WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

Uhali gani msomaji na mfuatiliaji wa VENANCE BLOG? Nakukaribisha katika darasa jipya la kufahamu mambo kadha wa kadha kama yanavyokuwa yakipigiwa kura na watu kutoka vyanzo tofauti kama vile tovuti, mitandao ya kijamii, watu wenye ushawishi, majarida n.k. Basi kwa kuanza leo nakuletea orodha ya waigizaji 10 wa kiume wenye mvuto nchini Korea. Vigezo vilivyotumika husemwa na mtandao husika unaotoa orodha hiyo. Ili kurahisisha kazi hii, mimi kama Blogger ntakuletea orodha hizi kila siku kwa lugha ya Kiswahili. Na tuanze sasa, tunaanzia Korea Kusini kuangalia waigizaji wa kiume wenye mvuto kwa mwaka 2017:

#10. Lee Byung-Hun

Lee Byung-Hyun ni muimbaji, mwanamitindo na muigizaji kutokea Korea ya Kusini. Anamiliki kampuni yake ya BH Entertainment. Ni muhitimu wa masuala ya filam na maigizo katika Chuo Kikuu Chung Ang. Anazungumza Kiingereza, Kifaransa, Kikorea na Kimandarin lakini pia ni mfuasi wa dini ya Budha. Alizaliwa Julai 12, 1972 katika jimbo la Gyeonggi Korea ya Kusini. Alianza kuigiza katika televisheni ya KBS katika baadhi ya matukio ya mchezo wa kuigiza "Asphalt My Hometown" Aliendelea kuigiza hadi mwaka 2000 alipoigiza muvi iliyompa umaarufu zaidi na kuuza sana nchini humo, muvi hiyo iliitwa "Joint Security Area" Lee ni mwanachama wa Academy of Motion Picture Arts and Science huko Hollywood Marekani.


#9. Jang Geun-Suk


Jang anapenda kutereza kwenye barafu, kuimba na kucheza. Ni muhitimu wa masuala ya filam na maonesho ya jukwaani katika Chuo Kikuu cha Yang Han nchini Korea Kusini. Alianza kuigiza mwaka 2008 katika Kdrama ambapo aliigiza katika "Beethon Virus" aliigiza pia mwaka 2009 katika "You are Beautiful" na mwaka 2010 "Marry Stayed Out All Night" yote akifanya Kdrama. Kwa sasa anafanya kazi kama muigizaji na muongozaji. Jang alizaliwa Agost 4, 1987 na ameonekana vyema katika maonesho zaidi ya 20 aliyowahi kuigiza. Jang anafahamika kama muigizaji anayejituma sana katika Kdrama. Mwaka jana 2016 aliachia albam zake kadhaa za muziki zikiwemo mbili za "Just Crazy" na "Lounge H". Mnamo Julai mwaka jana 2016 aifanya ziara yake ya kimuziki barani Asia ikiwemo Seoul nchini Korea Kusini, China na Japan ambako alipata mafanikio makubwa katika ziara yake hiyo ya "It's Show Time"  kwa sasa anashughilika na kipindi cha maisha halisi kinachoitwa "My Ear's Candy"


#8. Gong Yoo

Alizaliwa Julai 10, 1979. Ni muhitimu wa Chuo Kikuu cha Kyung Hee akiwa na Shahada ya Sanaa na Maonesho. Anafahamika zaidi kwa kucheza michezo ya Martial Art ya Urusi, pamoja na kupanda kwenye miamba kama alivyoigiza katika "The Suspect" (2013). Alitajwa kama muigizaji maarufu zaidi nchini Korea Kusini mwaka jana 2016. Amewahi kuigiza katika muvi ya mazombi "Train to Busan" alipoambiwa atoe maoni kuhusu muvi hiyo alisema "nilidhani muvi za mazombi na kupigana ni rahisi sana, nilihangaika mno"

#7. Song Joong-Ki

Song alianza kuigiza kama utani tu katika shindano la Kdarama ambalo lililenga kutafuta vipaji "Descendants of the Sun" Kuuigiza haikuwa chaguo lake. Amewahi kushiriki katika michezo ya kutereza kwenye barafu ngazi ya taifa lakini alishindwa kuendelea kutokana na majeraha ambapo alishindwa kushiriki Olympic. Mwaka 2010 aliandika kitabu cha "Beatiful Skin Project" Mwaka 2008 aliigiza katka "A Frozen River" japokuwa igizo lililompa umaarufu sana ni "Sungkyunkwun Scandal" Mwaka 2017 ameigiza katika "Battleship Island"

#6. Park Yoo-Chun

Park ni muigizaji mwenye tuzo nyingi katika tasnia hii ya filamu naa uigizaji nchini Korea Kusini. Anafahamika pia kwa jina la Micky Yoo-Chun, jina la kiingereza alilopewa alipokuwa Virginia nchini Marekani. Alizaliwa Juni 8, 1986 Seoul mji mkuu wa Korea Kusini. Ni mtuzi wa nyimbo, muimbaji na muigizaji, nyimbo zake zipo katika maadhi ya Kpop, rhythm naa blues. Amewahi kuwa mshiriki katika kundi la DBSK toka 2003 hadi 2009 na kwa sasa yupo ktk kundi la JYJ. Ameigiza katika "Sungkyunkwan Scandal", "Miss Ripley" na "Rooftop Prince" Anafahamika pia kwa jina la "Gland Slam" kutokana na kushinda tuzo kutoka SBS, MBC na KBS ambazo ni maarufu nchini Korea Kusini.

