Posts

Showing posts with the label Makala

UNICEF: WATOTO WALISHAMBULIWA KWA KIWANGO KIKUBWA SANA MWAKA 2017

Image
  Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF, limesema mwaka 2017 ulikuwa miongoni mwa miaka mibaya zaidi kwa watoto wanaoishi katika maeneo ya vita na mizozo duniani. Ripoti ya shirika hilo la UNICEF imesema pande zinazozozana katika vita duniani zilikiuka wazi wazi sheria za kimataifa linapokuja suala la kuwalinda watozo. Mkurugenzi wa UNICEF kuhusu mipango ya dharura Manuel Fontaine amesema watoto walilengwa na kuwekwa katika hatari ya mashambulizi wakiwa nyumbani, shuleni na wakicheza. Fontaine ameongeza kusema ulimwengu haupaswi kuyafumbia macho mashambulizi haya akisisitiza maovu dhidi ya watoto hayapaswi kuwa matukio ya kawaida katika ulimwengu wa sasa. Maovu dhidi ya Watoto ni makubwa Watoto katika mataifa yanayoshuhudia vita wamekuwa waathirika wakubwa wakiuawa, kulemazwa, kusajiliwa kwa lazima kuwa wapiganaji, kuolewa kwa lazima, kutekwa nyara, kutumikishwa na kubakwa. Wapiganaji watoto wa Sudan Kusini. Wengi wa watoto ha

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU KABLA YA KUCHAGUA KOZI CHUO KIKUU

Image
Kumekuepo na manung'uniko miongoni mwa wanafunzi wengi wa vyuo vikuu, manung'uniko haya hutokana na zile kozi wanazosoma chuoni. Kuna sababu kadha wa kadha zinazopelekea manung'uniko hayo miongoni mwa wasomi hawa tukiachilia mbali suala la ucheleweshwaji wa mikopo miongoni mwa wasomi hawa  (kwa sasa changamoto hii inapungua kadiri siku zinavyosonga) tatizo lingine ambalo linawasumbua wasomi hawa ni suala la uchaguzi wa kozi gani akaisome Chuo Kikuu. Kuna mambo kadhaa ambayo huwakuta wanafunzi hawa wawapo vyuo vikuu, mambo haya yaweza kuwa; kutoendelea na masomo ya Chuo Kikuu kutokana na kufeli masomo (Discontinuation from studies), kufeli majaribio mara kwa mara kutokana na kutoridhika na kile wanachosomea ama ugumu wa masomo. Sababu kubwa hapa zaweza kuwa tatu; kwanza, uchaguzi wa kozi kwa kufuata mkumbo wa marafiki, pili, kushawishiwa ama kuchaguliwa kozi na mzazi ama mtu yeyote aliyesoma kozi husika na kupata mafanikio kwa hivyo na mchaguaji anaona naye asome kozi

HABARI LEO TAHARIRI: TFF IFANYIE KAZI KASORO ZA MSIMU ULIOMALIZIKA

Image
MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara umemalizika Jumamosi iliyopita, huku timu za Polisi Morogoro na Ruvu Shooting ya mkoani Pwani zikishuka daraja. Kushuka kwa timu hizo mbili kunatoa nafasi kwa timu nne kupanda daraja kukiwa na lengo la kuongeza timu shiriki kutoka 14 hadi 16 katika msimu ujao wa ligi hiyo. Timu zilizopanda daraja ni Majimaji ya Songea, African Sports ya Tanga, Toto African ya Mwanza na Mwadui ya Shinyanga, ambazo zinakamilisha timu hizo nne. Wakati msimu huo wa ligi ukifungwa, tayari Yanga na Azam FC walishajitangazia nafasi za kwanza na pili na kuwa na uhakika wa kuliwakilisha taifa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa na ile ya Shirikisho la Afrika. Baada ya kumalizika kwa msimu huu wa ligi ndio mwanzo wa msimu unaokuja na timu zinatakiwa kujipanga vizuri kwa ajili ya msimu huo, ambao kama baadhi ya makosa yatarekebishwa, inaweza kuwa ligi bora zaidi. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), timu pamoja na wadau wengine wa ligi hiyo kama kamati mbalimbali, ambaz