LEO AGOSTI 6 KATIKA HISTORIA
Leo ni Agosti 6, 2018 ikiwa ni siku ya 218 katika mwaka 2018. Zimesalia siku 147 katika mwaka huu. Nakukaribisha tena katika muendelezo ya Leo Katika Historia. Kwa leo nimekuletea matukio kadhaa yaliyopata kutokea katika historia ya dunia, na tuanze kuyahesabu matukio hayo: MATUKIO 1787 - Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Marekani ilianza kujadiliwa huko Philadelphia. 1890 - Hukumu ya kuuawa kwa kiti cha umeme ilianza kutekelezwa katika gereza la Auburn huko New York, Marekani ambapo William Kemmier alihukumiwa kifo katika kiti cha umeme kwa kumuua mpenzi wake Matilda Ziegler kwa shoka. Adhabu hii ya kifo ilipendekezwa mwaka 1881 na Dk. Albert Southwick baada kushuhudia mlevi akiuawa kwa shoti ya umeme. Katika kutekeleza adhabu hii zilitumika volti 700 za umeme na katika sekunde 17 umeme ulifeli kabla Kemmier hajafariki na baadaye waliongeza umeme hadi volti 1,030 ndani ya dakika 2 na ndipo Kemmier alifariki. Kiti cha Umeme kilichotumika kutekeleza adhabu ya kifo kwa Kemmier. ...