Posts

Showing posts from May, 2015

RAIS KIKWETE AELEKEZA NGUVU KATIKA ELIMU YA KIDATO CHA 5 & 6

Image
Rais Jakaya Kikwete akipokea tuzo maalum kutoka kwa Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Dk.Shukuru Kawambwa kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza na kuboresha elimu nchini wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya elimu yaliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jana. Picha na Ikulu Rais Jakaya Kikwete jana alitumia kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Elimu kuaga wadau wa sekta hiyo, akisema sasa nguvu zielekezwe katika kujenga majengo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu ya sekondari. Rais Kikwete, ambaye alikiri kuwapo udhaifu katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne, alisema mafanikio pia ni makubwa kiasi kwamba sasa hakuna wanafunzi wanaokosa nafasi ya kwenda sekondari baada ya kufaulu na hivyo nguvu sasa inatakiwa kuwekwa katika kuongeza miundombinu ya kidato cha tano na sita. Kikwete alitoa kauli hiyo jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini hapa alipohutubia maelfu ya wakazi wa Dodoma, wakiwamo wanafunzi wa shule za sekondari na msing

PINDA: CCM ITAELEZA HAYA KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU

Image
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, jana alihitimisha mjadala wa makadirio ya Bajeti ya Ofisi yake ya Sh trilioni 5.7 ambayo ilipitishwa na Bunge, huku akifafanua hoja zitakazotumiwa na CCM kuomba kura za wananchi katika Uchaguzi Mkuu ujao. Pinda alisema hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino upo na kufafanua kuwa katika Uchaguzi Mkuu, CCM itatakiwa kueleza mafanikio ya Serikali katika nishati ya umeme vijijini, miundombinu ya barabara, elimu, maji na afya. Alitaka waliokuwa wakijiuliza nani atashinda katika uchaguzi huo, wapitie kidogo historia kuanzia mwaka 1995 mpaka katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika Desemba mwaka jana, ili waelewe nani alipata kipigo. Elimu Akifafanua kwa ufupi mafanikio yaliyopatikana katika elimu, Pinda alisema watakapoulizwa katika sekta hiyo nini kimefanyika, wataweka wazi kuwa ingawa bado kuna changamoto lakini yapo pia mafanikio makubwa. “Wacha tubebe lawama katika changamoto, lakini tutaeleza kuwa katika vyuo vya ufundi mwaka

RAIS NKURUNZINZA KULIPIZA KISASI KWA WAASI

Image
 Burundi Pierre Nkurunziza amewapongeza wanajeshi wazalendo waliozuia mapinduzi na kurejesha hali ya usalama na utawala huru mjini Bujumbura. Rais Nkurunziza amewataka waburundi wazalendo kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi utakaofanyika mwezi juni. Rais huyo alikuwa Mjini Dar es Salaam Tanzania siku ya Jumatano kuhudhuria mkutano wa viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki kundi la wanajeshi waasi walipotangaza ''Mapinduzi'' dhidi ya serikali yake. Viongozi watatu miongoni mwa makamanda 6 wa jeshi waliounga mkono tangazo hilo la ''mapinduzi'' ilikupinga muhula wa tatu wa rais huyo tayari wamekamatwa. Kufikia sasa watu 105,000 wameripotiwa kutorokea mataifa jirani kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa. Baada ya kurejea kutoka Tanzania rais Nkurunzinza alielekea Kaskazini mwa Bujumbura eneo alikotokea kabla ya kurejea katika kasri la rais lililoko katika mji mkuu wa Bujumbura. Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni rais Nkurunzinza a

