaka 1974 kombe liliitwa Kombe la Dunia la FIFA (FIFA World Cup) hadi sasa.
    Kombe la Dunia la Jules Rimet mwaka 1966.

    Brazil ilichaguliwa kuandaa michuano ya mwaka 1949 lakini baadye iliahirishwa kwa sababu za muda na kusogezwa hadi mwaka 1950. Uswisi ilipewa nafasi ya kuandaa michuano ya mwaka 1954. Hii ndiyo ilikuwa historia ya michuano hii ya kombe la dunia mpaka kufikia mwaka 1949.

    HISTORIA YA USHIRIKI

    Katika historia ya kombe la dunia mwaka 1930 ni nchi 13 zilishiriki bila kufuzu, zilialikwa nchi wanachama wa FIFA tu. Michuano hiyo ilifanyika kati ya Julai 13 hadi 30, 1930. Mataifa yaliyoshiriki mwaka huo ni Argentina, Ubelgiji, Chile, Bolivia, Brazil, Ufaransa, Mexico, Paraguay, Peru, Romania, Uruguay, Marekani na Yugoslavia.

    Mwaka 1934 zilishiriki timu 16 zikipitia kufuzu kwa hatua ya makundi. Michuano ilifanyika kuanzia Mei 27 hadi Juni 10, 1934. Hapa michuano hii ilihusisha mataifa kutoka kanda 4 za FIFA ambazo ni Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Shirikisho la Soka barani Amerika ya Kaskazini (CONCAF) na lile la Amerika ya Kusini (CONMEBOL) pamoja na Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA). Mataifa yaliyoshiriki ni Argentina, Austria, Ubelgiji, Brazil, Czechoslovakia kabla haijagawanyika kuunda nchi mbili za Jamhuri ya Czech na Jamhuri ya Slovakia, Misri, Ufaransa, Ujerumani, Hungaria (Hungary), Italia, Uholanzi, Romania, Uhispania (Spain), Uswidi (Sweden), Uswisi (Switzzerland) na Marekani.

    Mwaka 1938 zilifuzu timu 16 lakini Austria alijitoa baadaye na hivyo kubaki na timu 15 kutoka mashirikisho ya CONMEBOL, CONCAF, UEFA na Shirikisho la Soka barani Asia AFC. Michuano ilichezwa kuanzia Juni 4 hadi 19, 1938. Mataifa yaliyoshiriki ni Ubelgiji, Brazil, Cuba, Ufaransa, Czechoslovakia, Ujerumani, Hungaria, Italia, Norway , Poland, Romania, Uholanzi, Uswisi, Sweden na Dutch East Indies ambayo kwa sasa inafahamika kama Indonesia.

    Mwaka 1950 pia zilifuzu nchi 16 baadaye India, Uturuki na Uskochi (Scotland) zilijitoa na hivyo yakabaki mataifa 13. Hii ilichezwa kuanzia Juni 24 hadi Julai 16, 1950 ikihusisha kanda 3 za FIFA; CONCAF, CONMEBOL na UEFA. Mataifa yaliyoshiriki ni Bolivia, Brazil, Chile, Uingereza, Italia, Mexico, Paragwai, Uhispania, Sweden, Uswisi, Uruguay, Marekani na Yugoslavia.

    Mwaka 1954 zilicheza timu 16 kutoka kanda nne za FIFA duniani. Hii ilifanyiaka Juni 16 hadi Julai 4, 1954. Kanza zilishiriki ni AFC, CONCAF, CONMEBOL na UEFA. Mataifa yaliyoshiriki ni  Austria, Ubelgiji, Brazil, Czechoslovakia, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Hungaria, Italia, Korea ya Kusini, Mexico, Uskochi, Uswidi, Uturuki, Uruguay na Yugoslavia.

    Mwaka 1958 timu 16 zilishiriki lakini hakukua na timu ya bara la Asia wala Afrika. Hii ilifanyika kuanzia Juni 8 hadi 29, 1958. Kanda 3 za FIFA; CONCAF, CONMEBOL na UEFA ndizo zilishiriki mwaka huu. Mataifa washiriki ni Argentina, Austria, Brazil, Czechoslovakia, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Hungaria, Mexico, Ireland, Paraguay, Uskochi, Umoja wa Kisovieti (USSR), Uswidi, Wales na Yugoslavia.

