Posts

Showing posts from July, 2016

ACTION MUVI MPYA INATOKA AGUST 2, SNIPER: GHOST SHOOTER

Image
Muvi inaitwa Sniper: Ghost Shooter inatarajiwa kuingia sokoni tarehe 2 Agost mwaka huu (siku chache kutoka leo kama siku 5 mbele). Imechezwa na Chad Michael Collins, Billy Zane, Dennis Haysbert na wengine wengi. STORI KWA UFUPI Masnaipa wenye akili Chad Collins (katika muvi hii ameigiza kama Brandon Beckett) na Billy Zane (katika muvi hii anaitwa Richard Miller) wanapewa jukumu la kulinda bomba la gesi ili lisiharibiwe na magaidi. Wanapokuwa katika mambano na maadui inapelekea masnaipa wenzao wengine kuuawa na adui asiyefahamika alipo lakini yeye akiwa anafahamu wao (Richard na Brandon) walipojificha. Hofu inazidi kutanda hadi kufikia safu ya ulinzi kushutumiwa kushirikiana na maadui. Kuna mmoja kati yao anashirikiana na upande wa maadui? Je, mpango ni mwanzo wa mpango mwingine kumjua msaliti? Je, Kanali atatumia muda mwingi kuamua nini kifanyike? Haya yote utayapata katika muvi hii Sniper: Ghost Shooter kuanzia Agost 2, mwaka huu katika tovuti na application za kupakua muvi

CHADEMA 'YAIBIPU' POLISI

Image
Ni wazi sasa kwamba Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeamua kujipima nguvu na Jeshi la Polisi baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kutangaza kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima kuanzia Septemba mosi, mwaka huu. Kamati Kuu hiyo katika maazimio yake yaliyosomwa kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ilisisitiza kuwa azma yake hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kupinga agizo la jeshi hilo la kuzuia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Sababu nyingine zilizoisukuma Kamati Kuu kufikia azma hiyo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe ni pamoja na kupinga zuio la urushwaji wa moja kwa moja wa mijadala ya Bunge, kupinga wabunge wa upinzani kudhibitiwa bungeni, kuingiliwa kwa mhimili wa mahakama, upuuzwaji wa utawala wa sheria na haki ya kupata habari. Katika hatua nyingine, Kamati Kuu ya Chadema imezindua operesheni Ukuta yenye lengo la kupambana na kile ilichokiita kuwa ni udikteta nchini, huku ikitangaza kus

WAZIRI MKUU WA NEPAL KHADGA PRASAD OLI AMEJIUZURU

Image
Waziri Mkuu wa Nepal Khadga Prasad Oli amejiuziru wadhifa wake ikiwa ni muda mchache kabla ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye katika Bunge la nchi hiyo. Inadaiwa katika kura hiyo Oli angeshindwa. Oli mwenye umri wa miaka 64 alishinikizwa kujiuzuru na wapinzani wa chama chake kufuatia kutoheshimu mgawanyo wa madaraka ambao ndiyo uliompa Uwaziri mkuu miezi 9 iliyopita. "Nimekwisha wasilisha barua yangu ya kujiuzuru kwa Rais nilipokutana naye kabla hata ya Bunge" amesikika akisema Oli aliponukuliwa na The Reuters katika Bunge la Nepal. Oli aliyezaliwa kaskazini mwa Nepal Fenruari 22 mwaka 1952 alikuwa mwanachawa wa Nepal Communist Party mwaka 1970 baada ya kuvutiwa na viongozi wa kikomunisti alipokuwa kijana. Amewahi kutumikia kifungo cha miaka 14 jela. Oli aliingia madarakani Oktoba mwaka jana huku akikosolewa sana na kuwepo kwa maandamano kufuatia kushindwa kuchukua hatua katika tetemeko lililowaacha wananchi katika umaskini mkubwa. Zaidi ya watu 50 wali

BARAZA LA MITIHANI LIMETANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2016

Image
Matokeo ya Kidato cha Sita 2016 yametoka, unaweza kuyaona kwa kubofya  HAPA

SATELITE YA JUNO YAFIKA KATIKA SAYARI YA JUPITA

Image
Satelite ya Juno ikiwa imewasili katika sayari ya Jupita. Satelite ya Juno inayokuwa inayoongozwa taasisi ya Utafiti wa Anga NASA iliyoko nchini Marekani imefanikiwa kufika katika sayari ya Jupita ambayo ni sayari ya tano katika mfumo wa jua kutoka kwenye jua. Satelite hiyo ya Juno iliondoka duniani miaka mitano iliyopita ambayo ilikuwa na rocket engine kuiongoza satelite hiyo mpaka kuifika satelite hiyo.. Wattafiti wanapanga kuitumia satelite hiyo kuichunguza sayari hiyo kwa jina. Wanadai kuwa muonekano wa sayari hiyo na kemia yake unaweza kuichunguza zaidi sayari hii ambayo ni kubwa kuliko zote katika mfumo wa jua toka ilipotengenezwa zaidi ys miaka bilioni 4 na nusu iliyopita. Hakuna chombo kilichofanikiwa kupita au kuisogelea sayari hiyo ya Jupita kutokana na mionzi iliyopo katika sayari hii kama chombo hicho hakijalindwa na vifaa maalumu vya kieletroniki ambavyo vinazuia mionzi hiyo kupenya. Mahesabu ya haraka yanaonesha kuwa satelite hiyo imeundwa kwa miyonzi zenye

MAN WATER AELEZA SABABU ZA KUWARUDISHA WAKONGWE KWENYE MUZIKI

Image
Producer Man Water wa combinataion sound, ameelezea sababu ya kupenda kuwarudisha wasanii wa kitambo kwenye game, ambao tayari walishapotea kimuziki. Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Man Water amesema hupenda kufanya hivyo kwani ana imani wasanii hao bado wana uwezo mkubwa, na kwa kuwa alitoka nao mbali kikazi. “Kurudisha wasanii waliopotea mimi na kuwa nao karibu kwa sababu ni watu wangu ambao nimetoka nao mbali, najua hustle zao tulipita wote, na kwa sababu mi mwenzao bado nimebaki kwenye game, sasa nikiwaita wale nawaambia jinsi gani game ya sasa ilivyo na wabadilike vipi ili waweze kurudi”, alisema Man Water. Man Water alishawahi kumrudisha kwenye game msanii 20% , Alikiba, Lady Jaydee na wengine, huku bado akiwa na mpango wa kuendelea kuwarudisha wasanii wengine kama Mr. Nice. Chanzo: EATV