MSIBA: MZEE SMALL AFARIKI DUNIA



Muigizaji mkongwe hapa nchini, Said Ngamba maarufu kwa jina la Mzee Small amefariki dunia usiku wa leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu. Akithibitisha taarifa ya kifo cha Mzee Small, mwanae aitwae Mahmoud amesema mzee wake amefikwa na mauti hayo majira ya saa nne usiku wakati akiwa hospitalini hapo akiendelea kupatiwa matibabu. Mipango inafanyika nyumbani kwao Tabata na kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia tutaendelea kujulishana. Ni pigo lingine tena kwenye tasnia ya sanaa baada ya kuondokewa na wasanii na kadhaa majuma yaliyopita.

CHANZO: KAJUNASON BLOG

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

CELEBRITY: SHANIA TWAIN ANATIMIZA MIAKA 53 LEO AGOSTI 28, 2018

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

WAFAHAMU MATAJIRI 10 WA TANZANIA MWAKA 2018

FAHAMU MAMBO HAYA 20 KUHUSU TANZANIA

KANSELA ANGELA MERKEL ASEMA UJERUMANI YA SASA NI BORA ZAIDI