    Mwaka 1962 zilishiriki timu 16 bila nchi za Asia na Afrika kwa mara nyingine. Mechi zilichezwa kuanzia May 30 hadi June 17, 1962 kutoka Kanda 3 za FIFA; CONCAF, CONMEBOL na UEFA. Mataifa yaliyoshiriki ni Argentina, Brazil, Bulgaria, Chile, Colombia, Czechoslovakia, Uingereza, Ujerumani, Hungaria, Italia, Mexico, Umoja wa Kisovieti (USSR), Uhispania, Uswisi, Uruguay, na Yugoslavia.

    Mwaka 1966 zilishiriki timu 16 katika kanda 4 za FIFA huku Korea Kaskazini ikishiriki kwa mara ya kwanza. Michezo ilianza Julai 11 hadi 30, 1966 safari hii ikihusisha kanda 4 za FIFA; AFC, CONCAF, CONMEBOL na UEFA. Mataifa washiriki ni Argentina, Brazil, Bulgaria, Chile, Korea ya Kaskazini, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Hungaria, Italia, Mexico, Umoja wa Kisovieti, Uhispania, Uswisi, Ureno na Uruguay.

    Mwaka 1970 zilishiriki timu 16 kutoka kanda 5 za FIFA; CAF, AFC, CONCAF, CONMEBOL na UEFA huku Morocco ikiwa ni nchi ya kwanza ya Afrika kufuzu kucheza michuano hii. Michuano ilifanyika kuanzia Mei 31 hadi Juni 21. Mataifa yaliyoshiriki ni Ubelgiji, Brazil, Bulgaria, Czechoslovakia, El Salvador, Uingereza, Ujerumani, Israel, Italia, Mexico, Morocco, Peru, Romania, Umoja wa Kisovieti, Uswidi na Uruguay.

    Mwaka 1974 timu 16 kutoka kanda 5 za FIFA; AFC, CAF, CONCAF, CONMEBOL na UEFA. Michuano ilichezwa kuanzia Juni 13 hadi Julai 7, 1974. Mataifa ya Argentina, Australia, Brazil, Bulgaria, Chile, Ujerumani ya Mashariki na Magharibi, Haiti, Italia, Uholanzi, Poland, Uskochi, Uswidi, Uruguay, Yugoslavia na Zaire (kwa sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo) yalishirki.

    Mwaka 1978 zilishiriki timu 16 kutoka kanda 5 za FIFA, AFC, CAF, CONCAF, CONMEBOL na UEFA. Michezo ilifanyika kuanzia Juni 1 hadi 25, 1978. Mataifa washiriki ni Argentina, Austria, Brazil, Ufaransa, Ujerumani, Hungaria, Iran, Italia, Mexico, Uholanzi, Uskochi Peru, Poland, Uhispania, Uswidi na Tunisia.

    Mwaka 1982 ushiriki wa timu ukaongezeka hadi timu 24 kutoka kanda 6 za FIFA ikiwa ni mara ya kwanza kwa kanda zote kushiriki. Kanda hizo ni AFC, CAF, CONCAF, CONMEBOL, UEFA na OFC; Ukanda wa Visiwa vya Bahari ya Pasifiki ama kwa jina moja la kingereza, Oceania. Michuano ilianza Juni 13 hadi Julai 11, 1982 ikihusisha mataifa ya Algeria, Argentina, Austria, Ubeligiji, Brazil, Cameroon, Chile, Czechoslovakia, El Salvador, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Honduras, Hungaria, Italia, Ireland, Peru, New Zealand, Kuwait, Poland, Uskochi, Umoja wa Kisovieti, Uhispania na Yugoslavia.

    Mwaka 1986 zilishiriki timu 24 zikicheza jumla ya mechi 52. Kanda 5 za fifa zilishiriki isipokuwa Ukanda wa Oceania, OFC.  Mei 31 hadi Juni 29, 1986 ndiyo kipindi michuano hii ilichezwa. Mataifa yaliyoshiriki ni Algeria, Argentina, Ubelgiji, Brazil, Bulgaria, Canada, Denmark, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Hungaria, Iraq, Italia, Korea ya Kusini, Mexico, Morocco, Ireland, Paraguay, Poland, Ureno, Uskochi, Umoja wa Kisovieti, Uhispania na Uruguay.

    Mwaka 1990 zilishiriki timu zaidi ya 24 kukiwa na timu zaidi ya moja kutoka Asia. Kanda 5 za FIFA zilishiriki isipokua Ocenia kuanzia Juni 8 hadi Julai 8,1990.  Mataifa yaliyoshiriki ni Argentina, Austria, Ubelgiji, Brazil, Cameroon, Colombia, Costa Rica, Czechoslovakia, Misri, Uingerea, Ujerumani, Italia, Korea ya Kusini, Uholanzi, Jamhuri ya Ireland, Romania, Uskochi, Umoja wa Kisovieti, Uhispania, Uswidi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Uruguay, Marekani na Yugoslavia.

