Posts

Showing posts from August, 2018

WAFAHAMU MATAJIRI 10 WA TANZANIA MWAKA 2018

Image
10. YUSUF MANJI Manji ni mmiliki wa mali zisizohamishika hasa majengo kwa ajili ya makazi ya watu na biashara. Pia ni muanzilishi wa kampuni ya Quality Group of Companies. Anajihusisha pia na vipuli vya magari. Haya yamemfanya kua miongoni mwa matajiri wa juu zaidi nchini. 9. FIDA RASHID Fida ni muanzilishi wa kampuni ya Africarrier Group. Hii ni kampuni inayohusika na magari yaliyotumika. Pia kampuni hii inahusika na usambazaji wa magali ya kampuni ya Eicher na Golden Dragon hapa nchini. Hii imefanya kampuni yake kufanya vyema sana katika idara hii. Fida pia ni mmiliki wa mali zisizohamishika pamoja na majengo kama Zahra Tower na Raha Tower. Amekua mjasiriamali anayetengeneza zaidi mazingira mazuri ya biashara zake kama wafanyavyo wengine. 8. GHALIB SAID MOHAMMED Ghalib Mohammed alikua akifanya biashara ya korosho hapo awali na biashara nyingine akishirikiana na baba yake. Baadaye Ghalib Said aliamua kuanzisha kampuni yake na kuiita GSM Group ambayo inajihusisha

CELEBRITY: SHANIA TWAIN ANATIMIZA MIAKA 53 LEO AGOSTI 28, 2018

Image
KUZALIWA  Celebrity wetu wa leo ni Shania Twain. Jina lake la kuzaliwa ni  Eilleen Regina Edwards lakini umaarufu wake umetokana na jina lilizoeleka la Shania Twain. Wengine wanamuita Malkia wa Muziki wa Country.  Alizaliwa mnamo Agosti 28, 1965 leo anatimiza miaka 53 ya kuwepo duniani. Alizaliwa huko  Windsor, Ontario, Canada akiwa ni mmoja kati ya mabinti 3 wa Clarence na Sharon (Morison) Edwards. Yeye ndiye mkubwa. Alipokua na miaka 6 mama yake aliolewa tena na Jerry Twain ambaye alimchukua kama mwanaye. Alianza kuimba katika vilabu vya pombe na alipokua na miaka 13 alionekana katika The Tommy Hunter Show. Alipokua na umri wa miaka 22 wazazi wake waliuawa katika ajali na hivyo akaacha sanaa muziki ili awalee wadogo zake Mark na Darryl pamoja na dada zake wawili aliozaliwa nao kwa baba yake na mama yake mzazi. Mwaka 1991 alibadilisha jina lake alilopewa na wazazi wake na kujiita Shania Twain na hapo ndipo jina hili lilipokua.  Mwaka huo huo pia alisaini mkataba na lebo ya muziki

LEO AGOSTI 6 KATIKA HISTORIA

Image
Leo ni Agosti 6, 2018 ikiwa ni siku ya 218 katika mwaka 2018. Zimesalia siku 147 katika mwaka huu. Nakukaribisha tena katika muendelezo ya Leo Katika Historia. Kwa leo nimekuletea matukio kadhaa yaliyopata kutokea katika historia ya dunia, na tuanze kuyahesabu matukio hayo: MATUKIO 1787 - Rasimu ya Kwanza ya Katiba ya Marekani ilianza kujadiliwa huko Philadelphia. 1890 - Hukumu ya kuuawa kwa kiti cha umeme ilianza kutekelezwa katika gereza la Auburn huko New York, Marekani ambapo William Kemmier alihukumiwa kifo katika kiti cha umeme kwa kumuua mpenzi wake Matilda Ziegler kwa shoka. Adhabu hii ya kifo ilipendekezwa mwaka 1881 na Dk. Albert Southwick baada kushuhudia mlevi akiuawa kwa shoti ya umeme. Katika kutekeleza adhabu hii zilitumika volti 700 za umeme na katika sekunde 17 umeme ulifeli kabla Kemmier hajafariki na baadaye waliongeza umeme hadi volti 1,030 ndani ya dakika 2 na ndipo Kemmier alifariki. Kiti cha Umeme kilichotumika kutekeleza adhabu ya kifo kwa Kemmier.