Picha kwa hisani ya Freepik |
Shairi: Heko LiberiaMtunzi: Venance Gilbert MpateMwaka: 19 Novemba 2023HEKO LIBERIA
Heko Liberia naisifu yenu demokrasia,Wenu ukomavu yote Afrika imeshuhudia,Tupeni maarifa darasani tupate kujifunzia,Afrika matokeo mshindani hawezi kuridhia,Uchaguzi mtawala hakubali kupoteza felia,Ninyi metuonesha mtawala aweza kuwa felia,Mpinzani akashika dola imani ikaendelea,Heko Liberia naisifu yenu demokrasia.Mtawala akubali mwenyewe kupoteza,Dola pembeni madarakani kumbakiza,Tume uchaguzi naipongeza kujitakatifuza,Afrika demokrasia miguu yajikomaza,Kwingine tuanze maarifa kupenyeza,Yeyote uchaguzini aweza kupoteza,Hakika demokrasia haitakuwa ajuza,Heko Liberia naisifu yenu demokrasia.Afrika ikome migogoro uchaguzini,
Pumzi tulonayo watawala iheshimuni,
Vita uchaguzini visalie historiani,
Itamalaki demokrasia kote barani,
Furahani tuishi mwetu majumbani,
Yafaa nini kuwemo migogoroni?
Afrika Afrika tuishi demokrasiani,
Heko Liberia naisifu yenu demokrasia.
Kama una maoni kuhusu shairi hili usisite kuandika hapa chini ama kuniandikia katika barua pepe yangu: venancegilbert@gmail.com
0 comments:
Post a Comment