Posts

Showing posts from December, 2014

IN THE NEXT - A POEM BY VENANCE GILBERT

Image
Poem: IN THE NEXT   Poet:  Venance Gilbert   Composition: December 19, 2014  First published on the blog: December 29, 2014 The system has turned to uplift us, From nothing to something mammoth, Look at them brother, look them twice more, They have our consent in authority, Having our consent to share our sufferings, For self into their bellies, Look brother, feel pitty for ourselves, The cultural similarity is credited, Now brother tell them involved, Go into details to them, In the next to put their money where their mouth are, Let them experience a miss in the next, To re-drink the milk of human kindness. All rights reserved. Venance Gilbert © 2014. IF YOU HAVE ANYTHING TO COMMENT DON'T HESITATE TO CONTACT ME THROUGH: Facebook: VENANCE BLOG Twitter: @Venancetz Instagram: venancegilbert Mobile: 0753400208 Email: venancegilbert@gmail.com. VENANCE BLOG WISHES YOU A HAPPY NEW YEAR 2015!!

KOREA KASKAZINI YAMTUSI OBAMA

Image
Korea kaskazini imeilaumu Marekani kutokana na mataizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita. Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananishi rais wa marekani Barack obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa ka filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview. Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un. Korea kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.

KUMBUKUMBU YA MIAKA 10 TANGU JANGA LA TSUNAMI MWAKA 2004

Image
Mataifa yaliyoathirika na janga la Tsunami yameandaa ibada za kuwakumbuka watu 220,000 waliouawa wakati mawimbi makali yalipoyapiga maeneo ya pwani ya Bahari Hindi mwongo mmoja uliopita. Mnamo Desemba 26 mwaka wa 2004, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 9.3 katika upande wa magharibi wa Indonesia lilianzisha msururu wa mawimbi makali ambayo yaliupiga mwambao wa mataifa 14 ikiwa ni pamoja na Indonesia, Thailand, Sri Lanka na Somalia. Miongoni mwa wahanga waliopoteza maisha yao ni maelfu ya watalii waliokuwa wakisherehekea siku kuu ya Krismasi katika eneo hilo, na kulipeleka janga la maafa ya asilia ambayo hayakuwa yametarajiwa hadi majumbani kote ulimwenguni. Maelfu ya watu wameimba wimbo wa taifa wa Indonesia kama mwanzo wa kumbukumbu ya janga hilo, kwenye ibada iliyoandaliwa Banda Aceh - mji mkuu wa mkoa ulio karibu na kitovu cha tetemeko la arshi ambalo lilisababisha mawimbi hayo makali. Mapema leo misikiti pia iliandaa maombi kite katika mkoa huo, wakati watu w

BOTI YAZAMA NA WATU 36 JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO

Image
Ripoti kutoka kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo zinasema kuwa mashua moja iliyokuwa imebeba bidhaa na abiria imezama na karibu watu 36. Maafisa wanasema kuwa zaidi ya watu 100 wamenusurika. Inaripotiwa kuwa ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatatu umbali wa kilomita 30 kutoka mji wa kisangani na kusababisa maandamano yaliyofanywa na vijana wenye hasira kwenye mji wa Isangi ambapo mashua hiyo ilikuwa ikielekea nyumba kadha za serikali zinaripotiwa kuchomwa. Chanzo: BBC Swahili WASILIANA NAMI:  Facebook: VENANCE BLOG Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert Simu: +255712586027/753400208  Email: venancegilbert@gmail.com

VENANCE BLOG INAWATAKIA HERI YA CHRISTMAS 2014

Image
VENANCE BLOG inapenda kuwatakia heri ya Christmas kwa mwaka huu 2014 tusherekee kwa amani na upendo huku tukimtanguliza Mungu katika kila jambo kwani yeye ndo muweza wa yote. Heri ya Krismas na pia Heri ya Mwaka mpya 2015!! WASILIANA NAMI:  Facebook: VENANCE BLOG  Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert Simu: +255712586027/+255753400208  Email: venancegilbert@gmail.com