JACKLINE WOLPER ANASWA LIVE AKITOKA JUMBA LA FREEMASONS

Image
Mshtuko! Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ameibua maswali kwa mashuhuda walimuona ‘live’ akiingia kwenye hekalu la watu wa Jamii ya Siri (Secret Society) ya Freemasons yenye nguvu duniani inayohusishwa na imani za kishetani. TUJIUNGE MTAA WA SOKOINE Tukio hilo lililoibua kizaazaa kwa mashuhuda waliomuona Wolper, lilijiri juzikati, mishale ya jioni kwenye hekalu hilo lililopo Mtaa wa Sokoine mkabala na Hoteli ya Hyatt Regency, The Kilimanjaro jijini Dar jirani na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). SIMU ZAMIMINIKA Likiwa kwenye majukumu ya kusaka habari kama kawaida yake, gazeti hili lilipokea simu kadhaa kutoka kwa mashuhuda hao wakiwataka wanahabari wetu kuwahi eneo la tukio. Kufuatia umbali waliokuwa mapaparazi wetu, ilibidi kuwaomba mashuhuda hao ‘kumfotoa’ picha ambapo mmoja wao alifanya hivyo na kuziwasilisha kwenye meza ya gazeti hili. ALINASWAJE? Akidadavua mazingira aliyonaswa Wolper, shuhuda huyo alikuwa na haya ya kusema: “Kwanza mwanzoni hatukumjua

HABARI LEO TAHARIRI: TFF IFANYIE KAZI KASORO ZA MSIMU ULIOMALIZIKA

Image
MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara umemalizika Jumamosi iliyopita, huku timu za Polisi Morogoro na Ruvu Shooting ya mkoani Pwani zikishuka daraja. Kushuka kwa timu hizo mbili kunatoa nafasi kwa timu nne kupanda daraja kukiwa na lengo la kuongeza timu shiriki kutoka 14 hadi 16 katika msimu ujao wa ligi hiyo. Timu zilizopanda daraja ni Majimaji ya Songea, African Sports ya Tanga, Toto African ya Mwanza na Mwadui ya Shinyanga, ambazo zinakamilisha timu hizo nne. Wakati msimu huo wa ligi ukifungwa, tayari Yanga na Azam FC walishajitangazia nafasi za kwanza na pili na kuwa na uhakika wa kuliwakilisha taifa katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa na ile ya Shirikisho la Afrika. Baada ya kumalizika kwa msimu huu wa ligi ndio mwanzo wa msimu unaokuja na timu zinatakiwa kujipanga vizuri kwa ajili ya msimu huo, ambao kama baadhi ya makosa yatarekebishwa, inaweza kuwa ligi bora zaidi. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), timu pamoja na wadau wengine wa ligi hiyo kama kamati mbalimbali, ambaz

KUONDOKA KWA NGASA YANGA NI PENGO KUBWA KWA TIMU HIYO

Image
KATIBU Mkuu wa klabu ya Yanga, Jonas Tiboroha amekiri kuondoka kwa mshambuliaji Mrisho Ngassa ni pengo kubwa kwa timu yao, lakini amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuhakikisha wanapambana kumbakiza kiungo Haruna Niyonzima. Tiboroha alisema ana uhakika watafikia makubaliano na kiungo huyo bora Afrika Mashariki katika siku chache zijazo ili aendelee kuichezea timu yao msimu ujao na kwa kushirikiana na nyota wengine waliopo na watakaowasajili. Akizungumza na gazeti hili jana, Tiboroha alisema itakuwa wamefanya kosa kubwa endapo watamruhusu nyota huyo kuondoka kwani itakuwa ni pengo jingine baada ya Ngassa kuhamia Free State ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka minne. “Bado tupo kwenye mazungumzo na imani yangu kama Katibu Mkuu wa Yanga ni kwamba msimu ujao Niyonzima atabaki kuichezea Yanga kwa sababu mazungumzo yapo kwenye hatua nzuri na hata yeye mwenyewe ameonekana kutaka kubaki,” alisema Tiboroha. Kiongozi huyo alisema wamekuwa na vikao virefu na viongozi wa juu wa Yanga