    Mwaka 1994 zilishirki timu 24 kama kawaida kutoka kanda 5 za FIFA isipokua Ocenia. Michuano ilifanyika kuanzia Juni 17 hadi Julai 17, 1994. Mataifa washiriki ni Argentina, Ubelgiji, Bolivia, Brazil, Bulgaria, Cameroon, Colombia, Ujerumani, Ugiriki, Italia, Korea ya Kusini, Mexico, Morocco, Uholanzi, Nigeria, Norway, Jamhuri ya Ireland, Romania, Urusi, Saudi Arabia, Uhispania, Uswidi, Uswisi na Marekani.

    Mwaka 1998 timu ziliongezeka hadi 32 katika makundi 8 ya timu 4 kila kundi. Mashirikisho kutoka kanda 5 za FIFA yalishiriki isipokua ukanda wa Ocenia. Michuano hii ilifanyika kati ya Juni 10 hadi Julai 12, 1998. Mataifa 32 yaliyoshirki ni Argentina, Austria, Ubelgiji, Brazil, Bulgaria, Cameroon, Chile, Colombia, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Iran, Jamaica, Japan, Croatia, Denmark, Korea ya Kusini, Mexico, Morocco, Uholanzi, Naijeria, Norway, Paragwai, Romania, Saudi Arabia, Uskochi, Afrika ya Kusini, Uhispania, Tunisia, Marekani na Yugoslavia.

    Mwaka 2002 timu 32 huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa michuano hii kuchezwa barani Asia. Ilifanyika katika nchi mbili tofauti; Korea ya Kusini na Japan kuanzia Mei 31 hadi Juni 30, 2002 ikihusisha Kanda 5 za FIFA  isipokua Ocenia. Mataifa washiriki ni Cameroon, Nigeria, Senegal, Afrika ya kusini, Tunisia, Argentina, Brazil, Ecuador, Paraguay, Uruguay, China, Japan, Korea ya Kusini, Saudi Arabia, Costa Rica, Mexico, Marekani, Ubelgiji, Croatia, Denmark, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Poland, Ureno, Jamhuri ya Ireland, Urusi, Slovenia, Uhispania, Uswidi na Uturuki.

    Mwaka 2006 timu zilikua 32 zikiweka rekodi ya kucheza mechi 64. Michuano ilianza June 9 hadi Julai 9, 2006 ikihusisha kanda 5 za FIFA isipokua Ocenia. Mataifa washiriki ni Angola, Ivory Coast (Cote D'Ivore), Ghana, Togo, Tunisia, Australia, Iran, Japan, Korea ya Kusini, Saudi Arabia, Argentina, Brazil, Ecuador, Paraguay, Costa Rica, Mexico, Trinidad & Tobago, Marekani, Croatia, Jamhuri ya Czech, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Uholanzi, Poland, Ureno, Serbia na Montenegro, Uhispania, Uswidi, Uswisi na Ukraine.

    Mwaka 2010 zilicheza timu 32 huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa michuano hii kuchezwa barani Afrika. Huenda michuano hii iliyochezwa katika ardhi ya bara la Afrika ilikua na msisimko sana kutokana na kuchezwa kwa mara ya kwanza katika ardhi hii ya kifahari. Ilikua ni kati ya Juni 11 hadi Julai 11, 2010. Pamoja na yote binafsi huwa nazikumbuka zile nyimbo 3 ambazo zilikua na msisimko wa kipekee tangu kuanzishwa kwa michuano hii; wimbo wa kwanza ni ule wa Shakira - Waka Waka (This Time for Africa) ambao umetazamwa zaidi ya mara bilioni 3.4 katika mtandao wa YouTube, Shakira aliutendea haki huu wimbo na huenda ndiyo maana Mwenyezi Mungu akamkutanisha na Gerard Pique kabla hawajatengana 2022. Wimbo mwingine ni ule wa R. Kelly - Sign of Victory, huu nao ulikua ni 'wa moto' hadi dakika hii unaposoma hapa, mashairi yake yako 'relevant' sana. Kuna ule wa 3 aliuimba K'Naan - Wavin' Flag, nadhani unapata picha ya msisimko. Mataifa yaliyoshiriki kukipiga pale kwa Madiba ni  Algeria, Cameroon, Ivory Coast, Ghana, Nigeria, Afrika ya Kusini, New Zealand, Honduras, Mexico, Marekani, Argentina, Brazil, Chile, Paraguay, Uruguay, Australia, Japan, Korea ya Kaskazini na Kusini, Denmark, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ugiriki, Italia, Uholazi, Ureno, Serbia, Slovakia, Slovenia, Uhispania na Uswisi.