#5. Hyun Bin

Hyun ni mmoja kati ya washindi wa tuzo kadhaa nchini humo. Anapendelea mpira wa kikapu, kuogelea na kwenda maonesho ya filamu. Amezaliwa Septemba 25, 1982 Seuol Korea Kusini. Ni muigizaji katka Kdrama ambapo amekuwa maarufu kupitia "My Name is Kim Sam-soon" ambayo ilimpa umaarufu sana na kumfanya ashinde tuzo za MBC Drama, Top Excellence. Ameigiza pia katika "The Secret Garden" Mwaka 2010 aliachia wimbo wake "Dream In my Heart", mwaka 2011 alitoa "Cant Have You" na "That Man" Mwaka 2010 alishinda tuzo ya Netizen Popularity Award.

#4. Kim Woo-Bin

Kabla hajawa muigizaji katika Kdarama, Kim alikuwa ni mwanamitindo aliyekuwa anatokea katika maonesho ya Seoul Fashion Week nchini Korea Kusini mwaka 2009. Anapenda sana mitindo lakini aliambiwa ili aongeze uzuri katika kazi yake hiyo ashiriki katika uigizaji, alikubali. Aliigiza katika "White Christmas" na baadaye mwaka 2013 aliigiza katika "School 2013" na "The Heirs" ambazo zilifanya aanze kutazamwa na Netizen. Mwaka 2012 alionekana katika fiamu tano zikiwemo "The Con Artist" na "Twenty". Mwaka 2016 aliigiza katika filamu ya uhalifu ya "Master" kama Park Jong-goon.

#3. Lee Jong Suk

Yeye anapenda sana kucheza games. Katika muda wake wa mapumziko anapenda kucheza Taekwondo na kupiga piano. Amezaliwa Septemba 14, 1989 ni muhitimu wa Chuo Kikuu Konkum akiwa na shahada ya filamu. Alianza kazi zake katika tasnia ya burudani kama mwanamitindo akitokea katika Seoul Fashion Week mwaka 2005. Mwaka 2010 alionekana katika "Prosecutor Princess" na baadaye akaonekana pia katika "The Secret Garden" na "School 2013"


#2. Lee Min Ho

Lee Min Ho alizaliwa Juni 22, 1987, anapenda sana filamu, kucheza game, na kucheza soka la miguu. Alihitimu Chuo Kikuu Konkuk akisomea filamu, na pia ana mdogo mmoja wa kike. Kwa mujibu wa IMDB, Min Ho alipokua mdogo alikuwa na ndoto za kuwa mcheza soka mkubwa lakink ndoto hizo zilipotea baada ya kuumia katika mchezo huo. Ameanza kuonekana Kdeama mwaka 2006 katika "Secret Campus" Hakua maarufu sana mpaka alipoigiza kama Goo Jon Pyo kwenye "Boys Over Flowers", na hapo ndipo alipoanza kuwa maarufu katika tasnia ya maigizo. Mwaka 2009 alishinda tuzo kama chipukizi bora kwenye tuzo za KBS Drama Acting Awards. Mafanikio zaidi yalifuata alipoigiza "Personal Tatse", "City Hunter" na "Faith" mwaka 2016 alionekana katika "The Legend of the Blue Sea" pia ni mpiga piano mzuri na muimbaji mwenye voko zake.

#1. Kim Soo-yun

Kim soo-hyun alizaliwa Februari 16, 1988. Ni muhitimu kutoka Chuo Kikuu Chung-Ang. Alionekana kwa mara ya kwanza 2013 kwenye "My Love From Another Star" japokuwa haikua na mwisho mzuri lakini ndiyo hii iliyompa umaarufu katika tasnia hii. Amekuwa akifanya kazi mbali mbali katika tasnia ya burudani nchini Korea Kusini kama vile kuimba, kuigiza, kufanya matamasha na hata kuwa balozi kuiwakilisha nchi yake. Mwaka 2014 alikuwa Balozi wa Goodwill kwa jiji la Seoul. Ameshinda tuzo kadhaa kama vile SBS New Star mwaka 2010, KBS New Actor mwaka 2011, na tuzo ya Popularity and Best Couple Awards.



Chanzo: Trending Top Most

Je, una lolote ungependa kusikia kuhusu chochote kinachohusiana na haya? Niandikie kupitia moja ya njia hizi:
WhatsApp: +255 712 586 027
Facebook: VENANCE BLOG
Instagram: @venanceblog
Twitter: @Venancetz
Barua pepe: venancegilbert@gmail.com

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

BAADHI MAMBO AMBAYO HUKUYAFAHAMU KUHUSU BARA LA AFRIKA