BADO HALI INATATANISHA BRAZIL KUHUSU USAFIRI: MGOMO BADO UNAENDELEA KWA KASI

Wafanyikazi wa usafiri wa mjini Sao Paulo wamepiga kura kuidhinisha mgomo wao uendelee kwa muda usiojulikana licha ya uamuzi wa mahakama ya kazi nchini humo, iliyokuwa imewaamuru wafanyikazi hao kurudi kazini mara moja.

Mahakam ilikuwa imesema wakuu katika vyama vya wafanyikazi hao wa usafiri wa mjini Metro, walikuwa wametumia mamlaka yao vibaya kwa kuanzisha mgomo tangu alhamisi iliyopita.

Maandamano mengi yamekuwa yakulalamikia hali ngumu ya usafiri lakini sasa wafanyikazi wa treni za mijini ziitwazo Metro ndio waliogoma kutaka nyongeza ya mishahara. Huku nusu ya vituo vya usafiri vikiwa tayari vimefungwa, msongamano wa magari umezidi kuizonga Sao Paulo. 

Sasa wasiwasi unaongezeka, wa Je hali ikiendelea hivyo itakuaje hapo alhamisi wakati jiji hilo ndilo linafungua dimba hilo? Wafanyikazi hao wanadai nyongeza ya mshahara ya asilimia 12 ilhali serkali imesema itamudu nyongeza ya takrban asilimia 9.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017