Skip to main content

Posts

SHAIRI: HEKO LIBERIA

Picha kwa hisani ya Freepik Shairi hili linakuja kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka huu nchini Liberia. Katika hali isiyo ya kawaida George Weah aliyekuwa akitetea nafasi yake ali kubali kusindwa na mpinzani wake Joseph Boakai katika Uchaguzi huo pasipo mvutano na migogoro kama ilivyozoeleka katika mataifa mengi ya bara hili . Kama mshairi niliwiwa kuandika ili kupongeza kitendo hiki cha uungwana kukubali kukabidhi madaraka pasipo mvutano ambao mara nyingi hupelekea umwagaji damu. Karibu katika shairi letu kwa lugha adhimu ya Kiswahili. Shairi: Heko Liberia Mtunzi: Venance Gilbert Mpate Mwaka: 19 Novemba 2023 HEKO LIBERIA Heko Liberia naisifu yenu demokrasia, Wenu ukomavu yote Afrika imeshuhudia, Tupeni maarifa darasani tupate kujifunzia, Afrika matokeo mshindani hawezi kuridhia, Uchaguzi mtawala hakubali kupoteza felia, Ninyi metuonesha mtawala aweza kuwa felia, Mpinzani akashika dola imani ikaendelea, Heko Liberia naisifu yenu demokrasia. Mtawala aku...

TANGAZO LA AJIRA 289 ZA WATUMISHI KADA ZA AFYA KUTOKA WIZARA YA AFYA

Wizara ya Afya kupitia Kibali cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/128/01/” B”/75 cha tarehe 04 Mei, 2023 na Kumb. Na FA.97/128/01”B”/78 cha tarehe 09 Agosti, 2023; Inatangaza nafasi za kazi 289 za Kada za Afya. Muda wa kutuma maombi haya ni ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili. Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Wizara unaopatika kupitia tovuti ajira.moh.go.tz . Waombaji wote mnakumbushwa kuwa makini mnapowasilisha maombi kuhakikisha umejaza vizuri vipengele vyote vinavyotakiwa kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na kuambatisha nyaraka zote zinazohitajika. Unaweza kutazama tangazo hilo kwa kubofya  HAPA  ama kwa kulidownload moja kwa moja kwa kubofya  HAPA  ama kwa kusoma hapa chini nafasi zilizotangazwa: 1. Daktari wa Meno Daraja la II – TGHS E (NAFASI 3) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Udaktari/Udaktari wa Meno ku...

TEKNOLOJIA ZA KALE ZINAZOTUMIKA HADI SASA

U hali gani? Nakukaribisha tena kwa mara nyingine katika blog hii. Leo nakukaribisha hapa tuangalie kuhusu mfululizo wa teknolojia tukijikita zaidi katika teknolojia za kale. Kwa kusema hivi nataka nikukutanishe na vumbuzi 10 za kale ambazo zilibadilisha maisha ya binadamu kwa kiasi kikubwa na bado vumbuzi hizo ni za manufaa hata kwa maisha ya leo. Nakukumbusha tena kwamba huu ni mfululizo wa teknolojia na vumbuzi mbalimbali. Tuanze sasa kuhesabu vumbuzi hizo: 1. Gurudumu Mabadiliko katika maendeleo ya magurudumu katika vyombo mbalimbali. Ugunduzi wa gurudumu ni moja ya maendeleo muhimu zaidi ya kiteknolojia katika historia ya mwanadamu. Magurudumu ya awali zaidi hayakutumika kwa usafiri badala yake kama magurudumu ya mfinyanzi yanayoaminika kutumika mara ya kwanza huko Mesopotamia (kwa sasa Iraq) karibu mwaka 3500 KK (Kabla ya Kristo). Kufikia mwaka 3200 KK, watu wa Mesopotamia walianza kutumia magurudumu kwa magari ya vita na mikokoteni. Magurudumu haya ya kwanza yalikuwa...