ETI LLULU NA NANDO WA BIG BROTHER NI WAPENZII

Mambo hadharani! Uhusiano wa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa 2013, Amir Nando umewekwa kweupe. Kabla ya wawili hao kufunguka, kulikuwa na madai mazito kuwa Lulu na Nando ‘wanachepuka’ mara tu baada ya Nando kutolewa BBA kwa ukosefu wa nidhamu. Kuna habari kuwa Nando ndiye aliyevujisha ishu hiyo, jambo ambalo Lulu hakupendezwa nalo hivyo kumpiga chini. Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, gazeti hili lilimtafuta Nando ambaye mwanzoni alifanya kama utani akidai Lulu ni mwanamke anayefaa kuolewa (wife material) lakini alipoulizwa kwa msisitizo, alikana kuwa na uhusiano na mrembo huyo. “Lulu ni mkali, niko tayari kumuoa lakini sijamwambia, akikubali freshi nitamuoa. Kwa sasa ni mshikaji wangu tu na napenda kazi zake. Huwa ni mtu ambaye napenda kufuatilia ishu zake,” alisema Nando. Kwa upande wake Lulu alishtuka na kudai kuwa aulizwe huyohuyo Nando na si yeye kwani haoni sababu ya yeye kuulizwa. Alifunguka: “Hebu muulizeni Nando kama ni Lulu mimi au mwingine? Yeye akishatoa jibu sina la kusema.” Chanzo: UDAKU SPECIALLY

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017