AFUNGWA MAISHA KWA KUMLAWITI MTOTO WA KAKA YAKE

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wilayani Nzega, Tabora, imemhukumu Juma Lufunga (26) kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa kaka yake na kumsababishia maumivu makali.Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Joseph Ngomelo alisema Lufunga (26) ametiwa hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka sita na kumsababishia maumivu makali na hivyo kustahili kifungo cha maisha gerezani ili adhabu yake iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za aina hiyo.Alisema vitendo vya ulawiti wa watoto wadogo, vimekuwa vikiongezeka kila kukicha na kusababaisha jamii ishindwe kufanya kazi zingine za maendeleo kwa hofu juu ya watoto wao kwa kuwa watu wazima wamekuwa ni tatizo hasa wanaume.Kabla ya hukumu hiyo, mtuhumiwa huyo Juma Lufunga akijitetea mbele ya mahakama hiyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na yeye kuwa ni mwathirika wa virusi vya Ukimwi, hata hivyo mtuhumiwa huyo alipoombwa vyeti vya uthibitisho hakuweza kuwasilisha mahakamani.Awali, Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi, Melito Ukongoji alidai mahakamani hapo kuwa Desemba 24 mwaka 2012 majira ya saa 12 jioni katika kijiji cha Mwanihara, Lufunga alimlawiti mtoto wa kaka yake na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.Melito alidai taarifa ya daktari ilithibitisha unyama aliofanyiwa mtoto huyo ambaye jina lake linahifadhiwa.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017