KUELEKEA KOMBE LA DUNIA: FIFA YATANGAZA IMANI KUHUSU MICHUANO HIYO BRAZIL

Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa amesema kuwa ana imani kuwa kombe la dunia nchini Brazil litakuwa na ufanisi mkubwa. Bwana Sepp Blatter ametoa wito kwa raia wa Brazil wajitolee vilivyo kusaidia kufanikisha mchezo huo mwaka huu.

Matamshi ya Bwana Blatter yamekuja huku hofu ikielezewa mjini Sao Paulo juu ya msongamano mkubwa wa watu na magari kufuatia mgomo wa wafanyakazi wa shirika la reli. Maafisa wakuu wa Fifa wenyewe walikwama katika foleni ndefu ya magari barabarani. Usafiri huo unatarajiwa kutatizika zaidi kufuatia kuvunjika kwa mazungumzo kati ya muungano wa wafanyikazi hao na serikali. 

Orodha kamilifu ya timu zitakazoshiriki michuano ya Kombe la Dunia imetolewa. Majina ya makocha 32 ambao watasimamia mechi za mashindano hayo, pia majina ya wachezaji 736 watakaoshiriki mechi hizo zitakazochezwa kati ya Juni 12 hadi Julai 13 zimetangazwa.. Taarifa zaidi iliyotolewa ni kuwa timu zimepunguza idadi ya wachezaji, majeraha kukaguliwa na hali ya afya ya wachezaji kutathminiwa. Haya yote yakiwa ni matayarisho kwa michuano hayo yatakayo anza jijini Sao Paulo. Timu zote zimetayarisha wachezaji 23 ambao kwa sasa watazingatia uwezo wa kufanikisha timu zao.

Comments

Popular Posts

ZIFAHAMU NCHI ZINAZOZUNGUMZA KISWAHILI BARANI AFRIKA

MKUTAO WA G7 KUANGAZIA USALAMA NA MAZINGIRA

HISTORIA YA KOMBE LA DUNIA TANGU 1930, WAANDAAJI & WASHINDI

CHEKI PICHA HIZI ALIZOWEKA NICKI MINAJ INSTAGRAM

RAIS MTEULE WA MISRI EL SISI ATAAPISHWA LEO HII

MICHAEL JACKSON-HUMAN NATURE SONG LYRICS

SELECTED APPLICANTS TO JOIN MWENGE CATHOLIC UNIVERSITY (MWECAU) 2018/2019 ROUNDS 1 & 2

IFAHAMU ANDROID NOUGAT VERSION 7

WAFAHAMU WAIGIZAJI 10 WA KIKE WA KOREA AMBAO NI WAREMBO KWA MWAKA 2017