    Mwaka 2014 zilicheza timu 32 kutoka kanda 5 za FIFA isipokua Oceania. Michuano hii ilianza Juni 12 hadi Julai 13, 2014. Mataifa washiriki yalikua ni Algeria, Cameroon, Ivory Coast, Ghana, Nigeria, Ubelgiji, Bosnia & Herzegovina, Croatia, Italia, Ugiriki, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Ureno, Urusi, Uhispania, Uswisi, Australia, Iran, Japan, Korea ya Kusini, Argentina, Brazil, Chile, Colombia, Ecuador, Uruguay, Costa Rica, Honduras, Mexico na Marekani.
     
    Mwaka 2018 zilicheza timu  32 kutoka kanda 5 za FIFA isipokua Ocenia. Michuano ilianza Juni 14 hadi Julai 15, 2018. Mataifa washiriki ni Misri, Morocco, Nigeria, Senegal, Tunisia, Argentina, Australia, Ubelgiji, Brazil, Colombia, Costa Rica, Croatia, Denmark, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Iceland, Iran, Japan, Korea ya Kusini, Mexico, Panama, Peru, Poland, Ureno, Urusi, Saudia Arabia, Serbia, Uhispania, Sweden, Uswisi na Uruguay.

    Mwaka 2022 zilicheza jumla ya timu 32. Michuano hii ilifanyika nchini Qatar kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 18 mwaka 2022 ikijumuisha kanda 5 za FIFA isipokua Ocenia. Mataifa yaliyofuzu kushiriki michuano hiyo yenye msisimko wa kipekee duniani ni Qatar, Senegal, Ecuador, Uholanzi, Uingereza, Iran, Marekani, Wales, Argentina, Mexico, Poland, Saudi Arabia, Australia, Denmark, Ufaransa, Tunisia, Ujerumani, Japan, Uhispania, Costa Rica, Morocco, Ubelgiji, Canada, Croatia, Brazil, Cameroon, Serbia, Uswisi, Ghana, Ureno, Korea ya Kusini na Urugwai.

    Mwaka 2026 kwa mara ya kwanza dunia itashuhudia michuano hii ikichezwa katika majiji 16 ya mataifa matatu ya bara la Amerika ya Kaskazini; Marekani, Canada na Mexico. Ni kwa mara ya kwanza pia michuano hii itajumuisha jumla ya timu 48 kutoka katika kanda sita za FIFA. Marekani itahusika katika mechi 60 ikiwa ni pamoja na mechi zote za robo fainali hadi fainali. Canada na Mexico zitachezwa mechi 10 kila taifa na kufanya jumla ya mechi kuwa 80. Katika michuano hii ukanda wa Afrika (CAF) utakuwa na uhakika kupeleka timu 9 na moja italazimika kucheza play-off na timu kutoka ukanda mwingine wa FIFA. Ocenia (OFC) pia ina uhakika wa timu 1 na nyingine kama itafuzu kwenye play-off.

    WAANDAAJI (1930-2026)

    1930 Uruguay.
    1934 Italia.
    1938 Ufaransa.
    1950 Brazil.
    1954 Uswisi.
    1958 Sweden.
    1962 Chile.
    1966 Uingereza.
    1970 Mexico.
    1974 Ujerumani.
    1978 Argentina.
    1982 Hispania.
    1986 Mexico.
    1990 Italia.
    1994 Marekani.
    1998 Ufaransa.
    2002 Japan/Korea ya Kusini.
    2006 Ujerumani.
    2010 Afrika Kusini.
    2014 Brazil.
    2018 Urusi.
    2022 Qatar.
    2026 Canada/Marekani/Mexico.

