Posts

Showing posts from December, 2013

KILA LA HERI KUUMALIZA MWAKA 2013 NA KUUANZA MWAKA 2014

Image
Venance Blog inawatakieni kila la heri katika kuumaliza mwaka huu 2013 na kuuanza mwaka mpya 2014. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetulinda toka Januari 1 mpaka leo hii Desemba 31 muda na wakati kama huu, tumuombe pia atualie uzima tuweze kuufikia mwaka mpya 2014 tukiwa wazima wa afya ili pia tuendelee na ujenzi wa taifa letu Tanzania. Kwa hayo machache, Venance Blog inakutakia kila la heri na maandalizi mema ya kuupokea mwaka mpya, tusherehekee kwa amani na utulivu bila kuvuja sheria zilizowekwa... KARIBU 2014 KWA HERI 2013!!!

RAIS KIKWETE AKABIDHIWA RASIMU YA KATIBA MPYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amekabidhiwa rasimu ya pili ya katiba mpya na tume ya katiba inayoongozwa na mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba.Rais Kikwete amesema kuwa kazi iliyofanyika katika mchakato huo imewezesha makundi mbalimbali katika jamii kuchangia mawazo yao kupitia tume aliyoiunda ili kupata mawazo ya watanzania kuhusiana na katiba wanayoitaka.Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amekabidhiwa pia rasmu hiyo na kueleza kuwa kuwa wajumbe watakaoteuliwa katika bunge la katiba wanapswa kufanya kazi kwa bidii kama ilivyokuwa kwa kamati hii iliyomaliza kazi yake.Jaji mstaafu Warioba amesema rasimu hii wanayoiwasilisha ni ndefu kuliko ile ya awali iliyokuwa na ibara 240 wakati hii ina ibara 271 ikiwa ni matokeo ya tume kuzingatia maoni ya mabaraza ya katiba yaliyotoa maoni mengine mapyaAmeyataja baadhi ya mambo ambayo tume imebaini kuwa yalijadiliwa kwa hisia kali katika rasmu hiyo na ile ya awali kuwa ni suala la muungano hasa

JESHI LA DRC LAFANIKIWA KUZIMA SHAMBULIO LA KIGAIDI

Image
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limesema kuwa limefanikiwa kuzima shambulio lililolenga uwanja wa ndege na kituo cha taifa cha Radio na Televisheni linalodaiwa kutekelezwa kundi lisilofahamika la kigaidi.Waziri wa habari nchini humo Lambeart Mende amesema kwa sasa hali imedhibitiwa ambapo wamefanikiwa kuwaua watu 40 miongoni mwa waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo.Watu hao waliokuwa na silaha 16 kati yao wameuawa katika mapambano na polisi uwanja wa ndege,16 wengine katika eneo la jeshi na nane wao waliuawa katika ofisi za Radio ya Taifa.Amesema kuwa kulikuwa na matukio mengine mawili ya mashambulizi katika maeneo ya uwanja wa ndege na kambi ya jeshi.Kwa mjibu wa waziri Mende watu hao waliokuwa wakiendesha mashambulizi hayo katika televisheni ya taifa na makao makuu ya radio ya taifa walikuwa na silaha zikiwemo bunduki,visu lakini walidhibitiwa kabla ya kusababisha madhara .Mashambulizi haya yametokea wakati Rais Joseph Kabila akiwa ziarani katika jimbo la Katanga nchin

MTU MMOJA AUAWA KATIKA MAPIGANO CAIRO

Image
Mtu mmoja ameuawa katika mapigano kati ya wanafunzi wanaokiunga mkono Chama cha Muslim Brotherhood na wakazi jijini Cairo nchini Misri, maafisa wameeleza.Maafisa mjini humo wamesema kuwa mwanafunzi mmoja alipoteza maisha baada ya pande hizo mbili kushambuliana kwa risasi katika mji wa Nasr.Tukio hilo limetokea siku moja baada ya Serikali ya Misri kukitaja chama cha Muslim Brotherhood kuwa kundi la kigaidi.Katika tukio jingine, watu watano wamejeruhiwa kwa bomu lililokuwa karibu na basi moja mjini Nasr, bomu hilo lilitegwa na kulipuka wakati basi hilo lilipokuwa likipita karibu na eneo lilipotegwa bomu.Hakuna kundi lolote lililokiri kuhusika na tukio hilo.Siku ya alhamisi, takriban wafuasi 16 wa chama cha Muslim Brotherhood walikamatwa wakishutumiwa kujihusisha na kundi hilo linalodaiwa kuwa la kigaidi.Miongoni mwa waliokamatwa ni Mtoto wa Naibu Kiongozi wa Chama hicho.Shirika la Habari la Misri, Mena limesema Watu hao walikamatwa na kushutumiwa kuchochea machafuko na mapigano dhidi y

