Viongozi wa nchi tajiri zaidi duniani zinazounda kundi la G7
wanatarajiwa hii leo kutoa msimamo wa pamoja dhidi ya vitisho vya
kiuslama vinavyoikumba dunia vikiwemo kitisho cha makundi ya wanamgambo
wenye itikadi kali hadi kile Rais wa Marekani Barack Obama amelaani na
kuutaja kama uchokozi wa Urusi nchini Ukraine. Kwa mara ya tatu
mfululizo, viongozi hao wamemtenga Rais wa Urusi Vladimir Putin kutoka
mkutano huo ulioanza hapo jana na unaokamilika hii leo katika mji wa
Elmau nchini Ujerumani na badala yake wamewaalika viongozi kutoka
kwingineko akiwemo waziri mkuu wa Iraq Haider al Abadi na Rais wa
Nigeria Muhammadu Buhari ambao wote wawili wanakabiliwa na kitisho
kutoka makundi ya wanamgambo. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais
wa Ufaransa Francois Hollande wanatarajiwa kuangazia masuala ya
mazingira katika mkutano huo hasa kuongezeka kwa viwango vya joto
duniani na athari zake.
Chanzo: DW
Comments
Post a Comment