KAMANDA WA WAASI ADF KUREJESHWA UGANDA

Image
Waasi wa kikundi cha ADF. SERIKALI ya Tanzania inatarajia kumpeleka Uganda Kamanda wa Kikosi cha Waasi cha ADF cha Uganda, Jamil Mukumu aliyekuwa akitafutwa muda mrefu hapa nchini na Shirika la Kimataifa la Polisi (Interpol). Atapelekwa Uganda baada ya taratibu za kumfikisha mahakamani kukamilika. “Baada ya kukamatwa mtu huyo tuliwauliza Umoja wa Mataifa kama watamchukua, lakini walikataa njia iliyobaki sasa ilibidi tumfikishe mahakamani na kisha mahakama kwa kufuata sheria ya kubadilishana wafungwa na mahabusu atapelekwa Uganda kwenye mashitaka yake,” alisema Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Alisema utaratibu huo wa kumpeleka Uganda unafanyika kisheria kwa sababu ndio njia pekee iliyobaki. Membe alisema pamoja na tukio la wanajeshi wawili kuuawa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na wengine 15 kujeruhiwa, wanajeshi wa Tanzania wanafanya kazi nzuri. Kundi la waasi la ADF limejikita mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(

ALBINO AKATWA VIUNGO KATAVI

Image
Katavi. Mwanamke mmoja mwenye ulemavu wa ngozi, Remi Luchoma (30), Mkazi Kijiji cha Mwamachoma, wilayani Mlele amekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana na kutokomea nacho. Luchoma alikatwa mkono juzi saa sita usiku akiwa nyumbani kwa wazazi wake na sasa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda. Kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo, Dk Joseph Mkemwa alisema majeruhi huyo anaendelea vizuri na matatibu. Akisimulia tukio hilo, Luchoma alisema akiwa amelala chumbani, alishtukia akivamiwa na watu wawili baada ya mlango kuvunjwa. “Walipoingia ndani walinishika na mmoja alitoa panga na kunikata kiganja cha mkono wangu,” alisema Luchoma. Ndugu wa karibu wa Luchoma, Maliselina Jackson alidai kuwa alisikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa dada yake na alipoamka aliwaona watu wawili wakitoka chumbani. “Niliwaona watu wawili wakitoka chumbani alikolala dada wakiwa na kiganja cha mkono, nilipiga kelele za kuomba msaada,” alisema Jackson. Alisema

ANGALIA TRELA YA MUVI MPYA 'MINIONS' KUTOKA UNIVERSAL

Image
Movie mpya inayoitwa Minions imetengenezwa na kampuni kongwe kwa utengenezaji wa movie duniani, Universal. Itaoneshwa kwa mara ya kwanza kwenye sinema mnamo tarehe 10/07/2015. Imetengenezwa kwa wahusika ambao ni wanyama (Animated). Waongozaji wa movie hiyo ni Kyle Balda & Pierre Coffin ambapo Waandishi ni Ken Daurio & Brian Lynch na stering wa movie ni Chris Renaud, Pierre Coffin & Sandra Bullock. Waongozaji wa movie hii wamewahi kuongoza muvi inayoitwa Despicable Man. Tazama video hapo juu au bofya  HAPA . © VENANCE BLOG 2015.

ASTON VILLA YAPIGWA FAINI

Image
Chama cha soka cha England FA, kimeipiga faini ya pound 200,000 klabu ya soka ya Aston Villa, kwa kitendo cha mashabiki kuvamia uwanja kwenye mechi ya robo fainali ya FA Cup dhidi ya West Bromwich Albion. Katika mtanange huo uliopigwa March 7 kwenye dimba la Villa Park, mashabiki wa Aston Villa waliingia uwanjani wakati wachezaji walipopata majeraha na hata mwisho wa mchezo huku viti vikirushwa kutoka kwa mashabiki waliokuwa wamesimama mbali. FA inasema klabu hiyo imeonywa vikali hasa juu ya mwenendo wake katika siku zijazo. Lakini kwa upande wao Villa waliomba msamaha baada ya mechi kuisha na kuongeza kuwa ushindi wao walioupata siku hiyo ulitiwa doa na vitendo vya wale walioshindwa kujizuia wao wenyewe. Naye boss wa West Brom Tony Pulis amewakosoa walinda usalama wa uwanja huo na kuongeza kuwa usalam wa wachezaji wake ulikuwa mashakani.