    WASHINDI WA KOMBE LA DUNIA (1930-2022)

    1930 Uruguay ilitwaa ubingwa kwenye fainali dhidi ya Argentina.

    1934 Italia ilitwaa ubingwa kwenye fainali dhidi ya Czechoslovakia.

    1938 Italia ilitwaa ubingwa mara ya pili kwenye fainali dhidi ya Hungaria.

    1950 Uruguay ilitwaa ubingwa kwenye fainali dhidi ya Brazil.

    1954 Ujerumani ilitwaa ubingwa kwenye fainali dhidi ya Hungaria.

    1958 Brazil ilitwaa ubingwa kwenye fainali dhidi ya Sweden.

    1962 Brazil ilitwaa ubingwa mara ya pili kwenye fainali dhidi ya Czechoslovakia.

    1966 Uingereza ilitwaa ubingwa kwenye fainali dhidi ya Ujerumani.

    1970 Brazil ilitwaa ubingwa mara ya tatu kwenye fainali dhidi ya Italia.

    1974 Ujerumani ilitwaa ubingwa mara ya pili kwenye fainali dhidi ya Uholanzi.

    1978 Argentina ilitwaa ubingwa kwenye fainali dhidi ya Uholanzi.

    1982 Italia ilitwaa ubingwa mara ya tatu kwenye fainali dhidi ya Ujerumani.

    1986 Argentina ilitwaa ubingwa mara ya pili kwenye fainali dhidi ya Ujerumani.

    1990 Ujerumani ilitwaa ubingwa mara ya tatu kwenye fainali dhidi ya Argentina.

    1994 Brazil ilitwaa ubingwa mara ya nne kwenye fainali dhidi ya Italia.

    1998 Ufaransa ilitwaa ubingwa kwenye fainali dhidi ya Brazil.

    2002 Brazil ilitwaa ubingwa mara ya tano kwenye fainali dhidi ya Ujerumani.

    2006 Italia ilitwaa ubingwa mara ya nne kwenye fainali dhidi ya Ufaransa.

    2010 Hispania ilitwaa ubingwa kwenye fainali dhidi ya Uholanzi.
     
    2014 Ujerumani ilitwaa ubingwa mara ya nne kwenye fainali dhidi ya Argentina.
     
    2018 Ufaransa ilitwaa ubingwa mara ya pili kwenye fainali dhidi ya Croatia.

    2022 Argentina ilitwaa ubingwa mara ya tatu kwenye fainali dhidi ya Ufaransa. 

    REKODI ZA MICHUANO  (1930-2022)