WANAJESHI WAUAWA KWA BOMU SOMALIA

Image
Milipuko imekuwa ikijitokeza mara kwa mara nchini Somalia. Takriban wanajeshi watano na afisa wa jeshi wameuawa katika mlipuko wa bomu mjini Mogadishu nchini Somalia mashuhuda wameeleza. Mlipuko huo unaelezwa kutokea wakati wanajeshi hao wakipata malipo yao nje kidogo ya mji huo. Sababu ya mlipuko huo haijafahamika majeruhi kadhaa wamepelekwa hospitalini kwa matibabu. Wanamgambo wa kiislamu, Al Shabab walitimuliwa kwa nguvu mjini Mogadishu mwaka 2011 lakini wameendelea kufanya mashambulizi nchini humo. Kundi hilo lenye uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda linadhibiti maeneo kadhaa katikati ya Somalia.

96% WAHITIMU DARASA LA SABA KUJIUNGA SEKONDARI

ASILIMIA 96.15 ya wanafunzi wa darasa la saba waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu na kufaulu, ndio waliochaguliwa kujiunga na sekondari za serikali.Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI, Jumanne Sagini aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kwamba jumla ya wanafunzi 411,127 kati ya 427,609 waliofaulu mtihani huo ndio watakaoanza kidato cha kwanza mwakani.Alisema wasichana ni 201,021 na wavulana 210,106 na kwamba waliochaguliwa wameongezeka kwa asilimia 31.37 ikilinganishwa na asilimia 64.78 waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka huu.Kwa mujibu wa matokeo ya mtihani mwaka huu, alama ya juu kabisa kwa wavulana ilikuwa 244 huku ya wasichana ikiwa ni 241 kati ya alama 250 ambapo mwaka jana alama ya juu ilikuwa 237.“Matokeo yanaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 427,609 (wavulana 218,093 na wasichana 209.516) walifaulu kwa kupata alama A-C kati ya 844,938 waliofanya mtihani ikiwa ni sawa na asilimia 50.61 … takwimu zinaonesha ongezeko la asilimia 19 la ufau

JIJI LA MBEYA KUKUSANYA BILIONI 64.8 MWAKA WA FEDHA UJAO

JUMLA ya shilingi bilioni 64.8 zinatarajiwa kukusanywa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika mwaka wa fedha 2014/2015.Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Musa Zungiza alipotoa taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka huo wa fedha kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kujadili bajeti hiyo.Zungiza alisema kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 11.3 sawa na asilimia 17.5 zitakusanywa kutoka katika vyanzo vya ndani vya halmashauri wakati michango ya nguvu ya wananchi itakuwa bilioni moja sawa na asilimia 1.5.Kutoka serikali kuu, halmashauri inatararajia kupokea Sh bilioni 37.7 sawa na asilimia 58 kwa ajili ya mishahara ya watumishi, Sh bilioni 3.4 sawa na asilimia tano kwa ajili ya matumizi mengineyo na Sh bilioni 11.4 sawa na asilimia 18 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Zungiza alisema pia halmashauri inatarajia kutumia jumla ya Sh bilioni 64.8 katika mwaka huo wa fedha kwa ajili ya mishahara ya watumishi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo na matumizi ya