VIDEO MPYA: BRACKETS-ALIVE FT DIAMOND & TIWA ICHEKI HAPA NA KUDOWNLOAD

Image
Alive -“Hii ni hadithi ya kweli ya Vast Bracket, safari yake hadi alivyopona kansa mwaka 2013. Huu ni wimbo wa shukrani kwa kumfanya mshindi aliyeishinda kansa.” Hayo ni maneno yanayoonekana mwanzoni mwa video ya wimbo mpya ya kundi la Bracket kutoka Nigeria iliyotoka wiki hii, ambao wamemshirikisha Diamond Platnumz na Tiwa Savage. Kipindi Vast anaumwa kansa Memba wa kundi hilo aitwaye Vast, mwaka 2013 alikuwa akipigania uhai wake baada ya kuugua kansa ya damu ambayo baadae alifanikiwa kupona, ndio sababu ya kundi hilo kuamua kurekodi wimbo huu ‘Alive’ kwaajili ya kumshukuru Mungu kutokana na kumuwezesha msanii huyo kupona. Vast ni yule ambaye anaimba vesre ya kwanza na kwenye video anaonekana yupo hospitali. Video hii hapa Vast aliwahi kuelezea jinsi alivyougua hadi kupona katika mahojiano mbalimbali aliyofanyiwa 2013: “It all started when we went on an American tour and I started feeling feverish. I found myself taking my bath with hot

KUREJESHWA KWA ADHABU YA KIFO AFGHANSTAN KWAWAPA WASIWASI AMNESTY

Image
Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif ametangaza kurejeshwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa, kwa watakaokutwa na hatia ya ugaidi ingawa Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linapinga sheria hiyo. Pakistan imetoa uamuzi wa kurejesha sheria ya kunyonga watakaokutwa na hatia ya ugaidi. Hatua hiyo ilitangazwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Nawaz Sharif, siku moja baada ya mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Taliban na kusababisha vifo vya watu 150, wakiwemo wanafunzi 135. Mashambulizi hayo yalitokea tarehe (16.12.2014), katika shule inayomilikiwa na jeshi ilioko mjini Peshawar. Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kurejeshwa kwa adhabu ya kifo, hakutaisaidia Pakistan kupambana na Ugaidi. Azimio hilo lilipitishwa bila ya pingamizi tarehe (17.12.2014), katika mkutano uliojumuisha vyama vyote vya siasa vya nchi hiyo. Pakistan imesema kuwa kurejesha kwa sheria ya kunyonga walio na hatia ya ugaidi ni hatua muhimu, kwani katu haiwezi kuonye

MMAREKANI MWEUSI AWAUA ASKARI WAWILI WA MAREKANI NA BASTOLA NA KISHA KUJIUA MWENYEWE

Image
Mtu mmoja nchini Marekani amewaua askari wawili waliokuwa kaka patrol wakiwa wamevalia nguo za kazi. Inadaiwa kuwa mtu huyo aliwalenda askari hao na kuwafatulia risasi na baadae kujiua mwenyewe.  Hii ni bastola iliyokutwa eneo la tukio. Inasemekana kuwa mwanaume huyo aliwahi kumjeruhi mpenzi wake wa zamani kwa kumfyatulia risasi iliyomsababishia majeraha. Áidha inasemekana pia kuwa kabla hajatenda tukio hilo aliandika kwenye mitandao ya kijamii ujumbe ambao si mzuri kwa polisi. Pia aliweka picha ya bastola hyo katika akaunti yake ya Instagram na kuañdika kuwa hiyo ndio itakuwa post yake ya mwisho. Aidha mtu huyo ambaye ni Mmarekani mweusi ametajwa kwa jina la Ismaail Brinsley miaka 28 na maofisa hao kuwa ni Liu Wenjin na Raphael Ramos. Mauàji hayo yametokea kufuatia kuwepo na mauaji ya watu weusi Marekani wanaouawa na maaskari weupe wa Marekani na kutochukuliwa hatua zozote na nchi hiyo.. Rais Obama wa Marekàni aliye katika jimbo la Hawaii kwa mapumziko ya sikukuu a

ICHEKI KWA MARA YA KWANZA VIDEO YA ALI KIBA - "MWANA"

Image
Video iliyosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa Ali Kiba ‘Mwana’ imeachiwa leo hii Ijumaa ya 19 Decemba 2014.  Ali Kiba Alithibitisha kuwa video imekamilika na kusema Video imetayarishwa na muongozaji kutoka Afrika Kusini na imefanyika maeneo ya mjii wa Cape Town. Vituo vitakavyo rusha hii video  Cameroon, Ethiopia, Angola, U.S. & U.K. itachezwa kwenye vituo vya 1Musicnetworks. Nigeria na Ghana itachezwa kwenye kituo cha SOUNDCITYtv. Uganda itachezwa kwenye kituo cha NTVUganda. Kenya itachezwa kwenye kituo cha Citizen Tv kwenye kipindi cha Mseto. Tanzania itachezwa kwenye kituo cha CloudsTV. Hii ndio Video Halisi ya Mwana itazame .

