KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: BLATTER AWASILI BRAZIL NA KUKUTANA NA RAIS WA NCHI HIYO, DILMA ROUSSEFF

Rais wa FIFA, Joseph S. Blatter amekutana na Rais wa Brazil, Dilma Rousseff huko Palacio do Planalto, Brasilia. Kwa msisimko wa kihistoria wa kombe hilo ambalo litatolewa kwa bibngwa wa dunia, kombe hilo limetolewa na Blatter na Cafu aliyekuwa nahodha wakati Brazil ilipotwaa kombe hilo mwaka 2002. 

"Nilishasema kabla ya kuja Brazil, kwa mara ya kwanza itakuwa ni kuonana na Rais wa nchi hii. Hii yote ni kwa heshima na taadhima" alisema Blatter kabla ya kuanza kwa sherehe ambapo Rais Rousseff aliinua juu kombe la dunia ambalo huguswa na Marais na mabingwa pekee.

"Ni matumaini yangu na Wabrazil wenzangu zaidi ya milion 200, wanategemea hapo tarehe 13 Julai zaidi ya watu 23 wataweza kuligusa kombe hili" alisema Rousseff.Siku 10 kabla ya michuano kuanza.

Rais Dilma alishaitisha mkutano huko Brazil na wakuu wa majimbo kujadili juu ya mechi ya maandalizi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia huko Palacio do Planato katika dimba la Arena de Sao Paulo. Baada ya sherehe za ufunguzi Blatter na Rais Dilma walihudhuria mkutano na waandishi wa habari ambapo pia alikuwepo Waziri wa Michezo wa Brazil, Aldo Rebelo. 

Mwishoni mwa mwezi Januari Rais Blatter aliwkaribisha wakuu wa majimbo ya Brazil makao makuu ya FIFA huko Zurich."Ni matumaini yangu kwa zadi ya mwezi mmoja macho yote yataelekezwa Brazil katika kombe la dunia" alisema Blatter

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017