    • Tangu 1930 imechezwa michuano 22 ya Kombe la Dunia (1930-2022).
    • Hadi 2022 ni mataifa 80 tu ambayo yamecheza michuano hii.
    • Kwa sasa Argentina ndiye bingwa mtetezi (2022). Hii ni mara ya tatu kwa taifa hili kutwaa ubingwa huu wa dunia (1978, 1986 na 2022).
    • Ni nchi 8 tu duniani zimeshawahi kutwaa ubingwa wa michuano hii (Brazil, Ujerumani, Italia, Argentina, Ufaransa, Uruguay, Uingereza na Hispania).
    • Ni timu 13 tu katika michuano yote 22 ambazo zimefika hatua ya fainali (Brazil, Ujerumani, Italia, Argentina, Ufaransa, Uruguay, Uingereza, Hispania, Uholanzi, Hungaria, Czechoslovakia , Sweden na Croatia).
    • Ni timu za Ulaya na Amerika ya Kusini pekee zilizotwaa ubingwa wa kombe la dunia mpaka sasa.
    • Brazil ndiyo timu pekee ambayo imeshiriki michuano yote 22 tangu 1930 ikifuatiwa na Ujerumani mara 20. Italia na Argentina mara 18 na Mexico mara 17.
    • Brazil ndiyo timu iliyotwaa ubingwa mara nyingi kuliko nchi nyingine. Imetwaa ubingwa mara tano (1958, 1962, 1970, 1994 na 2002) wakifungwa katika fainali mbili (1950 na 1998).
    • Timu 5 zimecheza fainali bila Ubingwa (Uholanzi, Czechoslovakia, Hungaria, Sweden na Croatia).
    • Ujerumani na Italia zimetwaa ubingwa mara nne. Ujerumani ndiyo nchi iliyoshindwa kutwaa ubingwa mara nyingi katika fainali za kombe la dunia, imefungwa mara nne katika fainali (1966, 1982, 1986 na 2002). Italia imepoteza mara mbili tu (1970 na 1994).
    • Uholanzi ndiyo nchi pekee iliyofika finali na kucheza na timu zaidi ya mbili na kushindwa kutwaa ubingwa. Wamepoteza katika finali tatu (1974, 1978 na 2010).
    • Marekani na Uturuki ndiyo nchi pekee nje ya mabara ya Ulaya na Amerika ya Kusini kumaliza katika nafasi ya 3.
    • Ujerumani ndiyo timu inayoongoza kwa kucheza finali nyingi za kombe la dunia. Imecheza mara nane (1954, 1966, 1974, 1982, 1986, 1990, 2002 na 2014) Brazil inaifuatia Ujerumani kwa kucheza fainali mara 7, Italia na Argentina mara 6.
    • Ni nchi 2 tu ambazo zimetwaa ubingwa mara mbili mfululizo. Italia (1934 na 1938) na Brazil (1958 na 1962).
    • Mabingwa watetezi walioondolewa kwenye hatua za makundi michuano iliyofuata; Italia (1950), Brazil (1966), Ufaransa (2002), Italia (2010), Hispania (2014) na Ujerumani (2018).
    • Lionel Messi ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi katika michuano hii. Amecheza jumla ya mechi 26 katika michuano 5 (2006, 2010, 2014, 2018 na 2022).
    • Pele ni mchezaji pekee aliyetwaa ubingwa na timu yake ya Brazil mara tatu (1958, 1962 na 1970). Rekodi hii bado haijavunjwa. 
    • Norman Whiteside (Ireland Kaskazini) ndiye mchezaji mdogo kuwahi kucheza katika michuano hii akiwa na miaka 17 na siku 41 (Ireland Kaskazini vs.  Yugoslavia, Juni 17, 1982).
    • Pele anashikiria rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kucheza katika fainali ya kombe la dunia akiwa na miaka 17 na siku 249, fainali hii ilikuwa ni Brazil vs. Sweden Juni 29, 1958.
    • Essam El-Hadary (Misri) ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa kucheza katika michuano hii akiwa na miaka 45  na siku 161 (Misri vs. Saudi Arabia, Juni 25, 2018).
    • Dino Zoff (Ujerumani) ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa aliyecheza katika fainali za kombe la dunia akiwa na miaka 40 na siku 133 (Italia vs. Ujerumani Magharibi Julai 11, 1982).
    • Kylian Mbape ndiye aliyefunga magoli mengi katika hatua ya fainali akifunga jumla ya magoli 4 dhidi ya Croatia (2018) na Argentina (2022).
    • Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji pekee aliyefunga magoli katika michuano mingi, akifunga magoli 8 katika michuano mitano (2006, 2010, 2014, 2018 na 2022).
    • Lucien Laurent (Ufaransa) ndiye mfungaji wa bao la kwanza kabisa katika historia ya kombe la dunia (Ufaransa vs. Mexico, Julai 13, 1930).
    • Angelo Schiavio (Italia) ndiye mfungaji wa bao la 100 na michuano hii ya Kombe la Dunia (Italia vs. Marekani, Mei 27, 1934).
    • Miroslav Klose ndiye mfungaji mwenye magoli mengi katika michuano hii akifunga jumla ya magoli 16 katika mechi 24 kwenye michuano minne (2002, 2006, 2010 na 2014).
    • Asamoah Gyan ndiye mchezaji pekee barani Afrika kufunga magoli mengi katika michuano hii akifunga jumla ya magoli 6. Hii ni sawa na kusema Gyan ndiye mchezaji pekee nje ya bara la Ulaya na Amerika ya Kusini kufikia idadi hiyo ya magoli.
    • Mwaka 2022 yalifungwa jumla ya magoli 172 ikiwa ndiyo michuano yenye magoli mengi zaidi katika michuano yote 22.
    • Rekodi ya mechi iliyokuwa na watazamaji wengi uwanjani ilichezwa Julai 16, 1950 kati ya Uruguay vs Brazil katika uwanja wa Maracanã jijini Rio de Janeiro, Brazil. Mechi hii ilihudhuriwa na watu 173,850.
    • Vittorio Pozzo ndiye kocha mwenye mafanikio ya kubeba ubingwa wa kombe la dunia mara mbili kama kocha akiwa na timu ya Italia akishinda mara 2 mfululizo (1934 na 1938).


    MAKALA HII HUHARIRIWA MARA KWA MARA KUENDANA NA WAKATI TANGU MEI 2018. IMEANDALIWA NA KUANDIKWA NA VENANCE GILBERT KWA HISANI YA MTANDAO WA FIFA NA MITANDAO MINGINE.

    KWA UANDISHI WA MAKALA MBALIMBALI ZA SOKA, ELIMU, BURUDANI, SIASA N.K WASILIANA NAMI KWA BARUA PEPE venancegilbert@gmail.com ama namba ya simu 0753400208.