KOCHA NOOIJ ASEMA HATOPANGUA KIKOSI CHA TAIFA STARS

KOCHA mkuu wa timu ya soka ya taifa ‘Taifa Stars’, Mholanzi Mart Nooij amesema kamwe hatakifanyia marekebisho kikosi chake kilichotinga raundi ya pili ya kuwania kushiriki fainali za Mataifa Afrika kwa kuifunga Zimbabwe jumla ya mabao 3-2. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salam, Stars ilipata ushindi wa bao 1-0 kabla ya kutoka sare ya 2-2 na wenyeji wao Zimbabwe Jumapili iliyopita Jijini Harare na kukata tiketi ya kucheza raundi hiyo ya pili na sasa itakutana na Msumbiji Julai 18. Akizungumza baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Harare juzi usiku, kocha huyo alisema: “Mechi na Zimbabwe ilikuwa nzuri na ngumu kwetu, lakini nawapongeza vijana wangu walicheza kwa kujituma na kupata matokeo ambayo yametupeleka hatua nyingine, tuna muda mrefu kabla ya kucheza mechi inayofuata nitatumia muda huu kukirekebisha kikosi changu lakini siwezi kukibadilisha,” alisema Nooij. Akiuzungumzia mchezo wao unaofuata dhidi ya Msumbiji aliyowahi kuifundisha siku za nyuma, Nooij alisema ni timu ngumu yenye wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa Ulaya na Afrika, lakini anayajua vyema mapungufu yao na atayatumia ili kuweza kuiondosha kwenye kinyang’anyiro hicho kama ilivyokuwa kwa Zimbabwe. “Hakuna asiyejua kama Msumbiji ni timu nzuri ina wachezaji wengi wenye uzoefu kutokana na kucheza soka Ulaya na wengine kwenye klabu kubwa Afrika, lakini hilo halinipi wasiwasi kwa sababu nawajua vyema wapinzani wetu na Watanzania watarajia kupata matokeo mazuri,” alisema Nooij. Nooij alisema kitu kikubwa ambacho angependa kulishauri Shirikisho la soka Tanzania (TFF) ni kuiandaa timu mapema, ikiwa ni pamoja na kupata mechi za kirafiki za kimataifa ambazo zitawasaidia kujua mapungufu na uwezo waliokuwa nao kabla ya kuwavaa Msumbiji. “Itafurahisha kuanza maandalizi mapema kwa sababu tutapumzika muda mrefu na kwa vile hakuna ligi kwa sasa, lengo ni kutaka kujifunza zaidi uwanjani na kupata mechi za majaribio ambazo zitarudisha ari ya vijana wangu kabla ya kumenyana na Msumbiji,” alisema Nooij. Nooij, kocha mwenye uzoefu mkubwa na soka la Afrika, alianza kuifundisha Stars miezi mitatu iliyopita akichukua nafasi ya Kim Poulsen, siku za nyuma kuanzia mwaka 2007 hadi Septemba 2011 alikuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Msumbiji na kuiongoza kwenye michuano ya Mataifa Afrika yaliyofanyika Angola na timu hiyo kumaliza ya mwisho kwenye kundi lake baada ya kufungwa michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja.

Comments

Popular Posts

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

BIBI WA MIAKA 85 AKAMATWA KWA KUIBA HERENI

MAMBO YA MUHIMU KUFAHAMU NA KUZINGATIA KABLA YA KUCHAGUA KOZI (TAALUMA) CHUO KIKUU