KUELEKEA MWISHONI 2016 LADY JAY DEE KAYAANDIKA HAYA INSTAGRAM
Kuelekea mwisho wa mwaka 2016 msanii mkongwe Lady Jay Dee ameyaandika haya katika mtandao wa Instagram: "Kiukweli comeback yangu ya 2016 ilikuwa kubwa sana kuliko watu wengi walivyoitegemea mbali na changamoto ngumu na nyingi nilizowahi kupitia na ninazoendelea kuzipitia kuliko msanii yeyote yule wa kike wala wa kiume Tanzania nadiriki kusema bado nimesimama Imara *Kejeli *Dhihaka *Mabezo *Kutengwa *Story za kusingiziwa ikiwemo kuambiwa nyumba yangu inauzwa sijui inapigwa mnada na mengine yote mnayoyajua ni vitu vinavyovunja moyo sana. Ila Wa Tanzania ninawaheshimu sana linapokuja swala la kupigania kitu mnachokipenda. Hivi bila nyie si ningekuwa marehemu??? Bila fans JayDee ni nani??? Ninawashukuru kwa kuniamsha. Ninawashukuru kwa kuniamini. Ninawashukuru kwa kunipa nguvu na jeuri. Kuanzia Ndindindi mpaka Together *Mliijaza Mlimani City *Mkajaza mikoa niliyopita. Nawaomba muendelee kujaa 2017. Ili kuwadhihirishia wanadamu kuwa Mungu huwa ni mmoja tu. Happy new year to my fans a...