DOWNLOAD WIMBO MPYA WA BRACKETS FT DIAMOND PLATNUMZ NA TIWA SEVAGE HAPA

Image
Wakati Davido wa Nigeria akimponda sana Diamond Platnumz, kuwa hana fadhila, wasanii kutoka Nigeria Brackets wamakuja na ujio mpya wa Wimbo wao uitwao Alive ukiwa kama gospel fulani, wakiwa wanamshukuru Mwenyezi Mungu. Mwanadada Tiwa Savage pia amehusika humu ndani. Diamond a.k.a. Chibu Dangote kama kawaida kawakilisha kwa lugha yetu ya KISWAHILI.   ILI KUDOWNLOAD WIMBO HUU BONYEZA HAPA WASILIANA NAMI : Facebook: VENANCE BLOG Twitter: @ Venancetz Instagram : venancegilbert

UMOJA WA MATAIFA WAOMBA MSAADA KWA AJILI YA SYRIA

Image
Umoja wa Mataifa umeomba kiasi cha Dola bilioni 8.4 kwa ajili ya kutoa msaada wa dharura wa kibinaadamu kwa takribani watu milioni 18 wa Syria na kuzunguka ukanda huo unaokumbwa na mzozo. Ombi hilo limetolewa jana na maafisa wa Umoja wa Mataifa mjini Berlin, Ujerumani kwenye mkutano wa wafadhili na wamesema msaada huo unahitajika haraka nchini Syria, na katika nchi na jamii zinazopambana kuwahifadhi wakimbizi wa Syria. Kwa mara ya kwanza ombi hilo la Umoja wa Mataifa, linahusisha msaada wa chakula cha kuwapa nguvu na kurudisha afya, malazi, msaada mwingine wa kibinaadamu pamoja na msaada wa maendeleo. Maafisa wa umoja huo wamesema Dola bilioni 2.9 zinahitajika ili kuwasaidia watu milioni 12.2 walioko ndani ya Syria kwa mwaka 2015, na Dola bilioni 5.5 zinahitajika kwa ajili ya Wasyria walioomba hifadhi ya ukimbizi kwenye nchi jirani na zaidi ya watu milioni moja katika jamii zinazowahudumia. Kiasi hicho cha fedha kilichoombwa mjini Berlin, ni kikubwa zaidi ya kile kilichoombwa

BAISKELI YA DHAHABU YATENGENEZWA BEI YAKE INASHINDA FERARI

Image
Kampuni ya Goldgenie iliyopo nchini Uingereza inayojihusisha na kutengezeza vitu vya kifahari, imezindua baiskeli yake mpya ya dhahabu yenye thamani ya dola 390,000 ambayo ni bei ghali hata kuliko gari jipya la Ferrari. Gia za baikeli hiyo zimetengezwa kwa dhahabu pamoja na mikono na vyuma vyake vyote ambapo kiwango cha dhahabu iliyotumiwa ni karati 24. Wataalamu wa kampuni hio ya Goldgenie, wameweka dhahabu katika vyuma vya baiskeli hio vyote , mnyororo na mfumo unaofanya baiskeli kwenda na kubadilisha gia vyote vimewekwa dhahabu. Mkurugenzi wakampuni iliyotengeza baiskeli hiyo anasema inaweza kuendeshwa kwa barabara kama baiskeli nyinginezo. Na wakati baiskeli hio inavutia macho, inapowekwa nyuma ya kabati ya glasi na kulindwa na walinzi. Mkurugenzi wa kampuni hio anasema baiskeli hio inaweza kuendeshwa kwenye barabara. “Baiskeli hii sio tu ya kuvutia macho, bali pia ni nzuri ya kuendesha ikiwa mwenye kuiendesha atsatahimili kuangaliwa sana.” Muundo wa baiskeli h