AFUNGWA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO WA KAKA YAKE

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilayani Nzega, Tabora, imemhukumu Juma Lufunga (26) kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa kaka yake na kumsababishia maumivu makali.Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Joseph Ngomelo alisema Lufunga (26) ametiwa hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka sita na kumsababishia maumivu makali na hivyo kustahili kifungo cha maisha gerezani ili adhabu yake iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za aina hiyo.Alisema vitendo vya ulawiti wa watoto wadogo, vimekuwa vikiongezeka kila kukicha na kusababaisha jamii ishindwe kufanya kazi zingine za maendeleo kwa hofu juu ya watoto wao kwa kuwa watu wazima wamekuwa ni tatizo hasa wanaume.Kabla ya hukumu hiyo, mtuhumiwa huyo Juma Lufunga akijitetea mbele ya mahakama hiyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na yeye kuwa ni mwathirika wa virusi vya Ukimwi, hata hivyo mtuhumiwa huyo alipoombwa vyeti vya uthibitisho hakuweza kuwasilisha mahakamani.Awali, Mwendesha mashitaka

APIGWA HADI KUFA KATIKA FUMANIZI

MTU mmoja m kulima na mkazi wa eneo la Kumsenga wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, aliyefahamika kwa jina la Yusuph Pascal, ameuawa kwa kupigwa na vitu mbalimbali katika tukio linalodaiwa kuwa ni fumanizi la mapenzi.Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Fraisser Kashai alisema mjini hapa kwamba mtuhumiwa huyo wa fumanizi, aliuawa mwanzoni mwa wiki hii.Alisema baada ya kifo chake, mume wa mwanamke aliyefumaniwa kwa kushirikiana na watu wengine, waliuchukua mwili wa marehemu na kuutupa eneo la Mnarani mjini Kasulu.Kufuatia tukio hilo, kamanda huyo alisema watu watano wanashikiliwa na jeshi hilo, wakituhumiwa kuhusika na tukio hilo la mauaji ya mkulima huyo.Kashai aliwataja watu waliokamatwa kwenye tukio hilo kuwa ni watu watatu wa familia moja, ambao ni Augustino Adrian, Laurent Adrian na Peter Adrian, ambao ni wamiliki wa nyumba yalipotokea mauaji.Aliwataja wengine waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo kuwa Mihosho Hamza, ambaye ni mume wa mwanamke aliyefumaniwa akiwa ni mpangaji katika nyumba yal

JELA MIAKA 30 KWA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA

Image
Wakazi wawili wa vijiji vya Nyabisaga Kata ya Pemba wilayani Tarime mkoani Mara, Mhoni Chacha Ng’wena (25) na Isack Magawi Meng’anyi (30), wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha. Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Wilaya ya Tarime. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Tarime, Adrian Kilimi alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka, ukiongozwa na Inspekta Usu, George Lutonja kwamba washitakiwa walitenda kosa la unyang’anyi wa silaha.Alisema Mahakama imeridhika na ushahidi, ulioambatana na vielelezo vya mlalamikaji, vilivyokamatwa kwa watuhumiwa hao, vikiwemo baiskeli, simu ya mkononi, viatu na tochi.  Awali, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Inspekta Usu Lutonja alidai kuwa washitakiwa hao pamoja Januari 3, mwaka huu saa 12 alfajiri, wakiwa na silaha za jadi za mapanga na marungu walivamia na kuingia ndani ya nyumba ya Selestin Omahe, mkazi wa Sirari na kumshambulia n

WATU SABA WAFARIKI PWANI NA NJOMBE KATIKA MATUKIO TOFAUTI

Image
WATU saba wamekufa katika mikoa ya Njombe na Pwani katika ajali za gari na mtoto kutumbukia kwenye ndoo.Kutoka Njombe, mtoto wa mwaka mmoja, Pendo Mbena amekufa baada ya kutumbukia kwenye ndoo ya maji.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani alisema mtoto huyo alikufa juzi saa tatu asubuhi katika Kijiji cha Igoma wilayani Njombe.Akielezea tukio hilo, Ngonyani alisema Upendo alikufa baada ya kutumbukia kwenye ndoo iliyokuwa jikoni baada ya kuachwa na mama yake, Agness Mbena (28) aliyekwenda kuchota maji.Katika tukio lingine, Ngonyani alisema mtoto wa miaka mitatu, Kelvin Kyando, mkazi wa Mtalawe amekufa baada ya kugongwa na pikipiki.Alisema ajali hiyo ilitokea mtaa wa Posta, Njombe Mjini baada ya pikipiki yenye namba za usajili T 112 CLX aina ya Fekon, mali ya Kelvin Chaula (21) kumgonga mtembea kwa miguu, mwanafunzi, Anthon Bruno (12) aliyekuwa amembeba Kelvin.“Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa pikipiki. Chanzo cha ajali ni uzembe wa mwendesha pikipiki kwani hakuweza

