WATU SABA WAFARIKI PWANI NA NJOMBE KATIKA MATUKIO TOFAUTI

WATU saba wamekufa katika mikoa ya Njombe na Pwani katika ajali za gari na mtoto kutumbukia kwenye ndoo.Kutoka Njombe, mtoto wa mwaka mmoja, Pendo Mbena amekufa baada ya kutumbukia kwenye ndoo ya maji.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Fulgence Ngonyani alisema mtoto huyo alikufa juzi saa tatu asubuhi katika Kijiji cha Igoma wilayani Njombe.Akielezea tukio hilo, Ngonyani alisema Upendo alikufa baada ya kutumbukia kwenye ndoo iliyokuwa jikoni baada ya kuachwa na mama yake, Agness Mbena (28) aliyekwenda kuchota maji.Katika tukio lingine, Ngonyani alisema mtoto wa miaka mitatu, Kelvin Kyando, mkazi wa Mtalawe amekufa baada ya kugongwa na pikipiki.Alisema ajali hiyo ilitokea mtaa wa Posta, Njombe Mjini baada ya pikipiki yenye namba za usajili T 112 CLX aina ya Fekon, mali ya Kelvin Chaula (21) kumgonga mtembea kwa miguu, mwanafunzi, Anthon Bruno (12) aliyekuwa amembeba Kelvin.“Jeshi la Polisi linamshikilia dereva wa pikipiki. Chanzo cha ajali ni uzembe wa mwendesha pikipiki kwani hakuweza kuchukua tahadhari kwani aneo hili lilikuwa na watoto wengi waliokuwa karibu na barabara,” alisema.Mkoani Pwani, watu wanne wamekufa katika matukio mawili tofauti, wakiwemo watu watatu waliopoteza maisha kwa ajali ya gari.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei alisema ajali hiyo ilitokea saa tano usiku eneo la Vigwaza, wilayani Bagamoyo baada ya Fuso lenye namba za usajili T 775 CHX kugongana na lori lenye namba za usajili T 627 ANA/T 386 ACE.Alitaja waliopoteza maisha kuwa ni dereva Kalista Mwigeni (23), mkazi wa Ilula Iringa, Gerald Muhanga (umri wake kati ya miaka 23-25) utingo wa Fuso, na Deseselia Daudi (50) mkulima wa Morogoro aliyekuwa abiria kwenye lori.Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Noah Msalu (40), mkazi wa Iringa aliyekuwa amekodisha Fuso na Alani Philipo (60), mkazi wa Kipawa jijini Dar es Salaam ambaye ni dereva wa lori Katika tukio lingine, Matei alisema siku ya Jumanne saa 12 asubuhi, Mgaza Mbulu (61) mkazi wa Kijiji cha Kibindu, alikutwa amejinyonga juu ya mti kwa kutumia kamba.Alisema mwili wa marehemu ambaye alikuwa akiishi kijijini hapo bila ndugu wa karibu, ulikabidhiwa kwa viongozi wa kijiji baada ya kufanyiwa uchunguzi na daktari. “Marehemu hakuacha ujumbe wowote wa kueleza sababu za kujitoa maisha na upelelezi unaendelea,” alisema.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017