ZIFAHAMU GAUNI BORA 20 ZA MWAKA 2017
Uhali gani msomaji wa VENANCE BLOG? Natumai u mzima, leo nakukaribisha kuzifahamu gauni 20 bora za mwaka 2017 zilizovaliwa na nyota wa fasheni na mitindo uli mwenguni. Tuanze uchambuzi wetu. Huyuy ni Natalie Potman. Muigizaji maarufu katika kiwanda cha filamu Marekani Hollywood. Huenda miezi tisa ya ujauzito huwa migumu sana lakini Natalie hakuchoka katika hilo. Gauni hili ni ubunifu wa Prada na alilivaa katika tuzo za Golden Globe Awrds, unaweza kuona gauni lilivo zuri na kumpendeza mjamzito na mimba yake hapo juu. Unapenda fasheni na mitindo? Basi hili litamfaa zaidi mjamzito. Mwingine huyu. Anaitwa Brie Leson muigizaji mwingine kutoka kiwanda cha filamu Marekani. Brie alivaa gauni hili katika katika tuzo za 89 za Academy Awards. Ni ubunifu wa mwanamitindo Oscar de la Renta. Unaionaje gauni hiyo? Bila shaka kimpasuo hiko kidogo kinapendeza sana pamoja na mchanuo ule wa nyuma kama maua. Haya kazi kwako kupendeza na mtindo huu kwenye red carpet. Huwezi kushindwa ...