TIMU ZA SEVILLA NA DNIPOPETROVSK ZATINGA FAINALI EUROPA LIGI

Image
Mashabiki wa timu ya Dnipopetrovsk wakiishangilia timu yao. Nusu fainali ya pili ya Europa ligi iliendelea usiku wa kuamkia leo wakati Dnipopetrovsk ilipomenyana na Napoli huku Fiorentina ikiialika Sevilla. Hadi mwisho wa michezo yote miwili, Dnipro imeingia fainali kwa jumla ya bao 2 kwa 1 bada ya jana kushinda bao 1-0. Nayo Fiorentina imetupwa nje kwa jumla ya bao 5-0 baada jana kuzabuliwa bao mbili nyumbani walipocheza dhidi ya Sevilla. Fainali itapigwa mnamo May 27 huko nchini Poland kati ya Sevilla dhidi ya Dnipropetrovsk.

HALI BADO NI TETE NCHINI BURUNDI

Image
HALI ya Burundi imezidi kuwa tete huku makundi mawili hasimu ya wanajeshi, yamekuwa yakipigana, kila moja likitaka kutawala jiji la Bujumbura. Mapigano hayo ni kati ya wanajeshi wanaomtii Rais Pierre Nkurunziza, ambao wanapambana na wanajeshi wanaompinga, ambao wanamuunga mkono mwanajeshi aliyetangaza mapinduzi, Meja Jenerali Godefroid Niyombare. Ofisa Mwandamizi wa Jeshi nchini humo, alisema wanajeshi wanaomtii Rais Nkurunziza wamefanikiwa kudhibiti na kurejesha maeneo muhimu ya jiji hilo chini ya utawala wa Serikali, ukiwamo uwanja wa ndege. Hata hivyo, viongozi wa wanajeshi wanaompinga Rais huyo, wameendelea kudai kuwa wameipindua Serikali ya nchi hiyo. Hali ya machafuko nchini humo, ilianza baada ya kiongozi huyo kutangaza kuwa ana nia ya kuwania tena kipindi cha tatu cha urais, jambo ambalo wapinzani nchini humo wamedai ni kinyume cha Katiba. Kwa mujibu wa mashuhuda nchini humo, milio ya risasi na mabomu imekuwa ikisikika usiku kucha kuanzia juzi katika mapigano baina

WATU 23 WANADAIWA KUUAWA NA WAASI WA UGANDA HUKO DRC

Image
Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema kuwa watu ishirini na watatu wameuawa kikatili na wanaodaiwa kuwa waasi wa Uganda. Wanane kati ya waliofariki ni wanajeshi wa DRC. Shambulizi hilo lilifanyika Jumatano usiku. Waasi wengi wao wakiwa wa Allied Democratic Forces (ADF) wamefanyana mashambulizi kadhaa kusini mwa mji wa Beni katika siku za hivi karibuni. Umoja wa mataifa unasema kuwa huenda walifanya makosa ya uhalifu wa kivita na vitendo vinavyokiuka ubinadamu . ADF imewaua mamia ya watu wakati mwingine na ndo, panga na visu. Chanzo: BBC

MVUA ZINAZOENDELEA DAR ES SALAAM KUPUNGUA MAKALI JUMAMOSI HII

Image
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua za mfululizo zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zitaendelea kunyesha na kwamba zinatarajia kupungua mwishoni mwa wiki hii. Taarifa hiyo inaweza kuwa habari njema kwa wakazi wa Dar es Salaam na miji mingine iliyoathirika kwa kiasi kikubwa na mvua hizo zilizonyesha mfululizo na kusababisha vifo, uharibifu wa mali na miundombinu, huku hali ya usafiri, upatikanaji wa bidhaa hasa za vyakula ikiwa ngumu katika maeneo mengi. Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa  Huduma za Hali ya Hewa kwa Jamii wa TAM, Hellen Msemo alisema mvua hizi zinatarajia kupungua mwishoni mwa wiki hii; lakini sio kuisha kabisa na kwamba kwa sasa wananchi waendelee kufuatilia taarifa zinazotolewa. “Mvua hizi zitaendelea kunyesha mpaka Ijumaa ya wiki hii na tunaweza kuona jua kidogo Jumamosi lakini sio mvua za kukatika kabisa zitaendelea kunyesha kidogo kidogo,” alisema Msemo. Shule zajaa maji Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Msasani ‘B’, Jane Re