KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: MADEREVA WA UMMA WAGOMA NA KUANDAMANA BRAZIL

Maafisa wa polisi nchini Brazil wametumia gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji katika siku ya pili ya mgomo wa wafanyikazi wa sekta ya uchukuzi ambao umesababisha uhaba mkubwa wa usafiri wa uma katika mji wa Sao Paulo. 

Takriban nusu ya vituo vya treni vilifungwa na kusababisha msongamano mkubwa wa watu katika barabara za mji huo mkubwa ambao unatarajiwa kuandaa michuano ya kombe la dunia kuanzia alhamisi ijayo.

Wafanyakazi hao wa treni wanataka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia kumi. Awamu nyingine ya majadiliano imefeli na wafanyikazi hao wanasema kuwa mgomo huo utaendelea kwa mda usiojulikana.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

WALIOCHAGULIWA CHUO CHA MIPANGO MAJINA HAYA HAPA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

VALENTINE DAY'S QUOTES

DIAMOND AISIFIA NGOZI YA WEMA ASEMA INA MVUTO NA INANG'ARA KULIKO KITU CHOCHOTE

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIUME WENYE MVUTO KOREA 2017