WALAJI WA NGURUWE KUPATA KIFAFA

Image
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa. Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA, umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa. Akizungumza na gazeti la Habari Leo hivi karibuni, Mhadhiri na Mtafiti wa Idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya, zimebaini nguruwe wengi wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo. Kwa mujibu wa Profesa Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia Mradi wa Utafiti wa Kuboresha Ufugaji wa nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya nguruwe kwa ajili ya vipimo. “Majibu ya sampuli ambazo wataalamu w

CHRISTMAS PHOTOS

Image
MERRY CRISTMAS HAPPY CRISTMAS GREAT CHRISTMAS ENJCHRISTMAS FANTASTIC CHRISTMAS NICE CHRISTMAS JUST FOR YOU JUST FOR YUOU MERRY CHRISTMAS & HAPPY CHRISTMAS

QUOTES OF THE DAY/QUOTES FOR CHRISTMAS 2013

Image
1. He who has not Christmas in his heart will never find it under a tree. -Roy L. Smith  2. Christmas is not a time nor a season, but a state of mind. To cherish peace and goodwill, to be plenteous in mercy, is to have the real spirit of Christmas. -Calvin Coolidge  3. Christmas, my child, is love in action. Every time we love, every time we give, it's Christmas. -Dale Evans  4. Christmas waves a magic wand over this world, and behold, everything is softer and more beautiful. -Norman Vicent Peale  5. We consider Christmas as the encounter, the great encounter, the historical encounter, the decisive encounter, between God and mankind. He who has faith knows this truly; let him rejoice. -Pope Paul VI  6. Christmas... is not an external event at all, but a piece of one's home that one carries in one's heart. -Freya Stark  7. It's true, Christmas can feel like a lot of work, particularly for mothers. But when you look back on all the Christmases i

SALAAMU ZA SIKUKUU YA KRISMASI

Image
Venance Blog inawatakieni HERI YA KRISMAS. Mpendwa msomaji wa blog hii, leo Wakristu duniani kote wanaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwokozi wao, Yesu Kristu aliyezaliwa takribani miaka 2000 iliyopita. Venance Blog inakukumbusha katika sikukuu hii kama ni mnywaji usilewe sana na pia ukumbuke ugonjwa hatari wa UKIMWI hasa siku kama hii ya leo kuwa makini sana, pia tuwasaidie watoto wetu au wadogo zetu kuvuka mabarabara salama huko mitaani kwetu. Krismasi ni siku ya furaha na kuoneshana upendo, hivyo tupendane wote kwa pamoja. HERI YA KRISMAS NA KRISMAS YENYE FURAHA SHEREHEKEA KWA AMANI NA UPENDO!!!

CHRISTMAS GREETINGS

Image
  Venance Blog is grateful to wish you a MERRY CHRISTMAS. Venance Blog wishes you a nice celebration, one thing to remember is to keep our national peace and avoiding other evils, if you drink don't take too much remember there is HIV/AIDS so be careful help the children to cross the road along the streets because its a day for happiness and loving each other.. MERRY CHRISTMAS & HAPPY CHRISTMAS!!!

MAANDALIZI MEMA YA SIKUKUU YA KRISMAS

Image
Kwanza namshukuru Mungu toka tukiwa wadogo mpaka sasa anaendelea kutulinda. Uongozi mzima wa Venance Blog tunawatakieni maandalizi mema ya Krismas hapo kesho, wale wa kanisani tukafurahi kwani bwana atazaliwa. Msali salama katika misa za mkesha kubwa zaidi kudumisha amani na usalama kuanzia leo mpaka sikuku itakapoisha. MAANDALIZI MEMA YA KRISMAS!!!

(NEW VIDEO) SHILOLE - NAKOMAA NA JIJI

Image