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

Image
Nicki Minaja haishiwi vituko vya kupost picha mtandaoni akiwa uchi kabsa ama nusu uchi. Tazama hiyo picha hapo juu inayoonesha matako yake yakiwa wazi. Picha nyingine hii hapa japo amevaa nguo lakini mmmh!! Kwa wanaume so conducive kabisaaa. Cheki jinsi tako lilivyobinuliwa hapa hivi eti njiani anakopita kwa mavazi haya hawapi wanaume shida!!! Haya yote yanakuja wakati Nicki anajiandaa kuachia Album yake mpya ya Pink Friday Print. Album hiyo inapatikana kwenye iTune pia. Picha hizo ziko katika akaunti yake ya Instagram @nickiminaj.  WASILIANA NAMI:  Facebook: VENANCE BLOG  Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert  Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014

HUENDA TANZANIA IKAKOSA MSAADA KUTOKA MAREKANI KWA SABABU YA RUSHWA

Image
Serikali ya Tanzania iko hatarini kukosa dola za Marekani milioni mia saba sawa na trilioni 1.1 kwa fedha za Tanzania kwa ajili ya mradi wa pili wa mfuko wa changamoto za Milenia (MCC) kutokana na kushamiri kwa vitendo vya rushwa nchini humo. Marekani imebainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo. Haya yanajiri wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kutoa maamuzi ya mapendekezo yaliyofikiwa na Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 kutoka kaunti ya Tegeta Escrow wiki ijayo. Katika tamko hilo kwa umma ambalo limewekwa kwenye tovuti ya MCC, bodi ilieleza kutambua umuhimu wa kusubiri na kuona utekelezaji kamilifu wa tamko lililotolewa na Ikulu ya Tanzania Desemba 9, mwaka huu kwamba itachukua hatua za haraka na kutoa maamuzi dhahiri na thabiti kuhusu maazimio ya Bunge juu la suala la IPTL. Taarifa

VIDEO MPYA: NIKKI II FT BEN POL-SITAKI KAZI ITAZAME HAPA

Image
Nikki wa pili ameachia video ya wimbo wake Sitaki kazi alomshirikisha Ben Pol. Kitu kimoja Nikki alitakiwa afanye kuchoma vyeti kama alivyoimba hata asingechoma vyeti halisi ilitakiwa afanye hivyo. Video hii hapa chini: LIKE PAGE YANGU YA FACEBOOK NIFUATE TWITTER NIFUATE INSTAGRAM Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014

MTANDAO WA INSTAGRAM WAFIKISHA WATUMIAJI MILION 300

Image
Mtandao wa Instagram leo umefikisha jumla ya watumiaji milioni 300 dunia nzima huku kukiwa na picha na video zaidi ya milioni 70 ambazo zinawekwa kila siku katika mtandao huo. Uongozi wa mtandao huo umeahidi kutatua tatizo la akaunti za watu maarufu ambazo hu-hakiwa na watu na kuahidi kuzifuta akaunti hizo hivyo kutoa taarifa kwamba watu wasishangae kuona idadi ya watu wanaowafuata kupungua. WASILIANA NAMI:  Facebook: VENANCE BLOG  Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert   Asante kwa kutembelea VENANCE BLOG © 2014

VIDEO MPYA: AY FT MS TRINITY & LA'MYIA ICHEKI HAPA

Image
Mwanamuziki Ambwene Yesaya a.k.a. A.Y. kutoka hapa hapa Bongo land Tz ameachia video ya wimbo wake uitwao Touch me alowashirikisha Sean Kingston na Ms Trinity. Pata nafasi ya kuangalia video hiyo hapa chini ama fuatisha  KIUNGO HIKI  kuingalia katika akaunti yake ya Youtube. Video hii hapa chini;

EXCLUSIVE: DAVIDO ATOA VIDEO YA WIMBO WAKE 'OWO NI KOKO' ITAZAME HAPA

Image
  Mwanamuziki kutoka Nigeria, Davido ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao Owo ni Koko.  WASILIANA NAMI KWA: Facebook: VENANCE BLOG  Twitter: @Venancetz  Instagram: venancegilbert KWA HISANNI YA DJ CHOKA MUSIC